simba songea
JF-Expert Member
- Feb 8, 2016
- 1,498
- 1,214
Niwatakia eid njema waislamu wote,
Nadhani watu wengi watajiuliza kuhusiana na kichwa cha habari hapo juu. wageni watashangaa ila wenyeji hawatashangaa maana nilishawahi kuandika mada fulani humu inayosema'MUNGU HAFANYI AGANO NA MASIKINI' hii mada ilichafua hali ya hewa humu ndani na wengi walininipinga wachache walikubali, sikuvunjika moyo maana niliamini ili mada iwe tamu au iwe na muendelezo/isife lazima wapatikane wasioielewa ili waelekezwe na walioelewa. ndo maana nikapata moyo kuandika mada hii. Hata hivyo natumaini hii mada ipingwe na wengi ili isife.
Umaskini ni hali ya mtu kukosa uwezo wa kupata mahitaji muhimu kama vile chakula, malazi, mavazi.
Watu wengi tunajaribu kuupamba umaskini na kuwatia moyo ili waonekane kuwa hawana tofauti na walio na uwezo. Rais wetu Magufuli anajaribu kuupamba umaskini kwa kujiita mimi ni Rais wa maskini. Lakini kiuhalisia umaskini haupambiki hata ukiupaka lipstick bado hutopambika na unafaa kupingwa kwa hali ya juu ndo maana hata MWL JULIUS K NYERERE aliuhorodhesha umaskini miongoni mwa maadui wakuu watatu.
Tukija kwenye biblia tunaambiwa Ayubu alikosa furaha kutokana na umasikini pia alipoteza mke na marafiki kutokana na umaskini. Hata kuna baadhi ya wasanii wakubwa bongo walioheat enzi hizo wanalalamika kukimbiwa na nduguzo baada ya kufilisika.
Masikini hana haki wala mtetezi, mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe. Ukiwa mtu mzima afu ni maskini usitegemee kupewa heshima yoyote, heshima yako itakuwa ni 'shikamoo' tu, tena hapo wamekuhurumia.
Mara nyingi masikini hashirikishwi kwenye maamuzi yeye anasubiri wakuu wapange hata kama amewazidi umri hawamshirikishi zaidi ya kupewa taarifa au matokeo ya kikao walichokaa, na mbaya zaidi wanampangia maamuzi hadi yeye.
Masikini hata kama akija kwenye umati wa watu hapishwi kiti hata kama amekula chumvi nyingi. masikini hana sauti mbele ya matajiri, mchango wake ni kuunga mkono hoja ya matajiri iliyojadiriwa bila yeye kushirikishwa.
Masikini haesabiwi kama binadamu ndo maana anaitwa mzigo kwasababu hana mchango wowote.
Kama wewe ni mtu mzima alafu huna pesa basi wewe ni mzigo kwenye basi unaosubiria kushushwa ili watu waendelee na safari.