Masoko ya Mbeya yanachomwa na serikali ya Jiji?

Diehard

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
467
347
Nikiwa katika kipindi hiki cha Noeli kama wengine wasemavbyo nilibahatika kupita katika jiji la Mbeya, nilivutiwa kutembelea jiji hili kwani niliwahi kuishi huko miaka ya 80.

Kubwa lililonitatiza ni kuhusiana na masoko mawili makubwa yaliyoungua.

Soko la mwanjelwa niliwahi kujipatia mitumba enzi hizo liliungua Desema 2006 na soko kuu la uhindini hapa nilikuwa napata nyama choma uwanja wa fisi liliungua Desemba 2010.

Cha ajabu masoko yoyte baada ya kuungua serikali ya mkoa na ile ya halmashauri ya jiji zimetoa amri na marufuku ya kuwazuia wafanyabiashara kukarabati au kuendelea na biashara katika maeneo husika.

Jambo hili limewaacha wafanyabiashara ndogondogo pamoja na wale wafanyabiashara kubwa wasijue pa kwenda kwani maeneo mbadala hayajatengwa kwa wao kufanyia biashara.

Ikumbukwe hapajakuwa na taarifa rasmi ya nini vyanzo vya moto huo.

Swali ni je ni serikali ndio chanzo cha moto huo maana inaonyesha kila moto ukitokea polisi huwepo standby na kuwaibia walengwa ipasavyo, na pia yaonyesha kila moto ukiunguzwa ndio matumizi mbadala ya masoko hujitokeza.

Wito wangu kwa wanahabari za kichunguzi kujaibu kutuchunguzia sakata hili.
 
Kuna kijana mmoja anaishi mbeya nilikutana naye mwaka jana mwezi wa 12 akanambia wafanya biashara wa soko la mwanjelwa waliambiwa wahame ili soko hilo lijengwe upya wakagoma baadaye soko likaungua na hata Juma akukweti alipokwenda huko kutoa pole inasemekana aliwaambia wafanya biashara kwamba waliambiwa wahame siku nyingi nao hawakusikia matokeo yake soko likaja kuwaka moto. Kauli hiyo iliungwa mkono na mwandishi aliyeambatana na waziri huyo. Mtoa habari wangu kaniambia baada ya kutoa kauli hiyo wafanyabiashara walikasirika sana wakasema asubiri huko anakokwenda aone kama atafika salama. Hatimaye waziri Akukweti alipata ajali tarehe 16 December 2004 na kufariki tarehe 4 january 2007. Sijui kama kuna uhusiano kati ya maneno ya waziri Akukweti na maneno ya wafanyabiashara wa soko la mwanjelwa.
 
inawezekana. na sasa wameambiwa wauwe kitimoto zooote eti ugonjwa wa homa ya nguruwe! imeanza leo baada ya uchaguzi?
 
Jirani zangu wa mbeya poleni mungu atawalipa maana wanaofanya hiyo shughuli watakuja kujistukia siku moja wanaropoka tu nyie ngojeni.
 
Back
Top Bottom