SoC03 Masoko kimtandao na kidigitali nchini Tanzania

Stories of Change - 2023 Competition

Mamshungulii

Senior Member
May 3, 2023
124
66
Nchini Tanzania kama ilivyo sehemu nyingi duniani mitandao ni kitu kilichoshika kasi,na maisha yetu kwa sasa yametawaliwa na mitandao,kabla yakuona soko mtandao tujifunze kidogo kuhusu DIGITALI

DIGITALI NI NINI?
Hili linamaanisha kitu au teknolojia ambayo hutumia tarakimu badala ya ishara za analogi ,kkuhifadhi ,kutuma na kusindika Habari.

UJUZI WA KIDIGITALI?
• Ni ujuzi unaojumuisha uwezo wa kutumia vifaa vya kidigitali ,programu tuishi za mawasiliano ,na mitandao kufikia na kutumia taarifa.

• Mfano ANALOGI hutumia sauti za mawimbi ambayo yanaweza kurekodiwa kwa njia ya kumbukumbu ya mkanda ,wakati sautii ya dijiti ,inawakkilishwa kwwa nambari ambazo zinaweza kuhifadhiwa kwenye faili dijiti.

• Teknolojia za dijiti hutumika kwa kkiasi kikubwa katika Maisha ya kila siku ,kama vile simu za mkononi, komputa, mtandao wa intaneti na vifaa vingine vya kielektroniki.

• Teknolojia hizi zimeleta mabadiliko kwa njia tunazofanya kazi,kujifunza na kuwasiliana.

• Katika karne ya 21 stadi zakidigitali ni ujuzi wa muhimu na unaozidi kuongezeka umuhimu kila siku.

• Ukuaji wa teknolojia za kidigitali unazidi kubadilisha midfumo ya kidunia katika Nyanja zote ;kijamii,kisiasa na kiuchumi.

• Ukuaji wa teknolojia za kidigitali unaifanya dunia kuunganika Zaidi kufuatia ukuaji wa njia ya mawasiliano ya kidigitali.

• Hii inafanya mtu yeyote anayeishi katika kizazi cha karne ya 21 kulazimika kuwa na angalau stadi za kawaida za digitali.

A. UJUZI WA TARAKILISHI (KOMPYUTA) NA SIMU ZA RUNUNU (SIMU ZA MKONONI)
i. Ujuzi wa kawaida wa kompyuta na simu unajumuisha:

• Uwezo wa kuwasha na kuzima
• Uwezo wa kuandika
• Uwezo wa kujiunga kwenye mtandao/matumizi ya intaneti
• Uwezo wa kung’amua matumizi ya aplikesheni na programu mbalimbali zitakazo kuwezesha kutafuta taarifa ,kupakia na kupakua maudhui mtandaoni.
• Mtu yeyote mwemnye lengo la kkufanya matumizi bora ya teknolojiaza kidigitali anpaswa kujifunza na kujenga utamaduni wa kuendeleea kuongeza ujuzi wa kompyuta na simu hasa kwa kuzingatia teknolojia inakua kila siku.

ii. Ujuzi wa kuhariri
Ujuzi wa kuhariri ni uwezo wa kuvunjavunja au kuchuja maudhui mbalimbali kwa namna ambayo yataweza kuwasilisha ujumbe husika kwa ufanisi.Ujuzi huu unahusisha uwezo wa kupitia maudhui ya maandishi ,au picha ,au video au sauti na kuyaweka katika namna inayomvutia mtumiaji.

UJUZI HUU UNAJUMUISHA:
  • Uwezo wa kutumia aplikesheni mbalimbali za kuhariri
  • Uwezo wa kuchakata maudhui kwaajili iya majukwaa mbalimbali
  • Uwezo wa kusanifu maudhui

Ni muhimu kwa mjasiriamali kuwa na ujuzi wa namna ya kuhariri maudhuii ili kurahisisha msawasiliano yake ya masoko.

iii. Ujuzi wa uandishi wa kibunifu
Ubunifu ni sarafu muhimu katika mawasiliano ya kidigitali .Mjasiriamali anapaswa kukuza ujuzi wake wa uandishi wa kibunifu kwa lengo la kuongeza uf\anisi katika mawasiliano ya kidigitali.

