Mashoga Kuwa Mapadri Uingereza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashoga Kuwa Mapadri Uingereza

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jun 22, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  [TABLE="width: 491"]
  [TR="bgcolor: #E1E1E1"]
  [TD]Jumuiya makanisa ya Anglikana, Uingereza inatarajiwa kutangaza rasmi kuwa wanaume waliojitangaza wazi kuwa wao ni mashoga wataruhusiwa kuwa mapadri iwapo watatimiza sharti la kujizuia kufanya ngono[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="width: 491"]
  [TR="bgcolor: #E1E1E1"]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Taarifa rasmi ya kuruhusu mashoga kuwa mapadri inatarajiwa kutolewa jumatatu ambapo imetangazwa kuwa ni katika kuondoa ubaguzi katika masuala ya dini bila ya kuwabagua watu kwa tabia au matendo yao kinyume na maumbile.

  Sharti la kuwataka mashoga wajizuie kufanya ngono iwapo wanatakiwa kupewa nafasi hiyo kubwa ya kidini huenda ikasababisha mtafaruku kwani mchungaji mmoja shoga anapinga sharti hilo na anatishia kujitoa yeye na wafuasi wake duniani toka kwenye kanisa hilo.

  Mwaka 2003, mchungaji ambaye pia ni shoga na mwanaharakati wa kutetea haki za mashoga, Dr Jeffrey John alitajwa jina lake miongoni mwa wagombea wa uaskofu wa mji wa Reading hali iliyosababisha mtafaruku mkubwa kwenye kanisa la Anglikana na kupelekea aamue kulitoa jina lake.

  Kanisa la Anglikana halitaki mgogoro wowote utokee na kuwagawa waumini wa kanisa hilo duniani.

  Hata hivyo, baadhi wa waumini wa kanisa hilo la Anglikana wanapinga uamuzi wa kuruhusu mashoga kuwa mapadri kwani ni kinyume na mafundisho ya kanisa.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]   
 2. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #2
  Jun 22, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni Uingereza au Unguja?
   
 3. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #3
  Jun 22, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Jamani kweli mimi, zamani nilikuwa nawaheshimu sana wazungu kwamba reasoning capacity yao ni substantial. Kumbe bado wana akili ya wale wanakijiji wa sodoma na gomora. Sijui hata wanatumia Biblia gani kuwapadrisha W.A.S.E.N.G.E. Kwa hiyo Kanisa limebadilishwa na kuwa danguro la mashoga loo! Aibu! Hilo ni chukizo la uharibifu. (Soma Daniel 9:27)
   
 4. Lawkeys

  Lawkeys JF-Expert Member

  #4
  Jun 22, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 1,110
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mashetani kanisani, the Church is infiltrated with demons in the human form. That is an abomination.
   
 5. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #5
  Jun 22, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,205
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  Hakuna mtu yeyote alie ndani ya Yesu kristo anaeweza kujadili suala la mwanamume anaebanduliwa kushika/kutoshika nafasi ya uongozi ndani ya kanisa. Kwa kuanzia huyu mwenda kinyume na asili ni mpinzani wa Mungu katika uumbaji wa asili. Mungu aliumba kwa siku sita na ya saba kupumzika, na kila alichokiumba kilikuwa ni chema. Baadae ndipo alipojitokeza Shetani akipotoa yale ya asili. Mungu ni kweli, uongo ni kweli iliyopotoshwa. Uzinzi nao ni tendo halali la ndoa lililopotoshwa, kama vile kila kitu kitazaana kwa jinsi yake, sasa jiulize kwa shoga atazaa nini? Na basha anatenda uadilifu gani? Kama sio yule ibilisi na nyoka wa kale akiwa kazini kupotosha kazi njema ya Muumba? Watu hawa sawa na ufunuo 2:9 wao ni sinagogi la shetani, aya haisemi kwamba ni wa sinagogi, bali wao ni sinagogi la shetani. Wameyaacha ya asili na kuyatukana matukufu sawasawa na injili ya Yuda inavyowazungumzia. Na ni kwa nini watu wahitaji kutafsiriwa Neno la Mungu? Jengeni tabia ya kusoma neno la Mungu wenyewe na kujinasua na huu mtego wa viongozi wa dini wanaoikasimu nafasi ya shetani, kuwafasiria neno. Roho mtakatifu wa neno ni kila kitu anachohitaji mwamini wa kweli..
   
