Masikini kaka huyu

Masikini kaka huyu

miss chagga

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2013
Posts
57,805
Reaction score
49,104
Habari zenu wana Jf,

Ni moja ya rafiki zangu ni kijana mkimya, mpole, mcha Mungu, ana heshima na mpiganaji katika kutafuta maendeleo, katika pilika pilika zake Mungu akampa binti mzuri, mpole, msikivu na mwenye adabu hapa ndipo mwanzo wa misha yao mpaka ndoa. Kwa sasa wana mwaka mmoja ndani ya ndoa yao na Mungu kawamjalia mwanamke kwa sasa ana ujauzito wa miezi miwili katika ile hali ya kuugua ugua akaenda hospital.

Kinachosikitisha na kuhuzunisha ni kijana mwezi huu kagundua mkewe ni muathirika (VVU). Huyu rafiki yangu huwa na mwita kaka ili kukata mzizi wa fitina si unajua mabinti tulivyo. Baada ya kugundua hivyo nikaanza kumuuliza je hawakupima wakati wa maandalizi ya ndoa.? Majibu aliyotoa kiukweli ni huzuni eti hawakuona haja ya kupima kisa wote aliona wametulia na hakukuwa na hisia yeyeote ya uchepukaji na pia walikutana Kanisani.

Nilivyo fyoko fyoko nikauliza vipi mlianza kuzini kabla ya ndoa na mlikuwa mnatumia Condom? akaijbu ndiyo ili kuzuia mimba kwa hiyo walivyofunga ndoa tu wakaanza kunjunjana bila Condom bila hata kujua afya ya kila mmoja.


Mungu si nanjilinji bwana wee kijana hajaathirika kapima zaidi ya mara 7 kila akipima anaona negative kawa kama chizi akipita mjini akiona hospital anashuka anapima aamini majibu anayopata.Lakini kutokana na vipimo inaonekana ajaathirika, kaenda hospital na mkewe doctor wamempa namna ya kuishi na mtu wa VVU lakini ameshindwa kinachotokea kijana analala sebuleni mwanamke chumbani.

Kinachotokea mke kawa na gubu anamlazimisha mwanaume mapenzi (ngono) mwanume hawezi, jamani mimi nimeshindwa mshauri zaidi nilimwambia alale sebuleni au Mzungu wa nne mwanamke amegeuka moto anataka ngono bila hata condom. Jamani naombeni anayeweza toa njia nyingine ya kumsaidia kijana ili waishi at least kwa amani mwenye suluhu

Karibuni, ushauri
 
Huyo mwanamke anataka wafe wote au ni nn sasa hicho atleast watumie kinga ili angalau mmoja apone!!ingawa ngumu kumeza
 
huyo mwanamke anataka wafe wote au ni nn sasa hicho atleast watumie kinga ili angalau mmoja apone!!ingawa ngumu kumeza
mbaya zaidi kuna wakati hata kumeza dawa hataki anaamini mungu atamponya .. Ushauri please
 
Washauri waje njia hii kwangu ni kina kirefu siwezi tia neno jingine zaidi ya pole najua tunao watu humu sio wawe mahiri kwa kupromote mambo ya ajabuajabu waje hapa so far miss chaga pole na segadanse hata sisi tuliku jina lako pia.
 
kwa nini ang`ang'anie?mwanamke muathirika in the first place,probability kubwa kapata maambukizi either kwa kuchepuka ama ngono zembe before marriage.Ina maana hajatambua kama ana kosa?Inampasa ashuke,awe mdogo kama piritoni?..Unafahamu kuwa anaweza kufunguliwa mashataka ya kuambukiza VVU kwa makusudi?...
 
miss chagga pole sana na jela
Ashikilie msimamo wake bila condom hapana maana hapo mwanamke kashajijua anao anataka amwambukize na mwenzake waupate wote na hiyo ni mbaya sana.