Ujuzi wa uandishi kibunifu unajumuisha
  • Uwezo wwa kufanya utafiti
  • Uwezo wa kuandika kwa kuzingatia mpangililo sahihi wa lugha na sarufi
  • Uwezo wa kufanya uchambuzi na kutambua aina ya watumiaji wa majukwaaa ya mtandaoni na aina ya maudhui yanayowafaa.

iv. Ujuzi wa kuzalisha na kuandaa maudhui
Ujuzi wa kuzalisha maudhui unahusisha uwezo wa kuandaa maudhui kama picha ,video,maandiko na maudhui ya sauti.

Majukwaa ya digitali ni kama gari na maudhui ni kama mafuta yanayowezesha gari kutembea,hivyo, ni muhimu kwa mjasiriamalli kuwa na uwezo wa kuzalisha maudhui ili kufanikisha mawasiliano ya masoko kidigitali.

UJUZI WWA KUZALISHA MAUDHUI UNAJUMUISHA
  • Uwezzo wa kuandika
  • Uwezo wa kuandaa mwongozo wa ukkusanyaji maudhui
  • Uwezo wa kutumia vifaa vyaa kurekodi maudhui kama vile simu,kamera,virekodia sauti na drone .

v. Ujuzi wa ulinzi na usalama mtandaoni
Ujuzi wa ulinzi na usalama mtandaoni ni uwezo wa kung’amua hatari zinazpotokana na matumizi ya teknolojia za kidigitali na kkuzingatia tahadhari kwa lengo la kuongeza ufanisi. Mjasiriamali anapaswa kuwa makini na kutambua kwamba hatari mbalimbali mtandaoni zinaweza kutokea na kuathiri biashara yake.

Hatari kama wizi wa fedha,utapeli,udukuzi, na wizi wa taarifa za kibenki na za kibiashara zinaweza kutokea katika matumizi ya kidigitali.

UJUZI WA ULINZI NA USALAMA MTANDAONII UNAJUMUISHA
  • Uwezo wa kuweka nywila katika vifaa vyako vya kidigitali
  • Uwezo wa kutunza kwa usiri taarifa za muhimu za kurasa zako
  • Uwezo wa kubainisha hatari na kutambua hatari hizo
  • Uwezo wa kufahamu taratibu na miongozo kuhusu maudhui ya mtandaoni
  • Namna ya kutumia au kuepuka kutumia Brand kubwa za watu kama vile TATA,DIOR

vi. Ujuzi wa kutumia taarifa za mtandaoni
Hii inahusisha uwezo wa kuchakata na kutumia taarifa unazozipata mtandaoni kupanua wigo wa matumizi ya mtandao na kuboresha mbinu nyingine kama uzalishaji na usambazaji wa maudhui .kupitia majukwaa mbalimbali ya kidigitali unayoyatumia kama mjasiriamali unaweza kupata taarifa kama taarifa kuhusu mambo wanayopendelea wafuasi wako,kundi rika ,jinsia ,jiografia.

MJASIRIAMALI UNAPASWA KUHAKKIKISHA UNA UWEZO WA KUCHAMBUA TAARIFA HIZO NA KUZITUMIA KWA MANUFAA YA BISASHARA YAKO MTANDAONI:
Ujuzi wa kutumia taarifa mtandaoni unajuhusisha:-
  • Uwezo wa kukusanya taarifa
  • Uwezo wa kuchakata na kuchambua taarifa
  • Uwezo wa kupambanua taarifa husika

KWA KUMALIZIA
Stadi za kidigitali ni stadi ambazo hutegemeana, jinsi mtumiaji anavypopata stadi nyingi Zaidi ndivyo anavyojitengezea uwezekano wa kutumia majukwaa ya kidigitali kwa ufanisi Zaidi.

Ni muhimu kwa mjasiriamali na mfanyabiashara kujifunza stadi hizi ili kuimarisha uwezo wako wa kuutumia kwa ufanisi Zaidi majukwaa ya kidigitali kufanikisha shughuli zake za masoko mitandaoni.

Mjasiriamali asipokuwa na stadi hizi itambidi kugharamika kuwalipa watu wenye stadi hizo ili kufikia malengo.

20230525_180403-BlendCollage.jpg
 
Back
Top Bottom