M-mbabe
JF-Expert Member
- Oct 29, 2009
- 13,201
- 23,030
Wakapata na vikombe, mavazi na baiskeli,
Wakawanunua ng'ombe, majike kwa mafahali
Hawakuitaka pombe, sababu pombe si mali,
Kama mnataka mali, mtayapata Arumeru!
mimi mmasai bana, hakuna wa kuniweza,
watapiga huu sana, katika kujiliwaza,
watabanabana sana, hawataachia kwa fweza?
****** amenisweti, seuze yule napie?
nimetwanga kotekote, masijidi kanisani,
sasa walete walete, meru stepu namba wani,
meru mtaji wa kete, ya 2015 naawambieni!
****** hanacho chake, nimemshika pabaya!
mimi mmasai bana, mwanaume aje hapa,
ninayo himaya pana, ndani ya chama mi papa,
ka wabisha onekana, nikuone hapa hapa!
kweli utajitokeza, kwani wewe hujipendi?
mtunzi wa shairi: mr white head
lol!!!