Maskini hawakujuaaaaaaaaaaaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maskini hawakujuaaaaaaaaaaaa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Eeka Mangi, Feb 4, 2012.

 1. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #1
  Feb 4, 2012
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Tupo msibani! Kijana kafiwa na baba yake. Katikati ya maombolezo anafika binti mmoja hivi mtanashati ingawa tumbo kubwa lakini huachi kuona uzuri wake, anajiunga upande wa wamama asalimiana wanaendelea na maongezi. Pamoja na majozi alokuwa nayo kijana anapata faraja ya haja. Mara akawa kama amechangamka hivi. Tunamuuliza kulikoni kijana?

  Anasema da angalao mchumba wangu kaja maana nilikuwa nasikitika kumwacha mwenyewe mbali. Anha kumbe! Mjomba yupo hapa na unajua tena huku uchagani hawakopeshi.

  We Lelo unasemaje! Nyie watoto wa siku hizi mafirauni sana! Yaani unathubutu kulala na mtoto wa shangazi yako unakuja hapa unatwambia mchumba wako! Jamaa jasho likaanza kumtoka! Da kumbe kijana keshamvimbisha binti wa wenyewe na sasa ni mtoto wa shangazi!

  Ilikuwaje: Familia ya kijana wa kiume ilikuwa ikiishi nje ya Tanzania kwa kitambo kidogo. Ni mara chache sana walikuja Tanzania ingawa wazazi wote ni watanzania. Kwa kujua kuwa huyu mzee atastaafu mapema akaanza kumtanguliza mwanaye wa kiume aje Tanzania na akapata chuo cha kufundisha pale Dodoma.

  Akiwa hana hili wala lile akakutana na binti mrembo yuko idara moja na yeye. Mazoea yakajengeka! Upendo ukachanua! Wakajikuta watupu,,,,,,,,,,,hatimaye mmoja akawa amebeba kiumbe cha muunganiko wao. Tuongeapo sasa mimba ina miezi 6 na ushee.

  Maskini mzee wa watu hata hakustaafu bali kaugonjwa kakapita akaona wacha aje nyumbani akasalimie. Huku akazidiwa zaidi akalazwa pale KCMC. Mvulana akaomba likizo ya dharura pale chuoni aende kumuuguza mzee. Siku chache baadae baba akaaga dunia. Akamtaarifu mchumba wake kuwa baba mkwe wake mtarajiwa kafariki. Binti naye akaona ni vyema akajumuika msibani. So ikawa pia awatembelee wazazi wake huku kijijini.

  Kumbe naye msiba unamhusu kwa njia nyingine bila kujua. Mama wa huyu binti akamwambia kuwa mjomba wake kafa hivyo wakasalimie. Maskini hakujua kuwa huo ndo msiba aloujia! Wakati anaingia hakumwona Kijana hivyo alijua tu kuwa angewasliana na mchumba wake ili amwelekeze msiba uko wapi. Sasa mambo yameharibika!

  Mjomba najua na binti hajajua kuwa kule ndo kwa kijana mchumba wake kipenzi. Mimba hii ni kubwa sana inaweza ikaleta madhara! Maskini hawakujua kama ni ndugu! PANDE ZOTE ZIAMBIWE AMA TUACHE MPAKA MSIBA UPITE!

  Ni ushauri wako tu. Kama unahisi kuwa unataka kukashfu ni bora uasiweke bandiko iache tu ipite!


  UPDATES
  Wazazi wa huyu binti wameelezwa habari hizi. Wamehuzunika sana kwa kweli. Binti na kijana wameitwa na kuelezwa ukweli.
  1. Kijana amekataa kuamini amedai atatoa maoni yake baadaye.
  2. Binti ameondoka na ndugu zake hakuweza kusema chochote alibaki kushangaa tu.
  3. Hakuna hata mtu mmoja keshajua linaloendelea zaidi ya sisi ndugu wa karibu
  4. Wazee wameshauri hili suala lizungumzwe baada ya kuvunja tanga
  5. Focus now ni mazishi tu
  Nitawajulisha maendeleo ya hii kitu.
   
 2. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #2
  Feb 4, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Binamu nyama ya hamu haina shida kwa sisi wa pwani unaoa kabisa tena kwa shangwe na kigelegele
   
 3. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #3
  Feb 4, 2012
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ahaaaaaaaaaa kumbe ndo binamu kaka! Sasa huku uchagani yakhe hamna hii!
   
 4. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #4
  Feb 4, 2012
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Dah sio kazi rahisi

  Kwanza poleni saana na msiba

  Navyowajua wachagga hili jambo linaweza malizwa na wazee, ongeeni na wazee wa mbande zote mbili kwanza mnaweza angalia wale wazee wenye busara naamini watawapa muongozo mzuri na mahali pa kuanzia

  Kuambiwa naona ingekuwa jambo la busara muache kwanza mpaka mzike, nadhani mtakuwa na kikao cha ukoo, pale ndio sehemu muafaka pa kuyamalizia

  Mangi
  kama utakumbuka zamani zile watu walikuwa wanaacha wake zao nyumbani na kwenda mijini kutafuta pesa nini kilitokea, wapo baba wengi waliwageuka wake za watoto zao na wengine walienda mbali mpaka wakazaa nao, haya mambo kuna namna walikuwa wanayamaliza kiutu uzima, sasa huyu kama kampenda mtoto wa shangazi naamini hiili ni jambo ndogo saana, hao wazee lazima watalimaliza

  Mkumbuke kuandaa faini, lazima jamaa atozwe mbege,,,,,,,joke,,,,,
   
 5. salito

  salito JF-Expert Member

  #5
  Feb 4, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,366
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  waache tu wazae mtoto wao,na ikibidi wawabariki wafunge ndoa,maana hawakufanya kusudi,o ikishindikana wazae tu halafu kila mmoja aende na habari zake,lakini mtyakuwa mmewanyanyasa kuwalazimisha waachane,wakae wao wenyewe wakubaliane,halafu nyie itawabidi mkubaliane tu na msimamo wao.
   