 6. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #6
  Jun 22, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Dini inatakiwa isimamie misingi iliyokuwapo tangu uanzishwaji wake sio iwe kama koti likikubana unavua ukisikia joto unavaa liwacha wakati wa baridi unalivaa. Dini ni vazi linalotakiwa livalie wakati wote na muumini. Wenzetu kazi mnayo ila mrejee kwenye maandiko yenu ikiwa mnayaamini

  " Au, je, hamjui kwamba watu wabaya hawataurithi Utawala wa Mungu? Msijidanganye! Watu wanaoishi maisha ya uasherati, wanaoabudu sanamu, wafiraji au walawiti, wanyang'anyi, wachoyo, walevi, wenye kusengenya, walaghai, hao wote hawatashiriki Utawala wa Mungu" (1Wakorinto 1:9).

  Wakati sisi tunaishikia bango kubwa hali ya mtu kuvutiwa na jinsia yake, wakati tunalaani matendo ya kulawiti, ku****, usenge, ushoga na usagaji, Paulo, anazichanganya dhambi hizi na dhambi nyinginezo kama vile uchoyo, ulevi, kusengenya na kulaghai. Na bahati mbaya hakutofautisha ili kuonyesha ni dhambi ipi ni ndogo na ipi ni kubwa. Kama ushoga na usagaji zingelikuwa ni dhambi kubwa kuliko nyingine, basi Paulo, angezitaja peke yake ili kuuonyesha mkazo. Lakini yeye anaziweka kwenye ngazi moja na dhambi nyingine. Tuna watu wangapi katika jamii zetu wanaosema uongo, walevi, walaghai na wanaosengenya? Na je hawa tumewashikia bango mara ngapi kama tunavyowashikia mashoga? Je, wachoyo ni wangapi? Dunia yetu imegawanyika katika makundi ya maskini na matajiri kwa sababu uchoyo wa mali ni mkubwa sana. Hili tumelishikia bango? Hili tunalilaani kama tunayolaani ushoga na usagaji? Katika hali ya kawaida uchoyo wa mali ni dhambi kubwa, maana uchoyo wa mali unasababisha vita, mashindano na kuvuruga amani katika dunia yetu. Ushoga umeleta vita? Umeleta matabaka katika jamii? Hili ni jambo la kujadiliana kwa kina na wala si kulipinga kwa kufuata mkumbo.

  Pia tukiangalia Barua ya Paulo kwa Waroma tutakutana na kitu kilele:
  " Kwa hiyo, Mungu amewaacha wafuate tamaa mbaya. Hata wanawake wanabadili matumizi yanayopatana na maumbile ya miili yao kwa yale yasiyopatana na maumbile. Nao wanaume hali kadhalika, wanaacha kufuata matumizi ya maumbile ya mume na mke wakawakiana tamaa wao kwa wao. Wanaume wanafanyiana mambo ya aibu, na hivyo wanajiletea wenyewe adhabu wanayostahili kwa vitendo vyao viovu…Wamejaa kila aina ya uovu, dhuluma, ulafi na ufisadi. Wamejaa wivu, uuaji, ugomvi, udanganyifu na nia mbaya; husengenya, na kusingiziana……" (Waroma 1:18-32).

  Hivyo kufuatana na maoni ya Paulo, ugomvi, uuaji, wivu, udanganyifu, dhuluma, ulafi na ufisadi, ni tamaa mbaya kama ilivyo kuacha kufuata matumizi ya maumbile ya mme na mke na watu kuwakiana tamaa wao kwa wao (wanawake kwa wanawake na wanaume kwa wanaume). Kwa maoni ya Paulo, hizi ni dhambi ambazo ni lazima zishughulikiwe kwa pamoja.

  Barua ya kwanza ya Paulo kwa Timoteo, inafafanua vizuri kile ninachotaka kusema:
  " Twajua kwamba Sheria ni njema, kama ikitumiwa ipasavyo. Lakini tunapaswa kukumbuka kwamba sheria haziwekwi kwa ajili ya watu wema, bali kwa ajili ya wahalifu na wasiotii, wasiomcha Mungu na wenye dhambi, watu wasio na dini na wa kidunia. Watu wanaowaua baba na mama zao, au wauaji wowote wale; sheria imewekwa kwa ajili ya waasherati, wafiraji, wanaowaiba watu, waongo, na wanaoapa uwongo au wanaofanya chochote ambacho ni kinyume cha mafundisho ya kweli." (1 Timoteo 1:8-10).

  Kama tunasema kwamba ushoga na usagaji ni kinyume na maumbile, kama tunasema mashoga na wasagaji wana kasoro, ni wagonjwa na wana kilema kikubwa, basi tukubali kwamba na wasema uongo, walafi, mafisadi, wasengenyaji wana kasoro, ni wagonjwa wana kilema kikubwa na wanaishi kinyume na maumbile!

