Ndugu, mbona umeng'ang'ania sana miaka 30 iliyopita? Watanzania wa sasa siyo wale wa miaka 30 iliyopita, na wakati huo nchi ilikuwa ya chama kimoja na tulikuwa haturuhusiwi kusema neno zaidi ya zidumu fikra za mwenyekiti na pia rasili mali zetu nyingi zilikuwa hazitumiki na hakukuwa na mitandao ya kijamii kama sasa, habari zote tulitegemea RTD na magazeti ya Uhuru na Mzalendo, pia kumbuka miaka 30 iliyopita idadi kubwa ya wanachama humu Jf tulikuwa watoto, mimi nilikuwa na miaka mitano. Inamaana kiongozi akishindwa kurekebisha makosa ya waliyomtangulia asilaumiwe? Na kama hawezi kurekebisha basi aachie ngazi, tutafute watakaoweza. Usitetee U-dhaifu.
Ndugu, usipoteze lengo - please revisit post yangu ya kwanza, nilitangulia kuzungumzia kipindi cha Mzee
Ruksa alafu nikaja kipindi cha taugh
BENNY hapo tunazungumzia miaka
20 (ishirini) kipindi cha Kambarage niliongezea tu ku-draw attention ya wana JF wajue mambo ya Viongozi kushindwa kuwajibika ipasavyo na
udokozi havikuhibuka gafla bin voom!
Sasa swali: Je katika kipindi hicho kulikuwepo magazeti ya watu
binafsi mangapi? Radio na TV za watu
Binafsi ngapi? Vyama vya
upinzani vingapi? Kumbuka kwamba katika kipindi hicho kulikuwa na uhuru wa vyombo vya habari hadi leo, vile vile na vyama vya upinzani viliruhusiwa lakini madudu yalikuwa yanaendelea
unabated, two decades is no laughing matter. Kusema ulikuwa mtoto is no excuse kwa nini
usomi historia au kuhuliza walio kuzidi
umri ili at least uwe na basis za kumlahumu bila simile kiongozi wako wa sasa hivi, kumbuka kuna wana JF wa lika lako ambao wanafanya utafiti kwanza (past history) kabla ya ku-file posts za kulahumu leadership quality ya Kiogozi mkuu wa
TAIFA kwa kuangalia mabaya tuu wakati wote bila ya kuzungumzia mazuri ambayo amefanyia
TAIFA hili
within six years of his admistration. See - watu makini usema no research no....
JK ni mswahili mwenzetu sio mtawala (Kiongozi) kutoka nchi za nje (mkoloni), wala sisemi
JK ni
Malaika Gabriel kwa hiyo hana mapungufu yake kama binadamu wingine tulivyo, cha muhimu hapa ni sisi kubadirisha
mind set zetu tuweze kumpa ushirikiano, ushauri na maoni kwa ajili ya ustawi wa TAIFA letu bila kutumia lugha za
kashfa na mambo ya kumkatisha
tamaa; tutabaki
TAIFA la kulalamika mpaka lini? Mbona mtu kama
Zitto Kabwe anatoa ushauri/maoni yenye mshiko na Serikali yetu tukufu inamsikiliza -
WEWE JE?