Maslahi ya Waisrael yawachanganya MENGI na SAKINA DATOO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maslahi ya Waisrael yawachanganya MENGI na SAKINA DATOO

Discussion in 'Celebrities Forum' started by omarilyas, May 28, 2009.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kuna taarifa kuwa maslahi ya Waisrael ndiyo chanzo cha aliyekuwa mhariri mtendaji wa magazeti ya IPP kama The Gurdian, Nipashe, Alasiri na mengineyo mwanadada Sakina Datoo kulazimika kuachia ngazi.

  Inasemekana kuwa Mzee Mengi aliamua kumshusha cheo Sakina kwa kumpeleka kuwa mhariri wa gazeti lisilokuwepo la Thisday on Sunday mara baada ya kubanwa na mashushu wa kisrael ambao kwa miaka kadha sasa wamekuwa wakifanikisha michongo mbalimbali ya kibiashara na misaada katika vyombo vyake vya habari kufanya hivyo. Hii ilifuatia kitendo cha Safina kumpokea Balozi Mpya wa Palestina ambaye alimgongea ofisini kwake kumsalimu na pia kumpa makala yake ambayo ilitoka katika gazeti mojawapo la IPP Media.

  Inasemekana kuwa wakati Mengi amekuwa akijionyesha kuwa karibu na watu wa Palestina lakini ukweli Mengi amekuwa akitegemea sana misaada mbalimbali ikiwemo ya kiulinzi kutoka kwa "system" na serikali ya Israel.

  Baadhi ya wachambuzi wa kisiasa wamesema kuwa hilo si jambo la ajabu kwa Mengi kuamua kuchagua maslahi ya waisrael zaidi ya misingi ya kibinadamu na kitaifa ambayo amekuwa akijionyesha kuwa yupo mstari wa mbele kuitetea. Wanaendelea kusema kuwa iukiondoa tabia ya binafsi ya mfanyabiashara huyo mahiri inawezekana kuwa Mengi anatambua kuwa mahusiano mazuri na wababe kama Waisrael na Wamarekani ni muhimu sana kwake haswa wakati kama huu ambapo anaelekea kukosa ulinzi wa wenye kuhodhi nguvu za utawala.

  Wadau wa karibu wa IPP media wanadai kuwa shinikizo la mashushu na serikali ya israel kupitia njia za kibalozi limekuja wakati mbaya ambapo tayari pia mahusiano kati yake na Sakina yalikuwa yameharibika kutokana na Sakina kukataa kubebeshwa uongozi wa magazeti yake mengine ambayo yalianzishwa maalumu na kuendeshwa kwa minajili ya kupambana na "ufisadi" pamoja na maadui zake wa kibiashara na kisiasa.

  Inasemekana tayari Sakina Datoo ameacha kazi. Hii inakuwa mara ya pili kwa mwanadada huyu kuacha kazi kubwa kama hiyo inayompatia malipo makubwa kuzidi waandishi wengine wengi kutokana na mashinikizo yatokayo kwa wamiliki wa vyombo hovyo. Kabla ya Sakina kuajiriwa na Mengi alikuwa amejiuzulu The Citizen/Mwananchi baada ya kubanwa na wamiliki wake kutokana na taarifa aliyotoa iliyokuwa ikimpinga aliyekuwa waziri wa fedha wakati huo Bi Zakia Meghji.

  Ukweli ni kuwa ile hali ya kuibuka upya kwa magazeti ya IPP Media mara baada ya Mengi kumuajiri Sakina na kumpa kiasi cha shilingi Bilioni Moja (inasemekana kuwa Waisrael walikuwa na mkono wao katika fedha hizi) kuajiri idadi kubwa ya waandishi mahiri kutoka katika mageziti mengine imeanza kufifia.

  Baadhi ya waandishi hao mahiri waliopewa vidau vikubwa kuondoka katika vyombo walivyokuwa walimeanza kukimbia IPP Media na wengine wamekuwa wakihaha mitaani kuomba kazi za ama uandishi ama uafisa habai katika mashirika mbalimbali yakiwemo ya kitaifa na kimataifa.

  Hawa ndio masiha wetu ................

  Omarilyas
   
 2. V

  Vision2010 Member

  #2
  May 28, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ungeandika imeandaliwa na Zitto Kabwe kwa ushirikiano na Omar Ilyasi kwa kuwa financed na Rostam.

  Ndo first post yangu hapa JF lakini huu upuuzi siuachi upite hivi, heshima zenu wana JF, nimejiunga rasmi.

  Vision2010
   
 3. V

  Vision2010 Member

  #3
  May 28, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Omar, kaa mbali na Zitto, huyu si yule uliyekuwa unamfahamu awali. Angalia Tanzania Daima wenyewe wanakoelekea, kuwa makini utaelewa
   
 4. M

  Mkukuti Member

  #4
  May 28, 2009
  Joined: Feb 8, 2008
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Omar ndugu yangu mbona unajiangusha, na unatuangusha ndug zako? yaani umekuwa this low! yaani siwezi kuamini. Sasa naona unataka kupindisha ukweli na kuanza kuleta uislamu dhidi ya ubabe wa Waisrael na USA! Kijana nenda shule, achana na Zitto, yeye mwenyewe ameshapotea na sasa anataka kukupoteza nawe pia! Kua ndugu yangu.
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  May 28, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Omarilyas: Haya, tumwagie basi data za proof ya Mengi-Israel Connection na ya huyo mwanadada kukataa kutumika katika kuandika habari za kuwaponda mafisadi. Acha kukazania kusema tu 'inasemekana..., inasadikiwa..., inadaiwa etc etc. Acha udaku. Ningekuwa mods ningeifunguilia mbali thread hii ya kimajungu.
   
