Wewe pambana na maisha yako achana na siasa utashutuka umezeekaYaani wamejikita kuishambulia CHADEMA na Lowassa wao kwa yaliyotokea Kenya, vijana wa watu hawaelewi kua haki inayotolewa na mahakama za Kenya haipo Tanzania. Hawa vijana hawajui kabisa leo hii Raila Odinga angekua nchini mwetu hiyo haki asingeipata.
Sijui hawa vijana wana matatizo gani! Labda nieleweshwe vizuri nami nifahamu, tatizo ni elimu? Uelewa wa nmna ya kung'amua mambo? Wamekaririshwa? maisha magumu? Ningeomba watitokeze tu humu humu waseme tu wao wenyewe. Vinginevyo kama ndio mawazo yao haya, tusitegemee uhai wa CCM kabisa siku za usoni.Is this a CCM upcoming new generation?
Badala ya wao kumshauri mwenyekiti wao wa chama taifa wakae waone namna ya kubadilisha katiba ya nchi hivi sasa ili siku moja haki itendeke kwetu kama Kenya badala yake Wamejikita kuishambulia CHADEMA na Lowassa wao, mashsbulizi haya yana madhara gani kwa CHADEMA? Yana faida gani upande wa CCM?
Bado uchaguzi wa Kenya umeamriwa kurudiwa kwa muda wa Siku 60, Je,akishinda tena Uhuru Kenyatta ikiwa bado CHADEMA watendelea kuwaunga mkono muungano wa Jubilee itakuwaje? Bado wataachana na ajenda za kitaifa na kubaki kushambuliana na CHADEMA?
Ni aibu na fedhera kwa kwa vijana wanaoitwa vijana wa Chama tawala kuhangaika mambo ya ajabu ajabu wakiachana na mambo ya muhimu na majukumu waliyonayo. Au wengine hawa wengine ni wafuasi tuu lakini sio wanachama wa CCM ndio maana hawaelewi watendayo?
Kwa fikra hizi, Mwanadishi na Wakili msomi Jenerali Ulimwengu amesema itatuchukua miaka 40 kuyafikia maendeleo ya nchi ya Kenya iwe kisiasa,kielimu,kiuchumu na hata kijamii.
Sent using Jamii Forums mobile app