Masikini Hamis Kigwangalla, Akosa wadhamini 450 nchi nzima

Masikini Hamis Kigwangalla, Akosa wadhamini 450 nchi nzima

Rio Tinto

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2014
Posts
777
Reaction score
452
Wadau,

Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa mmoja wa watangaza nia wa uraisi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Hamisi Kigwangala anafikiria kujitoa kwenye kinyang'anyiro hicho mara baada ya kushindwa kupata wadhamini 450 kutoka mikoa 15 nchini huku mikoa mitatu ikiwa ni kutoka Zanzibar na angalau mkoa mmoja uwe wa Unguja au kisiwa cha Pemba...Habari zisizo rasmi zinadai Ndugu Hamisi Kigwangala amefanikiwa kupata wadhamini 289 mpaka sasa...ikumbukwe mwisho wa kurejesha fomu ni tarehe 2 July 2015 kabla ya saa kumi jioni....

Kila la heri Ndugu Hamisi Kigwangala katika kufanikisha akidi hiyo.
 
Poor Boy tulimwambia haya kama ni kweli imemtokea...
 
Habari zimewafikia nyinyi akina nani?
Zimewafikia kutoka wapi?

Weka ufafanuzi hapo

Halafu kichwani kwako unajua hilo zoezi ni halisi au nadharia na mpunga tu!

Unaambiwa mtu kapata wadhamini 120,000 yaani umati wa kujaa viwanja viwili vya Taifa!!
Na huo uhakiki wa umati huo unafanyika in hours???

Amka
 
Mama HELLENA ELINAWINGA kaamua kazitelekeza fomu zake pale ccm makao makuu Dododma, anadai amechoka kuombwa rushwa.. Ha!ha!ha! Nchi ngumu hii hawajui watu wanataka pesa kabla ya sera?
 
wamemshindwa temeke wamemshindwa ilala, nilijua huyu kigu hawezi kufika kokote ni kupoteza muda wake na pesa zake,mkaribisheni mtaani kwa upendo tu manake hata ubunge ali salenda
 
Hilo la udhamini sina hakika ila saizi kuna kipindi cha marudio FUNGUKA amebanwa sana ameondolewa confo na ujinga wake umedhihiri kweli siasa za kubebana huyu anayehojiwa hapa anataka urais na mweupe kichwani anaongelea umri , anaponda chama chake na viongozi wake , anaongea hoja za wapinzani mda wote , anasema yeye atawasema tu hamna mtu wa kumkataza kusema, elimu sio kipaumbele kwake bali uchumi,nchi ipo kwenye tafrani,mfumo wa serekali mbovu sana hauwezi kutusaidia ,nitaufumua wote, jamaa anambana tu ameonesha udhaifu, hawa vijana bado labda january aliweza ku-cope kidogo huyu dhaifu sana wakuu
 
Bado ana wiki nzima, angejua wenzake wanaopata maelfu ya wadhamini wanaandikisha wanachama wapya na kuwalipia ada.
 
Muda ukifika ukweli utajulikana, 02 July 2015 sio mbali
 
Wadau,

Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa mmoja wa watangaza nia wa uraisi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Hamisi Kigwangala anafikiria kujitoa kwenye kinyang'anyiro hicho mara baada ya kushindwa kupata wadhamini 450 kutoka mikoa 15 nchini huku mikoa mitatu ikiwa ni kutoka Zanzibar na angalau mkoa mmoja uwe wa Unguja au kisiwa cha Pemba...Habari zisizo rasmi zinadai Ndugu Hamisi Kigwangala amefanikiwa kupata wadhamini 289 mpaka sasa...ikumbukwe mwisho wa kurejesha fomu ni tarehe 2 July 2015 kabla ya saa kumi jioni....

Kila la heri Ndugu Hamisi Kigwangala katika kufanikisha akidi hiyo.
Zimewafikia wewe na nani? kutoka wapi?
 
Acha waendelee kuumbuka..mwisho wa dharau aibu..
 
Mama HELLENA ELINAWINGA kaamua kazitelekeza fomu zake pale ccm makao makuu Dododma, anadai amechoka kuombwa rushwa.. Ha!ha!ha! Nchi ngumu hii hawajui watu wanataka pesa kabla ya sera?

Kwa hiyo Milioni wameliwa
 
Nyie ndg msiwe wageni hao wengine wanaitwa wagombea VICOBA
 
Sasa na vile vijembe vyake vya ujinga, atakoma Sasa....
 
Back
Top Bottom