 6. V

  Vision2010 Member

  #6
  May 28, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapana, huu ujumbe alinitumia Sakina pia, amekosea sana Sakina. Kuna protocol za kazi, anajiamini kupitiliza.
   
 7. Companero

  Companero Platinum Member

  #7
  May 28, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,474
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mkataba wa awali kabisa wa Sakina na IPPMedia unasemaje?
   
 8. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #8
  May 28, 2009
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Omar niliisha mwambia; apunguze kujipendekeza. Wana JF hamuwezi amini, Omar amefikia hatua ya kuwabebea wahadhiri mashuhuri mikoba eti tu aonekane yuko karibu nao, anaongoza nao. Upuuuzi mtupu
   
 9. V

  Vision2010 Member

  #9
  May 28, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maneno mengi ya nini? Wala msiumize vichwa, kwenye mbio hizi wengi ni ngumu kuwaelewa, taratibu 2010 ipo mlangoni, kama ilivyokuwa 2005, vilevile kama sasa wataanza kuchafuana na kuwapoteza wengi malengo.

  Nawahakikishia, Sakina bado yupo IPP, kama mnabisha si mnaye Mwanakijiji? Ampigie simu na kuweka ukweli hapa. Zitto na usaliti wake anasikitisha, Omar: You have been warned!
   
 10. V

  Vision2010 Member

  #10
  May 28, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duuuh, tunaomjua Omar ni wengi basi. Mi sikutaka kumgusa Omar kama Omar, najua anamezeshwa na kina Zitto na mpambe wake Hussein Bashe mwana wa Rostam ambaye ndo mchonga deal za hela za kumsafisha JK.
   
 11. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #11
  May 28, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hao wengine naachana nao wanedelee na ujuha wao lakini wewe sikuwachi.....i feel very proud kubeba mikoba ya kina Shivji, Haroub Othman, Marehemu Chachage, Salim Ahmed Salim, Prof Muya.... na hata Dr Rwaitama na kaka zangu kina Bashiru na wengineo, very proud indeed.....

  Hata wazee wangu walibeba mikoba ya wale walikuwa wakiwaamini na kuwachukulia kama role models.....

  Kwa anayedhani kuwa kila nisemacho ni kutoka kwa Zitto nawaacha waendelee na ujuha wao.....

  Zitto will always be my friend, my comrade and my brother......but dont think i am that kind of friends you have in ur mind....

  Omarilyas
   
 12. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #12
  May 28, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wakati huo huo, habari nilizozipata hivi karibuni toka kwa mchunguzi wetu, Omarylas, aliyeko wizara ya mambo ya ndani ni kuwa, hivi sasa Serikali ya JK inafuatilia mambo mawili makuu juu ya Mengi;
  1. La kwanza ni kuwa, inasemekana wazazi halisi wa Reginald Mengi ni wazungu, (uhakiki wa DNA serikali wanao), ingawa walishindwa kuelewa ilikuwaje Mengi akawa na sura ya Kiafrika. Mama yake ni, Magareth Thacher, ambaye ni Mwiingereza na baba yake ni, Ariel Sharon, ambaye ni Mwiisrael.
  2. Ugomvi wa Mengi na Rostam unatokana na wivu wa Mengi baada ya kugundua kuwa, wazazi wa Rostam sio Mag.a.b.acholi kama sura ya Rostam, bali wote ni Wasukuma, bali alinusurika kutokuwa zeruzeru, na ndio maana serikali imekuwa ikimpa upendeleo zaidi kwani hana nchi ya kukimbilia zaidi ya Tanzania, tofauti na Mengi ambaye ni mzungu anayeweza kukimbilia kwao ulaya.
  LOL.
   
 13. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #13
  May 28, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nilidhani unajijua kumbe bure kabisa...........

  Endelea na ujuha wako kudhani kuwa unachokiona magazetini, kwenye TV zao na umbeya wa kwenye vikao vyenu vya udaku wa kiume ndio ukweli wenyewe

  Omarilyas
   
 14. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #14
  May 28, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Du........

  We nakuaminia.....

  Angalao leo nimecheka kuondoa maudhi ya siku.

