Maskini Karagwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maskini Karagwe

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Igabiro, Nov 3, 2010.

 1. Igabiro

  Igabiro JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2010
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kuna tetesi kuwa karagwe CCM wamechukua jimbo, hii ni baada ya kijina wa CHADEMA aliyekuwa akiongoza kwa tofauti ya kura 500+ kukubali kurudia kuhesabu kura, hii inatokana na Mh. wa zamani (Sr. Kahama) kumuaidi (pleadge) kiasi cha 200Millioni ili hata akishindwa apoze machungu. Hii ni very sad. Ilitakiwa aige mfano wa Mrema wa Arusha mjini yeye alisema kura hazihesabiwi upya labda kama Mungu anashuka.
   
 2. m

  mbea Member

  #2
  Nov 3, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kumbe chadema dhiki tupu!
   
 3. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #3
  Nov 3, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Acheni umbeya jamani. Nimekuwa hapa tangu day one ya kupiga kura.
  Hakuna cha mtu kuhongwa hapa, bali uchakachuaji wa system tu ndio umezamisha jahazi la Chadema.
  Leo asubuhi waliletwa maafisa watendaji wa kata wote na kuulizwa kura za Blandes kutoka kila kata.
  Walizotaja ni tofauti na zilizojazwa katika fomu ya msimamizi wa uchaguzi. Yaelekea syetms ilichakachua formu za msimamizi na kuingiza nyingine mpya zenye figures za kumsaidia Blandes.

  Msiwakatishe tamaa watu, hakuna aliyehongwa katika Chadema, labda kama kahongwa msimamizi ili aruhusu system kuchakachua.
   
 4. m

  mashuke Member

  #4
  Nov 3, 2010
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 66
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Kwahiyo unaona hao CCM wanaohonga kama unavyosema wanfaa kutuongoza.Tume ya uchaguzi iliandaliwa kuipa ushindi CCM kwa gharama zote.
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  Nov 3, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Umeliwakilisha vizuri jina lako.
   
 6. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #6
  Nov 3, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  CHADEMA wangekuwa na njaa, Lema angekuwa wa kwanza kuchukua bil.3 za EL vs Batilda.
  Watu wa Arusha tulikomaa kuwa hakuna kura kuhesabiwa tena.
  Hicho kilichofanyika Karagwe ni uhuni wa CCM na Mzee Kahama.
   
 7. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #7
  Nov 3, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Hakuna uwanja sawa wa ushindani katika uchaguzi huu.Tume inaripoti Ikulu unategemea nini?
  Pale ambapo vyama vingine vimeshinda hususani Chadema ni kwa sababu nguvu ya umma ilikuwa kubwa.
  Haya mambo ya kuhongwa ni propaganda tu maana nimesikia kuwa kilombero G.S amehongwa million 200,huku nako million 200,inakuwaje figure zifanane?Hamjui hata kudanganya,kweli nyie mabogas.Huu ni mpango wa kukichafua chama,kamwe hautafanikiwa.
   
 8. Utotole

  Utotole JF-Expert Member

  #8
  Nov 3, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 6,344
  Likes Received: 3,178
  Trophy Points: 280
  Mtu yeyote mwenye taarifa za uhakika kuhusu uchakachuaji huu? Maana kama hali itaendelea hivi inaelekea CCM wamepanga kuhakikisha majimbo yote yaliyosalia yanaangukia mikononi mwao.
   
 9. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #9
  Nov 3, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kuna watu knye hiki kijiwe chetu wametumwa na mafisadi tuwe makini nao sana, wanaleta habari za umbeya
   
 10. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #10
  Nov 3, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  source please
   
 11. inols

  inols JF-Expert Member

  #11
  Nov 3, 2010
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 285
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Kudadadeki, karagwe kwishnei, chadema tunajapinga upya kuanza na wave nyingine ya mashambulizi, aluta continua
   
 12. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #12
  Nov 3, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,356
  Likes Received: 3,123
  Trophy Points: 280
  pesa za epa zilizoibiwa na ccm zitawamaliza wote (akina KIBONDE) isipokuwa wachache
   
 13. K

  Kishalu JF-Expert Member

  #13
  Nov 3, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 850
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  Mbea mkubwa au ni wale nduguze wameteuliwa na JK,jina lako tumeliona
  maana ww unabariki ufisadi
   
 14. c

  chairman Member

  #14
  Nov 3, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jaribu kuwa na data tafadhali na kama ameahidiwa kiasi hicho nani aliona au ndo majungu.
   
