Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,014
- 144,372
Hivi ndivyo unavyoweza kusema na hali hii utaiona mara tu mishahara ikitoka ambapo baadhi ya watumishi humiminika katika taasisi hizi za kifedha(sio mabenki) kupeleka marejesho au kufuata mishahara yao kwani baadhi ya wanaowakopesha hukaa na kadi zao za ATM kama moja ya mashariti ya kupewa mikopo ingawa siku hizi kuna huduma za mobile banking zinazomuwezesha mtu kutoa hela kutoka kwenye akaunti yake bila kwenda benki wala kutumia kadi yake ya ATM.
Ukiacha hizi financial institutions ambazo nazo hutoza riba kubwa,kuna watu binafsi nao ambao hufaidika na matatizo ya watumishi kwa kuwapa mikopo yenye riba kubwa inayofikia hadi asilimia 20 mpaka 30 ya mkopo mtumishi anaokopeshwa.
Mfano, kila shilingi 100,000/=,wanatoza riba ya asilimia 20 hivyo wanaokopa shilingi 100,000/= kwa mwezi,mwisho wa mwezi wanarudisha shilingi 120,000/=, na wanaokopa shilingi 500,000/=, mwisho wa mwezi wanarudisha shilingi 600,000/=.Kwa wale wenye wateja wengi,hakika hii ni biashara nzuri sana ingawa ina changamoto zake tena isiyo na kodi wala leseni ya biashara.
Hii mikopo imepewa jina la mikopo ya dharura ingawa kiuhalisia sio ya dharura bali ni ya kujaribu kupambana na hali ngumu ya maisha inayochangiwa na masilahi duni ya watumishi inayowakabili watumishi na hata wasio watumishi maana baadhi ina makato ya kufikia mpaka miezi 6 na zaidi.
Kumbuka mikopo hii ni mbali na ile ya mabenki ambayo mtumishi hukatwa moja kwa moja kwenye mshahara wake hivyo jiulize mtumishi huyu anabaki na kiasi gani na hapa ndio huwa nakumbuka ule msemo: "mtanzania anaishi kwa mbinu."
Ukweli ni kwamba hata ilie sheria/utaratibu wa kutaka kila mtumishi abaki na angalau moja ya tatu ya mshahara wake baada ya makato yote,sheria/utaratibu huu umebaki nadharia tu kwa baadhi ya watumishi na binafsi sioni hata umuhimu wa hii sheria kuendelea kuwepo bali ni bora tu ikafutwa na mtumishi abaki huru katika kuamua matumizi ya mshahara wake.
Kwa hakika watumishi wa umma,kama ilivyo kwa raia wengine,wanahitaji mkombozi/meteztei vinginevyo huko mbeleni hali inaweza kuja kuwa mbaya sana kwa baadhi ya watumishi.
Ama hakika karibu kila kitu ni fursa yakiwemo na matatizo ya watu wengine.