  Omarilyas
   
 15. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #15
  May 28, 2009
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Omar, sisemi wala sikukatazi kuwaiga role models. La asha. Katika jibu lako unajaribu kucheza na maneno kubadilisha “kubeba mikoba” kuwa kuiga wasifu na matendo ya role models. Binafsi nazungumzia tabia ya “KUJIKOMBA” kiasi cha kujidharirisha. Kama unabeba kwa kwa kufuata njia yao ili nawe siku moja uwe kama wao tueleze basi ni lipi hadi leo umelifanya la kujivunia kutokana na kubeba mikoba yao kama si “KUJIMWAMBAFAY” tu!
  Huna tofauti na wale wanaokimbilia kusema aaah Fulani Namfahamu sana, Aaagh Fulani Rafiki yangu sana (Zitto, Shivji, Bashiru, Rwaitama), mwishowe utasema aagh fulani (John Mrema) yule nimemlea mimi. Achana na adithi za kitoto za tajiri fulani nilikuwa nampenga kamasi!
   
 16. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #16
  May 28, 2009
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  I love JF.......................... Drink Fanta stay bambucha!
   
 17. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #17
  May 28, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Inaelekea nimeshika pabaya sana. Kama ambavyo manyang'au wetu hupenda kufanya wayafanyao na huku wakijidai wanatetea maslahi ya taifa, basi hata huyu MASIHA wenu naye ana yake ambayo yeye na wafuasi koko wake kamwe hawapendi yatoke nje na watu wakayajua...

  Wewe binafsi umesema kuwa Safina alikutumia msg inayohusu hayo na ukamlaumu kwa kutojua protocol. Unapozungumzia protocols ni wazi unagusia suala la balozi kumtembelea Sakina moja kwa moja bila ya kwenda kusujudia Mengi kwanza. Ina maana unalijua sana hili suala na hata kutambua EGO ya Mengi ambayo ukichanganya na mengine yamemfanya kufanya makosa Mengi ya ki-mikakati kiasi cha kuhatarisha himaya yake na kukimbilia kung'aka kuwa hao MAFISADI wake na walinzi wa ufisadi ndio wanaomuharibia.

  Kaka ni wazi unamjua na unajua mambo ya MASIHA wenu huyu ambaye kamwe hajawahi kuwa mfano bora kwa jamii tunaoutaka kutuwezesha kuondokana na mfumo fisadi unaomaliza TAIFA. Lakini kwa kuwa wewe ni mmoja wa wale wanaokubali kuchagua upande wa WATU badala ya misingi na fikira basi usingependa haya mambo yakajulikana na kuhatarisha UMAHIRI wa MASIHA wenu.

  Na kama unanijua kweli, ni wazi ungetambua msimamo wangu pale inapokuja suala la hatima ya Wapalestina na maslahi ya Waisrael....kwenye wababe na wanyonge daima nitachagua wanyonge....na hadi Wapalestina watakapokuwa wanatambulika kama binadamu kama wengine wenye haki ya kuishi na kujiamulia hatima yao katika ardhi yao, daima nitakuwa na WAPALESTINA. Na daima sitasita kuwasemea hata kama ni kuhatarisha maisha yangu ama kwenye misemo yenu takatifu mngelisema "maslahi yangu".

  Unataka kuniambia kuwa Mengi hana Biashara na Waisrael? Unataka kuniambia kuwa hakukuwa na shinikizo kwa Mengi mara baada ya balozi huyo kumtembelea Sakina na makal ile kutoka gazetini? Unataka kuniambia Mengi hana ulinzi wa Waisrael na Wamarekani? Unataka kuniambia Hawa wote hawafadhili vyombo vyake vya biashara? Unataka kuniambia kuwa Waandishi na wataalamu wa Mengi hawapatiwi mafunzo na utawala wa Waisrael?

  Kujishusha kubeba mikoba ya walionizidi kihekima, kiujuzi, kielimu, kiumri na hata kumuono kusikufanye kunichukulia kama asiyejua kinachoendelea. Nilienda shule kuelimika na sio kupata vyetu vya kuajiriwa na hao mnajidai kupambana nao....Sio wote tuliokuzwa, wengine tumelelewa...

  Najua "wasasa" kama wewe, misimamo na mitazamo kama hii haiwezi kuingia akilini mwenu lakini ukweli ndio huo.

  Kamwe sitanyamaza eti kwa kuogopa EGO na vandetta za hao MASIHA FEKI wenu....

  omarilyas
   
 18. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #18
  May 28, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Never expect this from me.....ukiambiwa basi ujuwe anayekuambia anakuona mjinga wa kutupwa...

  omarilyas
   
 19. M

  Mkukuti Member

  #19
  May 28, 2009
  Joined: Feb 8, 2008
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Omar,
  RA anafadhiliwa na nani?
   
 20. M

  Mkukuti Member

  #20
  May 28, 2009
  Joined: Feb 8, 2008
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bwana mdogo Omar,
  embu kua kidogo, unajidharirisha wewe mwenyewe, famili yako na hata marafiki zako. Madai yako dhidi ya Mengi yanaonyesha shule haijakusaidia kabisa, kwani kimpangilio wa hoja unaonyesha kabisa uwezo wa hao role model wako kuwa walishindwa kazi ya kukufundisha shule. Dogo uko shallow sio kwa hoja tu, bali hata mpangilio wa habari yenyewe, "inasemekana" au "inahisiwa". Kijana umeenda shule, mbona unaandika kama profesa "maji marefu"?
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...