Waisrael kadhaa waangamizwa katika shambulizi la kulipiza kisasi

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,992
17,892
Waisrael kadhaa waangamizwa katika shambulizi la kulipiza kisasi

Jun 21, 2023 12:08 UTC

[https://media]

Makundi ya muqawama ya Palestina yamefanya operesheni ya ulipizaji kisasi na kuwaangamiza Wazayuni wanne na kujeruhi wengine wanne karibu na Ramallah katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan linalokaliwa kwa mabavu na Wazayuni.

Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vimetangaza kuwa, shambulizi hilo la kulipiza kisasi lilifanywa jana Jumanne na Wapalestina wawili karibu na kituo cha mafuta katika eneo la Eli linalokaliwa kwa mabavu, baina ya miji ya Nablus na Ramallah.

Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Palestina (HAMAS), Hazem Qassem amesema shambulizi hilo la ufyatuaji risasi lililofanywa na mujahidina wa Palestina ni la kulipiza kisasi cha ukatili wa Wazayuni Jenin, na pia kwa kuuvamia Msikiti mtukufu wa Al-Aqsa.

Habari zaidi zinasema kuwa, makabiliano makali yameshuhudiwa pia baina wanajeshi wa Israel na wanamuqawama wa Palestina katika kambi ya wakimbizi ya Jenin na karibu na eneo la al-Jabriyat.

Operesheni hizi za ulipizaji kisasi zimejiri baada ya jeshi la utawala wa Kizayuni Israel kuua na kujeruhi makumi ya Wapalestina katika mji huo wa Jenin. Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Palestina, mbali na Wapalestina sita kuuawa shahidi katika uvamizi wa askari wa Kizayuni huko Jenin, wengine zaidi ya 40 walijeruhiwa vibaya.

[https://media]Wanamuqawama katika operesheni mjini Jenin

Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vimekiri kuwa, matukio ya huko Jenin katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan yalikuwa ya kipekee kutokana na silaha zilizotumiwa na makundi ya muqawama ya Palestina na yametoa pigo kwa jeshi la utawala wa Kizayuni

4c0t3ede67249122nx8_800C450.jpg
 
Back
Top Bottom