  Hata tukiachana na Biblia. Tukiangalia Mwongozo wa kanisa Katoliki kuhusu swala hili uliotolewa Desemba 1975 na ule wa Kadinali Ratzinger, yote inakazia Utafiti juu ya hali ya mtu kuvutiwa na jinsia yake. Je jambo hili limefanyika? Tuangalie hapa Tanzania. Utafiti huu umefanyika? Kanisa katoliki la Tanzania limejenga mazingara ambamo watu wenye kilema hiki wanaweza kujitokeza wazi na wakakubalika na kusaidiwa bila kungoja matukio kama lile la padri kulawiti. Kadinali Ratizinger, alishauri kwamba watu wenye matatizo haya wasitengwe, wapatiwe huduma zote za kiroho, wasikilizwe na kusaidiwa kwa kutumia hekima na busara kubwa. Tumesikia kwamba huyu Padri aliyelawiti, amesimamishwa kutoa huduma za kiroho. Je, huku si kumtenga? Kama kuna mapadri wengine wenye matatizo kama haya watakubali kujitokeza ili wasaidiwe? Je, kama kuna waumini wengine wenye matatizo kama haya watajitokeza? Kama padri amesimamishwa kutoa huduma za kiroho si waumini wakijitokeza watafungiwa huduma za sakramenti na kutengwa na kanisa?

  Tusikae kimya. Tujadiliane, tufanye utafiti, tuelimishane na kusaidiana ili tuweze kuendelea kuishi hapa duniani kwa furaha, heshima na matumaini.
   
 7. A

  Anold JF-Expert Member

  #7
  Jun 22, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 297
  Trophy Points: 180
  Mapepo makubwa hayoo! Hao sio wakristo wa kweli ni maajenti wa shetani. Huo moto wa sodoma ningeomba uteketeze watu kama hao wanaomtukana Mungu asubuhi kweupe.
   
 8. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #8
  Jun 22, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Mkristo wa kweli Kadinali Ratzinger (sasa ni Papa Benedict wa 16) Tarehe 1Oktoba 1986 Kadinali Ratzinger (sasa ni Papa Benedict wa 16), alitoa mwongozo wa Kanisa Katoliki juu ya watu wanaovutiwa na jinsia zao (homosexuality). Mwongozo huu ilikuwa ni barua aliyowaandikia Maaskofu wote wa Kanisa Katoliki:
  "ON THE PASTORAL CARE OF HOMOSEXUALS". Katika barua hii Kadinali Ratzinger, aliwakumbusha maaskofu juu ya mwongozo mwingine kuhusu swala hili hili uliotolewa Desemba 1975: " Declaration of Certain Questions Concerning Sexual Ethics" uliosisitiza kwamba hali ya mtu kuvutiwa na jinsia yake ifanyiwe utafiti na ichukuliwe kwa uangalifu na busara.

  Katika barua hiyo Kadinali Ratzinger, aliwashauri maaskofu kwamba hali ya mtu kuvutiwa na jinsia yake inahitaji wachungaji (mapadri) wenye kufanya utafiti kwa uangalifu mkubwa, wenye kujali, wa kweli na wenye theolojia isiyokuwa ya msimamo mkali.

  Ingawa Kadinali Ratzinger, anapinga hali hii na kuiona kama hali Fulani ya ugonjwa na kufanya mambo kinyume na maumbile, anashauri watu wenye matatizo ya kuvutiwa na jinsia zao wasitengwe. Wapatiwe huduma za kiroho, washauriwe na kuvumiliwa hadi pale watakapobadilika.

  Tatizo linalojitokeza kwenye barua hii ni kwamba Kadinali Ratzinger, anapinga hali hii kwa kutumia biblia. Msingi mkubwa wa hoja yake ni Biblia. Mfano anatumia kitabu cha mwanzo ambacho kinaelezea kwamba Mungu, aliwaumba Mwanamke na Mwanaume. Pia katika agano jipya anatoa mifano ya Mtakatifu Paulo anapolaani vitendo vya kulawiti na ku****. Kimsingi ameqoute aya inayochanganya dhambi ya ku**** na dhambi ndogo ndogo ili kuamsha mjadala na kusimamia utetezi wake kwa mapadri wafiraji wa kanisa la Roma.

  http://www.vatican.va/roman_curia/congregations/cfaith/documents/rc_con_cfaith_doc_19861001_homosexual-persons_en.html
   
 9. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #9
  Jun 22, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Shuzi limepata Mjambaji lol!
   
