Maskini vijana wa CCM mitandaoni, utawahurumia

Maskini vijana wa CCM mitandaoni, utawahurumia

Ukawa: Tanzania hakuna Demokrasia, si unaona Wakenya wamefuta matokeo ya Urais,Haijawahi kutokea Afrika nzima...
1f44d.png
Mzalendo: Afrika? Mbona hata hapa Tanzania matokeo ya Urais yameshafutwa na Jecha kule Zanzibar kama yalivyofutwa na Maraga kule Kenya
1f918.png
Ukawa: Matokeo Tanzania yakifutwa ni kwa maagizo toka juu na sio Mahakamani
1f44d.png
Mzalendo: Hata Yale ya Jana ya Ubunge wa Longido ni maamuzi toka juu? Au ni maamuzi toka Mahakamani?
1f918.png
Ukawa: Kwanza Mahakama zetu hazipo huru, ni kupendeleana tu.
1f44d.png
Mzalendo: Unataka kusema hata ile kesi ya Bulaya wa Chadema kumshinda Wasira wa CCM Ubunge wa Bunda ilijaa upendeleo? Mahakama haikuwa huru kuamua?
Ukawa: Basi yaishe mi ni NYUMBU wa Mbowe napiga vuvuzera na kuongea nisiyoyajua nimekumbuka hata Lijualikali na Suzan Kiwanga walishinda ubunge wao na mahakama ikabariki
1f6b6_200d_2642.png
Twaweza walikuwa sahihi sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu naona hukulala vizuri
Kunywa sleeping pills upate kuichangamsha akili yako ukiamka.
Mada haina mashiko wala mantiki.
Kenya na CCM wapi na wapi?
Rudia ena na tena ku correlate ideas zako uje na mada liyoenda shule!!
Unataka jibu gani sasa? Kama huna hoja waweza pita tu mkuu.
 
Yaani wamejikita kuishambulia CHADEMA na Lowassa wao kwa yaliyotokea Kenya, vijana wa watu hawaelewi kua haki inayotolewa na mahakama za Kenya haipo Tanzania. Hawa vijana hawajui kabisa leo hii Raila Odinga angekua nchini mwetu hiyo haki asingeipata.

Sijui hawa vijana wana matatizo gani! Labda nieleweshwe vizuri nami nifahamu, tatizo ni elimu? Uelewa wa nmna ya kung'amua mambo? Wamekaririshwa? maisha magumu? Ningeomba watitokeze tu humu humu waseme tu wao wenyewe. Vinginevyo kama ndio mawazo yao haya, tusitegemee uhai wa CCM kabisa siku za usoni.Is this a CCM upcoming new generation?

Badala ya wao kumshauri mwenyekiti wao wa chama taifa wakae waone namna ya kubadilisha katiba ya nchi hivi sasa ili siku moja haki itendeke kwetu kama Kenya badala yake Wamejikita kuishambulia CHADEMA na Lowassa wao, mashsbulizi haya yana madhara gani kwa CHADEMA? Yana faida gani upande wa CCM?

Bado uchaguzi wa Kenya umeamriwa kurudiwa kwa muda wa Siku 60, Je,akishinda tena Uhuru Kenyatta ikiwa bado CHADEMA watendelea kuwaunga mkono muungano wa Jubilee itakuwaje? Bado wataachana na ajenda za kitaifa na kubaki kushambuliana na CHADEMA?


Ni aibu na fedhera kwa kwa vijana wanaoitwa vijana wa Chama tawala kuhangaika mambo ya ajabu ajabu wakiachana na mambo ya muhimu na majukumu waliyonayo. Au wengine hawa wengine ni wafuasi tuu lakini sio wanachama wa CCM ndio maana hawaelewi watendayo?

Kwa fikra hizi, Mwanadishi na Wakili msomi Jenerali Ulimwengu amesema itatuchukua miaka 40 kuyafikia maendeleo ya nchi ya Kenya iwe kisiasa,kielimu,kiuchumu na hata kijamii.

ningekuwa wewe this time....ningekaa kimya kushusha aibu kwa kutupa lawama kunadharaulisha
 
Chadema bwana mnashangilia ya watu, mbon wa zanzibar ulifutwa mkazira kurudia mwambien na best yenu azire
 
Mbona tume ya uchaguzi zanzibar ilitengua matokeo ya uchaguzi?na uchaguzi ukarudiwa.
Hii nayo haijawahi kutokea duniani! Mwenyekiti wa Tume anapoyafuta matokea HALALI aliyokwisha yatangaza kwa kufuata taratibu zote za kikatiba (na kisheria). Anaamrishwa: FUTA matokeo. Jifiche. Mpaka leo hasikiki kwenye Jamii. kenya wameshatoka toka kwenye GIZA la KIVAITU na JECHA..
 
CCM wamechukizwa sana na demokrasia ilivyoendelea kenya!Na uhuru kwasababu ameonyesha ukomavu wa kidemokrasia,atashinda kwa kishindo sana!
 
Mkuu kubishana na Misukule wa Lumumba unaweza kupasuka msamba, pale ni UKUKU tu...

Sent From Kisana Kiki Iphone
 
Kaka chama hakibadili maendeleo, bali fikra huleta mabadiliko ya maendeleo. Good lkn fikiria kwa mara nyingine ,tatizo letu mfumo wa elimu ulipo nchin umeshindwa kubadilisha au kuleta mabadiliko kwa mtz, kwamaana angalia maprofesa wetu na darasa la saba leaver kwenye hoja utagundua hakuna tofauti kwenye maamuzi, .
Hongera Livingstone, Majimarefu na Msukuma nimewaangalia hoja zao zinamashiko kuliko haya maprofesa wetu wengi

Sent using Jamii Forums mobile app
Huo mfumo ulioshindwa kuleta mabadiliko haujaundwa na chama tawala ccm!?!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utafiti hua unatoa majibu ya ukweli mkuu.
2015 hii hii twaweza tuliipiga mawe nakusema wamehongwa wanajioendekeza kisa tuu wameonyesha kuwa ccm itashinda leo imekuaje tena ndugu yangu?
 
Ila Chadema Wenye akili wametimiza Robo Karne ( 1992-2017) bila hata ya kupata theluthi Moja ya Wabunge Bungeni wakati TANU iliwachukua Miaka 7 tu kukamata dola, ASP iliwachukua Miaka nane tu kushika Dola
Tanzania mmekataza wapinzani wasifanye siasa ili muendelee kutawala milele.... Fumbua macho utaliona hili!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona nyie mliushangilia ushindi wa Kenyatta Na kuanza kuwananga Odinga Na Magufuli? Leo hii uchaguzi umetenguliwa mnashangilia tena
Uhuru atashinda tena , lakini tunachoshangilia sisi ni uhuru wa Mahakama ya Kenya , hii inatokana na nchi hiyo kuwa na Jaji Mkuu kamili , siyo Kaimu .
 
Ila Chadema Wenye akili wametimiza Robo Karne ( 1992-2017) bila hata ya kupata theluthi Moja ya Wabunge Bungeni wakati TANU iliwachukua Miaka 7 tu kukamata dola, ASP iliwachukua Miaka nane tu kushika Dola
Acheni kutumia vifaru kudhibiti wanasiasa .
 
Back
Top Bottom