 15. c

  chairman Member

  #15
  Nov 3, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli kijiwe kimevamiwa tuwe macho na wanajamii ambao wametumwa na mafisadi kutuharibu. lakini sisi tunasema hatudanganyiki hivyo vibia na vichips wanavyohongwa shair zao. hiki sio kijiwe cha ccm tafadhalini mliotumwa na mafisi ya ahadi
   
 16. C

  Campana JF-Expert Member

  #16
  Nov 3, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Karagwe wanasema wanatokomea migombani sasa. Wakiibuka watastrike. Hakuna kulala
   
 17. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #17
  Nov 3, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Hawa nao wameshirikiana na CCM kuchakachua ......... the-the-the...

  WAANGALIZI wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu uliofanyika Oktoba 31,kutoka Jumuiya ya Ulaya ( EU EOM) na Umoja wa Afrika wamesema kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa huru na haki, utulivu na amani.

  Waangalizi hao walitoa kauli hizo kwa nyakati tofauti wakati walipofanya mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana(leo) kuhusu taarifa ya awali ya uchaguzi huo.

  Akizungumza na waandishi wa habari Mwangalizi Mkuu wa EU EOM, David Martin alisema uchaguzi huo ambao ni wa nne kufanyika nchini tangu mfumo wa vyama vingi kuanzishwa Tanzania, hadi sasa kwa ujumla umefanyika kwa amani na mpangilio mzuri.

  " Siku ya Uchaguzi Mkuu ilijitokeza kwa utulivu mkubwa na kwa ujuml a waangalizi wa uchaguzi wa Ujumbe Maaalumu wa Jumuiya ya Ulaya(EU EOM) ulikadria mchakato mzima wa uchaguzi huo kuwa ama ulikuwa ‘mzuri' au ' kuridhisha' katika asilimia 95 ya vituo vyote vya kupigia kura walivyovitembelea upande wa Tanzania Bara na upande wa Zanzibar," alisema Martin.

  Aliongeza kuwa kwa ujumla taratibu muhimu katika vituo vya kupigia kura zilitumwa kwa ulinganifu kwa kila kituo cha kupigia kura nchini kote, licha kuwepo mapungufu machache.

  Martin alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) zilisimamia chaguzi kwa namna ya kitaalamu, hivyo kwa sehemu kubwa ziliwapatia watu watu wote haki ya kupiga kura.

  Aliongeza kuwa ujumbe huo utabakia nchini kuzidi kufuatilia kwa karibu zaidi zoezi la kuhesabu matokeo ya uchaguzi, utangazaji wa matokeo na matukio yoyote yatakayojitokeza baada ya uchaguzi.

  "Taarifa hii ni ya awali .Taarifa ya kina ya mwisho itatolewa baina ya miezi miwili na miezi mitatu baada ya mchakato mzima wa uchaguzi kukamilika," alisema.

  Kwa upande wake Kiongozi wa waangalizi hao, kutoka AU, Rais wa zamani wa Jamhuri ya Sierra Leone, Dk. Ahmad Tejan Kabbah alisema uchaguzi huo umefanyika wa amani na umefanyika kwa mujibu wa sheria za uchaguzi wa Tanzania .

  Aliongeza kuwa umefanyika kwa kuzingatia Azimia la Durban Demorasia katika Chaguzi za Afrika la Julai mwaka 2002.

  " Waangalizi wa Umoja wa Afrika wamesema uchaguzi umefanyika kwa huru, haki , uwazi na uadilifu(Credible)
   
Loading...