Gubu haliwezi kuisha na wala halitamuua kijana ila akijifanya anafanya bila condom ajue tayari anaupata maana mwanamke inaonekana kadhamiria jamaa aupate na yeye

Asikilize ushauri wa wataalam na akiona yanazidi hapo ni kuwaita wazazi na kuwapa ukweli wa kinachoendelea. Mtoto anaweza kuzaliwa bila kuupata na hapo ajue hata maziwa ya mama hayanyonya

Kama ni mapenzi ampende na kumtimizia kama mke ila kushiriki tendo la ndoa bila mipira asijaribu hata siku moja maana hapo dhamiri ishamtoka huyo mama
 
Katika ndoa mnahaidi kuvumiliana hadi mmoja aidha atoweke duniani, achepuke au awe na UKIMWI. Hivyo mwambie asepe maana akijaribu tu anapata. Kwani wengine hawapo?
 
Mwambie huyo KAKA yako atengane na huyo WIFI yako! akizubaa iko siku atajikuta anaonja kidogo na ndio kuukwaa!!

Ndoa za kikristo unajua tena wif hataki kusikia wala kuelewa
 
Katika ndoa mnahaidi kuvumiliana hadi mmoja aidha atoweke duniani, achepuke au awe na UKIMWI. Hivyo mwambie asepe maana akijaribu tu anapata. Kwani wengine hawapo?
sasa kuachana si makubaliano ya wawili mkuu? binti mjamzito sasa
 
miss chagga pole sana na jela
Ashikilie msimamo wake bila condom hapana maana hapo mwanamke kashajijua anao anataka amwambukize na mwenzake waupate wote na hiyo ni mbaya sana. Gubu haliwezi kuisha na wala halitamuua kijana ila akijifanya anafanya bila condom ajue tayari anaupata maana mwanamke inaonekana kadhamiria jamaa aupate na yeye
Asikilize ushauri wa wataalam na akiona yanazidi hapo ni kuwaita wazazi na kuwapa ukweli wa kinachoendelea. Mtoto anaweza kuzaliwa bila kuupata na hapo ajue hata maziwa ya mama hayanyonya
Kama ni mapenzi ampende na kumtimizia kama mke ila kushiriki tendo la ndoa bila mipira asijaribu hata siku moja maana hapo dhamiri ishamtoka huyo mama
swala la kinga kuna ugumu ahat binti hayupo tayari.. nafikiria kama wakiishi miaka 30 ndani yandoa kila siku wanatumia kinga? mi nachomwombea huyu rafiki yangu ni mtoto asiathirike tu
 
kwa nini ang`ang'anie?mwanamke muathirika in the first place,probability kubwa kapata maambukizi either kwa kuchepuka ama ngono zembe before marriage.Ina maana hajatambua kama ana kosa?Inampasa ashuke,awe mdogo kama piritoni?..Unafahamu kuwa anaweza kufunguliwa mashataka ya kuambukiza VVU kwa makusudi?...
Tyta kijana ana moyo wa uvumilivu hata kuendelea kuishi naye ila binti kawa mkorofi analazimisha penzi na kilio juu.. mimi naona huruma sana kwa kijana analalamika maisha yake kaingiza doa japo kijana naye kafanya uzembe kuoana bila kupima
 
Last edited by a moderator:
ki ukwel kwa hizo vurugu za huyo mke anaonekana dhahir kua anataka na mumewe kuupata ili wawe sawa kwahyo hata kwa kutumia condom anaeza pia kumnga'ata au vyvyte ili apate contact ya damu
ishaur wangu aendlee kukaa seblen na aende kwa wazaz wa pande zote mbili au kama mke ana ndugu mkubwa tofaut na wazaz amuelezze hiyo case jins ilivyo.
kingne asimuache mkewe kwa faida ya mtoto alie tumbon kwa maana anaweza akazaliwa bila maamumbikizo na pia ili mama asije akamdhuru mtoto
ila kwa situation yake hil swala ni gumu sana atumie busara zaid kuliko hasira.
 
kwani walipoenda kupata ushauri si walishauriwa na jinsi ya kukutana kimwli wakiwa katika halo hiyo?
 
Back
Top Bottom