 6. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #6
  Feb 4, 2012
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kuacha kutomwambia ina maana aondoke hapa msibani sasa hivi ili asimwone kijana la sivyo lazima waambiwe sasa maana wazee ndo wanakaa kujadili. Sijui itakuwaje maana hata wazee wengine wanaanza kulaumu wazazi pande zote kwa kuwa mbalimbali kiasi cha watoto kutokutambuana. Naona shangazi anaitwa wacha tuone!
   
 7. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #7
  Feb 4, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Aiseee!!
  Bora waambiwe mapema na mtoto aachwe azaliwe maana hamna ujanja. Imeshatokea hivyo kubalini tu hali halisi.

  Ila nisingeshauri waendelee kuwa wapenzi, it's just weard!!
   
 8. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #8
  Feb 4, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  well maji yashamwagika, ki ujumla wote familia nzima ina makosa; msiwaonee hao wapenzi peke yao!
   
 9. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #9
  Feb 4, 2012
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Hivi katika kipindi chote hicho hawajaulizana wanatokea uchagani sehemu gani?

  Lazima wangefahamiana kuwa wanatoka kijiji kimoja na ukoo wa Mzee fulani hapo kijijini.

  Au waliamua kunyamazia walikwisha tambua yote? Hapa kidogo ni kizungu mkuti,
   
 10. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #10
  Feb 4, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,974
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Mtoto wa shangazi sio mbaya waweza kuishi pamoja.wapeni baraka zenu wazazi
   
 11. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #11
  Feb 4, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kuna watu wanakutana juu kwa juu, na kumalizana juu kwa jua yani hata kushea historia zao ni mitihani. Pia malezi yanachangia. . Imagine huyo binti hakua anajua jina la mama yake la mwisho la asili kwamba linafanana na la mshkaji, au sijui hata hilo hawakuambizana. Ndio matokeo ya kulea watoto kimjini mjini sijui kiulaya ulaya hata ndugu zao hawawafahamu.
   
 12. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #12
  Feb 4, 2012
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Lizzy kuna watu hata huwezi jua kuwa ukoo wao ni upi. Mfano Hawa jamaa wanaoitwa Kiria wakishakuwa wasomi na wenye hela wanaitwa Mworia. Wale wa ukoo wa Mboro wakiwa wasomi tu wanajiita Mboya ama unaweza kukuta wanajiita Ndossi. So Kijana anatoka katika hii jamii ya wanaojua kuwa wao eti wameendelea na anajiita jina la kisomi badala ya lile la asili yao kabisa! Kisa sijui.
  Same applied mama kaolewa anabadili jina kwa la mumewe na watoto hawajali sana kujua.

  Ila ninapoongea nanyi Mama wa binti, binti na akina mama kadhaa na wazee wameondoka hapa. Nafikiri sasa yanaenda kuongelewa huko na tusubiri!
   
 13. de'levis

  de'levis JF-Expert Member

  #13
  Feb 4, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,188
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  ni rahisi sana....watafute kondoo wachinje na ile damu itakayotoka iwekwe kwenye kibakuri kisha imwagwe chini na waitwe hao wawili(kijana na binti) kisha wairuke ile damu......aanze binti kuruka....kisha kijana..hapo watakuwa wamevunja ukoo....
   
 14. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #14
  Feb 4, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 305
  Trophy Points: 160
  wawowane tu
  binamu?! Nilidhani mimba ya marehemu na marehemu alikuwa baba yake.
   
 15. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #15
  Feb 4, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,230
  Trophy Points: 280
  mabinamu hao! Ruksa
   
 16. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #16
  Feb 4, 2012
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  ha ha haaaaaaaaaaaa niko msibani man usitake ncheke kwa sauti wat wasikie. Huku ni Kibosho Mangi hiyo ni style ya wapi?
   
 17. Dunda kwetu

  Dunda kwetu JF-Expert Member

  #17
  Feb 4, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 265
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kabisa mtoto wa shangazi ruksa kujihifadhi
   
 18. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #18
  Feb 4, 2012
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Nyie vipi nyie huko kwenu bana huku kwetu so ruksa bhana.
   
 19. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #19
  Feb 4, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kaka hii issue siyo kubwa kivile (in my views)!!

  Hakuna mtu mwenye makosa hata mmoja. Wanaolaumu wazazi wanawaonea kwani sasa hivi watu wanakimbizana na maisha....

  Biologically hawa watu wana uhusiano ila degree of relatedness ni ndogo sana......<10%.

  Wafuate taratibu za kimila halafu wafunge ndoa....BASI!!

  Kule kwetu kulikuwa na taratibu ambazo ni kama hiyo ya kuchinja mbuzi na kufunga mizimu ili kuvunja ukoo na baada ya hapo watu wanabanjuana kama vichaaa!!

  Babu DC!!
   
 20. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #20
  Feb 4, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Kweli kaka ila sasa mna-deal na situation ambayo siyo ya kawaida...Huweza kutumia rules zile zile kama ambazo ungetumia kwa watu ambao ndo kwanza wanaonana!

  Fanya lolote ila mjue kuwa hawa watakuwa wazazi na huyo mtoto ni wao....Ukweli ho haukwepeki...Deal with it sir!!
   
Loading...