 10. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #10
  Jun 22, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,205
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  shosi again!!
  Shetani anao uwezo wa ku-quote maandiko, kama alivyofanya alipokuwa akishindana na Yesu kwa kumwambia 'imeandikwa'.
  Lakini andiko huua bali roho iliyoko ndani ya neno la Mungu, huhuisha. Shetani anaweza kuigiliza(impersonate) kila kitu, ila tu tunda la roho mtakatifu.
  Kanisa haliongozwi kama watu wafikirivyo, bali ni Roho mtakatifu akiliongoza kanisa kwa neno lake kupitia watu. Sasa sharti watu hao wawe wamezaliwa personal na hilo neno na kubatizwa ubatizo wa kiroho wa roho mtakatifu. Sasa tunachopingana nacho na huu uhuni wa shetani kutaka kumfanya mtu ambae hajazaliwa mara ya pili kuwa kiongozi wa kiroho. Huu ndio ushetwain uliopindukia mipaka na kama uliwahi kusikia mfumo wa kibabeli (babilone system) ndio huu. Ndugu yangu shosi kama wewe ni shoga/basha ama msagaji unakaribishwa kwa Yesu kwa heshima zote ili katika neno kukuzaa upya uachane na matendo yako mafu ya kale. Lakini kama bado umeyashikilia hayo kama sehemu yako, sahau kabisa kuhusu ufalme wa Mungu. Labda tu kitu unachoweza pata ni ushiriki/uongozi katika madanguro yenye kila namna za matendo ya kuzimu yanayojinasibu kwa jina la kanisa. Hivyo usione ajabu kuwekwa mzee, shemasi, kasisi, kuhani nk, huko, pamoja na ushetani uliojisajili kwao.
  .
   
 11. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #11
  Jun 22, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Hilo kanisa la anglikana Uingereza linahitaji wamisionari kutoka nchi nyinginezo wakawahubiri injili sahihi.
   
 12. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #12
  Jun 22, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Sasa ikiwa Kadinali Ratzinger (sasa ni Papa Benedict wa 16) na kanisa la kilutheri vinatetea haya mambo ya ushoga nyie waumini mnalionaje hiliswala? nini mfanye ili kurudi kwenye maandiko na mafundisho ya Yesu?
   
 13. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #13
  Jun 22, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Mkuu hata hao wamissionari wengine wanapigia upatu hayo mambo na hata Kadinali Ratzinger (sasa ni Papa Benedict wa 16) Tarehe 1Oktoba 1986 Kadinali Ratzinger (sasa ni Papa Benedict wa 16), alitoa mwongozo wa Kanisa Katoliki juu ya watu wanaovutiwa na jinsia zao (homosexuality). Mwongozo huu ilikuwa ni barua aliyowaandikia Maaskofu wote wa Kanisa Katoliki:
  "ON THE PASTORAL CARE OF HOMOSEXUALS". Katika barua hii Kadinali Ratzinger, aliwakumbusha maaskofu juu ya mwongozo mwingine kuhusu swala hili hili uliotolewa Desemba 1975: " Declaration of Certain Questions Concerning Sexual Ethics" uliosisitiza kwamba hali ya mtu kuvutiwa na jinsia yake ifanyiwe utafiti na ichukuliwe kwa uangalifu na busara. Anataka busara na uangalifu kwa kuzingatia haki za kibinadamu.
   
 14. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #14
  Jun 22, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Mungu sio mjinga kumuumba Adamu na Hawa/Eva..
   
 15. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #15
  Jun 22, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Yaani wanaume kwa wanaume wanapigana ndonga halafu ndio waniongoze kwenye Ibada huu upuuzi siwezi kuukubali
   
 16. W

  WIERD Member

  #16
  Jun 22, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yeah its th end f days!
   
 17. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #17
  Jun 22, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  sipati picha akiwa madhabahuni akihubiri...mikono na midomo ikibinuliwa.
  Tubuni,Yesu Yu Aja.
   
 18. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #18
  Jun 22, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Dhambi ni dhambi. Hakuna ndogo wala kubwa zote ni dhambi. Na dhambi zote zinatakiwa kukemewa na watu kumwomba Mungu msamaha. Ushoga ni dhambi kama dhambi nyingine yoyote na mshahara wa dhambi ni mauti. Hili kanisa haliko sahihi kwa mwenendo huo wa kusupport ushoga ama mapadre mashoga. Limekuwa kanisa la kisodoma na Gomorrah
  Ratzinger yuko sahihi ktk hilo la kupinga ushoga lakini ikumbukwe pia kuna mapungufu makubwa sana katika kanisa lake la Roman Catholic.
   
 19. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #19
  Jun 22, 2011
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Naomba kuuliza: hivi Kanisa la Anglikana nalo lina mapadre (priests), ambao huwa tunaona kifupi chake ni mfano Fr MCDonald Williams au tunatumia neno mapdre tu kama tunavyotaka? Naona mnieleweshe wanaJF wenzangu.
   
 20. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #20
  Jun 22, 2011
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  As far as I'm concerned any person who is heterosexual, homosexual, bisexual or transsexual can become a pastor, a priest, a bishop or pope. Nobody sins because of his or her sexual orientation. One can sin only if he or she breaks God's commandments and not being heterosexual, homosexual or bisexual or transsexual.
   
Loading...