Maskini Mji wa Moshi

Maskini Mji wa Moshi

Binafsi nilishasema kuwa Moshi hapa endelei kabisa miaka nenda rudi, vijana wa kichaga wakanuna kweli.
 
Wanachokijua Ni Mbwembwe Za Kujengea Tu Makaburi Kifahari Na Kuishi Ki Dili Dili Na Kimagumashi Humu Mijini Mwetu.

Akili yako finyu na utaishi kifinyufinyu hadi uwe maiti! acha chuku chapa kazi uwe kama wao! Tuwe na wivu wa maendeleo kama wao na tujuulize kwanini wanafanikiwa kila kukicha? kwanza wana ushirikiano na hawakati tamaa hawa jamaa. wewe baki unabung'aa na kusema wanaishi kimagumashi!
 
Binafsi nilishasema kuwa Moshi hapa endelei kabisa miaka nenda rudi, vijana wa kichaga wakanuna kweli.

Mdau Moshi inakuwa sana tu tena sio mjini nenda milimani kwako ndio utachoka kwani kuna nyumba na mahekalu kama uko DSM!
 
Wanachokijua Ni Mbwembwe Za Kujengea Tu Makaburi Kifahari Na Kuishi Ki Dili Dili Na Kimagumashi Humu Mijini Mwetu.

we apa mjini umejenga!?,au unakaa tu kwe kibaraza kwa babako ukinywa kahawa?.
 
Nilivyosoma title "MASKINI MJI WA MOSHI" nikajua labda umeungua moto...dah kuna watu mnajua kuunda headlines!
 
picha imepigwa toka kahawa house akachagua upande mmoja lakn angegeuka kushoto angepiga uelekeo wa mawenzi hosptl au double road kuko fresh tu. mji wa moshi wanauonea, au mnataka ulingane na dar au mwanza? mji uko km 70 toka mji wa kimataifa wa Arusha. hii ni factor kubwa ya kutokukua mnavyotaka. factor nyingine ni nature ya watu wa klmanjaro kutopenda kukimbilia kujenga mjini, nenda vijijin uone. Mwanza imeendelea kwa gharama za musoma, bukoba na shinyanga. Mbeya kwa gharama za songea na sumbawanga. poleni sana haters lakn ndo ukweli.
 
Barabara karibu Tanzania nzima zimeharbika ikiwa ni sababu ya mvua zilizokuwa zinanyesha na ubovu/kutokuwa imara/ujenzi chini ya kiwango ama kukaa kwa muda mrefu kwa barabara nyingi

Tatizo bajeti zinazotengwa kwa kiasi kikubwa zinalenga kuanzisha barabara mpya na halmashauri zinalenga viraka
 
Tutoke kwenye ulevi wa vyama na utumbo wa chama flani kimefanya hivi. Moshi yetu tuipende na kuijenga kwa pamoja. Tuangalie maslahi yetu kwanza km tulivyolelewa na wazee wetu.

Hatua za mwanzo za vyama vingi iliwezekana kuwa na wanachama wengi tu wa upinzani na hata kushinda ubunge. Mfano hai imekua na wabunge wa vyama tofauti hata CCM nao wametoka na wamerudi wamechemsha wametupwa.

Tumelelewa kujua tunalotaka kwa wasiotujua. Msitupandikize michuki yenu.

Ni kweli Moshi hapa nyuma iliporomoka. Zile fine kubwa kubwa kwa kuchafua au kupaki hovyo zilisimama na ndo hali ikidorora. Juzi nimeenda na kushuhudia mabadiliko, wamekaza tena kiusafi naamini itarudi. Mzee eti Ndesa pia bado yupo.

Kuhusu ujenzi siridhiki na maendeleo ninayoyaona. kwa utajiri wa watu wa Moshi ningetarajia majengo mazuri na makubwa zaidi kama la NSSF pale.

Barabara pia zimeporomoka.
Ila Nina hakika wanamoshi watajenga na jitihada zipo.

Moshi ya wanamoshi Mi vyama yenu ya siasa sio agenda yetu kwenye maendeleo kama kwa jamaa flani flani humu.

Tuipende na kuilinda Moshi yetu Wanamoshi.

Eeka Nsuri
 
Last edited by a moderator:
Mpaka ifikapo 2025 moshi itakuwa jiji likipanuliwa kuelekea Boma ng'ombe via KIA. hiyo ni mipango miji na mikakati ya kuifanya moshi kuwa jiji kutoka manisipaa. Je wadau wa moshi linawezekana hilo kulingana na resounce zake?
 
Akili yako finyu na utaishi kifinyufinyu hadi uwe maiti! acha chuku chapa kazi uwe kama wao! Tuwe na wivu wa maendeleo kama wao na tujuulize kwanini wanafanikiwa kila kukicha? kwanza wana ushirikiano na hawakati tamaa hawa jamaa. wewe baki unabung'aa na kusema wanaishi kimagumashi!

Mapovu Ya Nini? Kwani Majambazi Na Matapeli Wengi Wanatoka Wapi Tanzania? Mmefilisi Hadi Che Nkapa!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom