Mashuka na foronya vinaficha mengi

Mashuka na foronya vinaficha mengi

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
359,869
Reaction score
828,403
Jana ilikuwa siku ya wandwanao maandalizi yalikuwa mengi huko magetoni.. Hasa usafi kwa ajili ya maandalizi

Shughuli ya usiku wa jana imewaacha wengi wakiwa hoi na uchovu mwingi na wengine muda huu wanaperuzi mitandaoni wakiwa bado vitandani

Waliopata wageni wa kulala muda huu ndio wanapata wasaa wa kutathimi hali ya kitanda/godoro/mito. Vurugu za usiku wa wapendwanao zimefaragua shuka nzuri na sasa kuna siri zinatoka!😂
Mito iliyotumika kama kigogo mpaka foronya zikapanda juu kwa shuruba sasa ni wakati wa kuonesha yasiyopaswa kuonekana! Angalia yako utaona
Godoro lilivyo chafu na cover isiyotamanika.. Mito iliyojaa jasho, uchafu., michirizi ya udenda wa usingizi
Vingine vina uchafu na madoa ya off target kwenye harakati za utamu.. Uchafu uliopenya mashuka na foronya za mito🤪

Wengi wetu ni wasafi na watanashati wa nje.. Tunanukia na kumeremeta lakini ndani tumefutika uvundo na uchafu mkubwa

Usafi na management ya magodoro na mito yetu ni very very poor.. Tunajipa matumaini ya uokozi wa shuka, bed covers na foronya.. Lakini ukivitoa hivyo vitu magodoro na mito yetu ni majanga makubwa..
Nitarejea....
83cb7704-d3a8-423b-b78f-aec6c776db3b.jpeg
29e5d919-8d4c-4208-b9bc-92d6a5150933.jpeg
 
Sisi wenye wivu , tunawacheka tu wale waliouza mechi kiboya , sasa wanasikilizia dalili za ukimwi kwa mashaka kama digidigi🤣🤣
Mimi simo 🙌🏿🙌🏿🙌🏿🏃🏿😂
 
Kikubwa tumewabandua na tumeinjoi,hayo mengine tuwaachie wachunguze wakichoka watarejea makwao!
 
Naendelea...
Eneo la usafi katika ujumla wake halizingatiwi na wengi.. Mtu yeyote anayechukia rangi nyeupe huyo ni mchafu by nature..!😀
Shuka nyeupe
Magodoro yenta cover nyeuor
Mito ni myeupe by nature
Socks zinaweza kuwa nyeupe kulingana na aina ya viatu ama va mavazi
Chupi nyeupe😀 ugomvi mtupu hapa. Kuna watu wana mzio
Rangi nyeupe ni rangi ya usafi.. Hivyo nyeupe ni alama ya usafi kimwili na kiroho..!
Kuna baadhi ya kazi zinatulazimu kuvaa rangi tofauti lakini si wakati wote
 
Kuna madoa yanatia hata kinyaa kuyaangalia
29e5d919-8d4c-4208-b9bc-92d6a5150933.jpeg
d812c9d2-2dcf-46ce-9e49-1469a2ae9e23.jpeg

Here is why pillows are typically made with white materials:
Signals Cleanliness and Hygiene: White is closely associated with purity and cleanliness, providing a psychological assurance that the pillow is sanitary. It makes it easier to spot stains, dirt, or dust mites, prompting users to wash or replace them.
Allows for Easy Washing and Bleaching: White materials, particularly cotton and polyester, can withstand high-temperature washing and bleaching, which is necessary to eliminate germs without worrying about colors fading or bleeding.
Cost-Effective Manufacturing: Synthetic materials, such as polyester (a common white filler), are inexpensive to produce in bulk.
Prevents Color Showing Through: White casing prevents the dark, off-white, or brownish color of materials like down or lower-grade foam from showing through a white pillowcase.
Maintains Neutral Aesthetics: White is the standard in hospitality because it complements any decor and gives a luxurious, hotel-like feel.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom