Maskini Mji wa Moshi

Maskini Mji wa Moshi

Ulalule...... Manispaa wajitahidi hizo barabara zitengenezwe. Diwani wa Kata ya Longuo B na yule wa Kata ya Kilimanjaro tunawataka walivalie njuga hili swala ili Halamashauri ikarabati hizo barabara. Tuache utani!
 
Naona Mandra Jr umekuja kwa style nyingine ya DM ukimaanisha dodoma mji wako uliokuwa unaulinganisha Na Chaggaland, hahaa Bahati mbaya habari tunayo. Kuna miji kibao haina hata hiyo lami, je haistahili kuwekewa lami au yenyewe siyo sehemu ya Tz, kuijadili Kilimanjaro siyo mbaya kwakuwa Ni nia njema kuonesha mapungufu, lakini mi naona Kama tumeisahau mikoa mingine Kama shy, Iringa, Songea, Mtwara, n.k. Hasa kwenye nyanja mbalimbali za kinamii.
 
mji wa moshi unachafuliwa na siasa,ikifika wakati wa kuwaondoa machinga na mafundi cherehani,ccm wanawazuia maofisa wa manispaa kuendesha oparesheni wakidia kufanya hivyo ni kupoteza wapiga kura,leo ni miaka 20 jmbo la moshi liko upinzani na ccm hawana chao licha ya kudai hao ni wapiga kura wao.

1995-2000 alikuwa mtui wa NCCR-Mageuzi,2000-mpaka sasa mji umekamatwa na 'babu' ndesamburo na ccm kimya,
anayeuliza ndesa yupo ni kweli babu yupo huyo ni ng'ombe hazeeki maini

suluhisho la yote ni kuacha siasa za majitaka zinazofanywa na ccm,ukifika soko la mbuyuni uchafu umetanda hadi barabarani,nenda kata ya bondeni pale manyema ndo kabisaaaaaaa usiseme,nenda kata ya kiusa,gereje bubu ndo wamekamata mji,mitaro mingi ni michafu mpaka soko kuu limefungwa kwa sababu ya uchafu.

sifa ya mji wa moshi inapotea sanaaaaaaaaaaaa wala msijidanganye kwamba mji wa moshi ni msafi,usafi wa mji huu unaangaliwa katikati ya mji na si pembezoni mwa mji
 
Back
Top Bottom