Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,744
- 25,446
Nia ya Rais ya kufufua haya mashirika ya Umma ilikuwa njema lakini naona shughuli yake inaenda kuwa pevu.
Kwa mara nyingine jana nilikwenda kubadili fedha kwenye duka la Shirika la Posta Masaki. Mara ya mwisho kwenda pale wahudumu waliokuwepo waliniambia anayehusika na kitengo cha kubadili fedha ana msiba!
Jana alikuwepo na alinibadilishia isipokuwa alisema hawatoi risiti! Nikamuuliza kwa nini, akaniambia mashine ni mbovu na amewatumia wakubwa taarifa mara nyingi lakini mafundi hawajaletwa. Pia alinionya kuwa mashine inatengenezwa mara kwa mara lakini huwa haichelewi kufa
Najiuliza, pamoja na upendeleo huu wa kibiashara, mashirika haya yabebewe mbeleko gani ili yaweze kujiendesha kibiashara? Najiuliza, hali ingekuwaje kama duka binafsi lingebainika kubadili fedha bila kutoa risiti? Lingepewa kesi ya namna gani?
Credit: James Gayo