Masikini hakai siti ya mbele habadani

simba songea

JF-Expert Member
Feb 8, 2016
1,498
1,211
Niwatakia eid njema waislamu wote,

Nadhani watu wengi watajiuliza kuhusiana na kichwa cha habari hapo juu. wageni watashangaa ila wenyeji hawatashangaa maana nilishawahi kuandika mada fulani humu inayosema'MUNGU HAFANYI AGANO NA MASIKINI' hii mada ilichafua hali ya hewa humu ndani na wengi walininipinga wachache walikubali, sikuvunjika moyo maana niliamini ili mada iwe tamu au iwe na muendelezo/isife lazima wapatikane wasioielewa ili waelekezwe na walioelewa. ndo maana nikapata moyo kuandika mada hii. Hata hivyo natumaini hii mada ipingwe na wengi ili isife.

Umaskini ni hali ya mtu kukosa uwezo wa kupata mahitaji muhimu kama vile chakula, malazi, mavazi.

Watu wengi tunajaribu kuupamba umaskini na kuwatia moyo ili waonekane kuwa hawana tofauti na walio na uwezo. Rais wetu Magufuli anajaribu kuupamba umaskini kwa kujiita mimi ni Rais wa maskini. Lakini kiuhalisia umaskini haupambiki hata ukiupaka lipstick bado hutopambika na unafaa kupingwa kwa hali ya juu ndo maana hata MWL JULIUS K NYERERE aliuhorodhesha umaskini miongoni mwa maadui wakuu watatu.

Tukija kwenye biblia tunaambiwa Ayubu alikosa furaha kutokana na umasikini pia alipoteza mke na marafiki kutokana na umaskini. Hata kuna baadhi ya wasanii wakubwa bongo walioheat enzi hizo wanalalamika kukimbiwa na nduguzo baada ya kufilisika.

Masikini hana haki wala mtetezi, mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe. Ukiwa mtu mzima afu ni maskini usitegemee kupewa heshima yoyote, heshima yako itakuwa ni 'shikamoo' tu, tena hapo wamekuhurumia.

Mara nyingi masikini hashirikishwi kwenye maamuzi yeye anasubiri wakuu wapange hata kama amewazidi umri hawamshirikishi zaidi ya kupewa taarifa au matokeo ya kikao walichokaa, na mbaya zaidi wanampangia maamuzi hadi yeye.

Masikini hata kama akija kwenye umati wa watu hapishwi kiti hata kama amekula chumvi nyingi. masikini hana sauti mbele ya matajiri, mchango wake ni kuunga mkono hoja ya matajiri iliyojadiriwa bila yeye kushirikishwa.

Masikini haesabiwi kama binadamu ndo maana anaitwa mzigo kwasababu hana mchango wowote.

Kama wewe ni mtu mzima alafu huna pesa basi wewe ni mzigo kwenye basi unaosubiria kushushwa ili watu waendelee na safari.
 
Tatizo la watanzania wengi wanadhani kuwa na maisha bora ni lazima uwe tajiri. Hata nchi zenye maisha mazuri dunian high living standard kama za skendinevia/nordic matajir ni wachache mno ila kila mwananchi anaweza kupata malazi chakula na mavazi kwa urahis sana hayo ndio maisha bora.

Bongo sasa unakuta watu wanaiba milion 8 kwa dakika kwa miaka kumi na hakomi shame on previous regime.
 
Umaskini ni laana uogope sana, hakuna mtu dunian ana ndoto zakubaki maskin maishani mwake
 
Ukiniambia maskini hana samani nakushangaa!!!!

Nijuavyo Mimi mjinga au mpumbavu ndio huwa hasaminiki ukiwa maskini na ukawa na hekma na busara nani atakukwepa

Wengi wanaopuuziwa ni wasio na akili (wajinga)
 
Heri walio maskini maana Ufalme wa Mbingu ni wao! Kajipange mkuu.

nt from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
hahaha mkuu naona unajaribu kubishana na ukweli.. hayo maneno umeyatoa math 5;3 yalisemwa na Bwana Yesu, kwa huo aliyasema hayo maneno alipokuwa anawahutubia maskini. Vp kuhusu zakayo aliyetoa nusu ya mali zake kwa maskini..kwa nn Yesu hakula chakula na maskini? alitaka kuubariki utajiri kupitia kwa zakayo
 
Masikini masikini nawaonea huruma.


But

Masikini ni yupi?


Kuna umasikini mwingi hata Prezda ni makini wa vitu flaniflani kama unabisha muulize Zitto Kabwe au Tundu .A. Lissu
kama umesoma vizuri ukaelewa kuna sehemu nimeandika maskini mtu anayekosa mahitaji muhimu kama chakula,malazi,mavazi,
 
Ukiniambia maskini hana samani nakushangaa!!!!

Nijuavyo Mimi mjinga au ******** ndio huwa hasaminiki ukiwa maskini na ukawa na hekma na busara nani atakukwepa

Wengi wanaopuuziwa ni wasio na akili (wajinga)
Yesu aliwaambia wanafunzi wake anawaadithia kwa mifano ili waelewe..nafikiri umeshindwa kulielewa somo hujalipata hili janga..ukweli utadumu milele umaskini haupambiki...hata tukiupamba tulioupitia huu umaskini tunayajua maumivu yake na wala sitaki kuusikia
 
Ukiniambia maskini hana samani nakushangaa!!!!

Nijuavyo Mimi mjinga au ******** ndio huwa hasaminiki ukiwa maskini na ukawa na hekma na busara nani atakukwepa

Wengi wanaopuuziwa ni wasio na akili (wajinga)
kisaikolojia hakuna maskini aliye sawa au anayetoa mawazo chanya. kama ameshindwa kujinunulia nguo unadhani huyu mtu ana akili sawa kweli mpk akushauri? maskini atabaki kuwa chini tyuuu
 
hahaha mkuu naona unajaribu kubishana na ukweli.. hayo maneno umeyatoa math 5;3 yalisemwa na Bwana Yesu, kwa huo aliyasema hayo maneno alipokuwa anawahutubia maskini. Vp kuhusu zakayo aliyetoa nusu ya mali zake kwa maskini..kwa nn Yesu hakula chakula na maskini? alitaka kuubariki utajiri kupitia kwa zakayo
Na mtoa mada anazungumzia maskini wa vitu(km sijakosea) ila umaskini wa Yesu ni wa roho(kukosa kuwa na maarifa/neno) UMASKINI NI LAANA TUPU
 
Back
Top Bottom