Maskini vijana wa CCM mitandaoni, utawahurumia

Maskini vijana wa CCM mitandaoni, utawahurumia

Unapigana na Mtu unamwambia asitumie Kisu kwa kuwa Wewe huna Kisu! Pambana na Wewe umiliki Panga sio kulia lia Eti usitumie kisu
Tukileta vifaru vyetu patakalika hapa ? Unashadadia vita ili iweje ?
 
Mbona tume ya uchaguzi zanzibar ilitengua matokeo ya uchaguzi?na uchaguzi ukarudiwa.
Ndio maana mleta mada anashangaa akili zenu! Kama zingekuwa timamu huwezi kuuliza jambo kama hilo.
Lakini sishangai, nilisoma mahali kwenye makundi wa WhatsApp ya ccm naibu waziri wa Ardhi Mama Mabula akiwa ameandika kuwahamasisha vijana wajitokeze kujibu mapigo yanayo elekezwa ccm na akawaahidi wasiwe na hofu utaratibu wa kuwaona (in terms of airtime bundles) umeandaliwa.
Ndipo nikaamini yale mambo ya Buk7 team
 
Mbona tume ya uchaguzi zanzibar ilitengua matokeo ya uchaguzi?na uchaguzi ukarudiwa.
Ni mgombea gani kule Zanzibar alilalamikia matokeo au rafu za uchaguzi hata kupelekea kufutwa kwa matokeo yale? Nani alipeleka malalamiko yake kwenye tume? Sbb sheria haziruhusu any petition mahakamani. M/mkiti na wajumbe wengine walimkana Jecha kwamba yale yalikuwa maamuzi yake binafsi hakuwashirikisha wajumbe wenzake. On top of that Jecha, constitutionally hana hiyo power /mandate ya kufuta matokeo ya uchaguzi. Kenya NASA wameenda mahakamani, petition imefanyika in accordance to their new constitution requirements na yakatokea yaliyotokea. Hapa kwetu kila kitu ni sanaa tu. Kosa yote ila sio fikra.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
.....
.....Makofi tafadhali...kwakwakwa .. hapondoo mwishowao wa maarifa
 
Uhuru atashinda tena , lakini tunachoshangilia sisi ni uhuru wa Mahakama ya Kenya , hii inatokana na nchi hiyo kuwa na Jaji Mkuu kamili , siyo Kaimu .
Jaji Mkuu kamilo ndiyo analeta nini? Mahakamani Ni ushahidi Na Sheria tu hata tukikuweka wewe
 
Mnanishangaza nyie maana mmekosa cha kusema, mmebaki kuishambulia CDM...

Kinachonishangaza na kuniskitisha ZAIDI ni NYIE (CCM) MLIOIKATAA RASIMU YA WARIOBA YENYE KIPENGELE CHA KUHOJI MATOKEO YA URAISI MAHAKAMANI, ETI mnatoa pongezi kwa mahakama ya Kenya... UNAFIKI ULIOTUKUKA
Lowassa wenu aliitaa hiyo rasimu Na mpaka leo mmeshindwa kumuhoji
 
Yaani wamejikita kuishambulia CHADEMA na Lowassa wao kwa yaliyotokea Kenya, vijana wa watu hawaelewi kua haki inayotolewa na mahakama za Kenya haipo Tanzania. Hawa vijana hawajui kabisa leo hii Raila Odinga angekua nchini mwetu hiyo haki asingeipata.

Sijui hawa vijana wana matatizo gani! Labda nieleweshwe vizuri nami nifahamu, tatizo ni elimu? Uelewa wa nmna ya kung'amua mambo? Wamekaririshwa? maisha magumu? Ningeomba watitokeze tu humu humu waseme tu wao wenyewe. Vinginevyo kama ndio mawazo yao haya, tusitegemee uhai wa CCM kabisa siku za usoni.Is this a CCM upcoming new generation?

Badala ya wao kumshauri mwenyekiti wao wa chama taifa wakae waone namna ya kubadilisha katiba ya nchi hivi sasa ili siku moja haki itendeke kwetu kama Kenya badala yake Wamejikita kuishambulia CHADEMA na Lowassa wao, mashsbulizi haya yana madhara gani kwa CHADEMA? Yana faida gani upande wa CCM?

Bado uchaguzi wa Kenya umeamriwa kurudiwa kwa muda wa Siku 60, Je,akishinda tena Uhuru Kenyatta ikiwa bado CHADEMA watendelea kuwaunga mkono muungano wa Jubilee itakuwaje? Bado wataachana na ajenda za kitaifa na kubaki kushambuliana na CHADEMA?


Ni aibu na fedhera kwa kwa vijana wanaoitwa vijana wa Chama tawala kuhangaika mambo ya ajabu ajabu wakiachana na mambo ya muhimu na majukumu waliyonayo. Au wengine hawa wengine ni wafuasi tuu lakini sio wanachama wa CCM ndio maana hawaelewi watendayo?

Kwa fikra hizi, Mwanadishi na Wakili msomi Jenerali Ulimwengu amesema itatuchukua miaka 40 kuyafikia maendeleo ya nchi ya Kenya iwe kisiasa,kielimu,kiuchumu na hata kijamii.
Nimependa sana hoja yako mkuu,ila nitapingana kidogo tu. Kwa heshima kabisa tuondoe ccm tuweke Tanzania. Hili tatizo la uelewa(perception) ni kubwa mno na ni la kitaifa kuliko kichama. Mabadiliko endelevu ni kitu bora zaidi kwa binadamu wote,,hivyo tunapaswa kushiriki kikamilifu pasipo visingizio vya vyama. Lililo zuri Kenya linaweza lisiwe zuri Tanzania,muhimu ni kujenga hoja siyo kukopi kwa wakenya.Kenya ipo East Africa sawa lakini muundo wake kiutamaduni na kisiasa ni tofauti sana na Tanzania. Yapo mazuri wanayo lakini siyo excellent kivile, personally nisingependa sana kuishi nchi yenye kiwango kile cha ukabila,wako mbele kiuchumi pia ila mafukara wao ni zaidi ya mafukara,hivyo tinapojaribu kuchambua tuwe specific zaidi with a good rationale kuliko kusema tu vijana wa ccm fanyeni hivi ili tupate vile.
NB isipokuwa kama uzi wako ni propaganda za kisiasa naomba kuishia hapo..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom