Mashinikizo toka mataifa ya nje ndiyo njia pekee ya kuudhibiti utawala huu wa Magufuli

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,484
30,160
Tumeshuhudia tokea utawala huu wa awamu ya 5 uingie madarakani, kukifanyika juhudi kubwa sana ya kutaka nchi hii irejee kwenye mfumo wa Chama kimoja.

Tunashuhudia katika nafasi zake za uteuzi, namna ambavyo Rais anavyojitahidi kuwateua makada wa CCM wa kiwango cha "die hard supporters" kuwa ndiyo maDC, maRC na maDED, jambo linalofanya viongozi wa vyama vya upinzani, hususani wa Chadema, kuwa "treated" kama wahaini ndani ya nchi yao!

Hivi unawezaje kuieleza hali ya viongozi wote wa ngazi ya juu wa Chadema kuwa na kesi mbalimbali kwenye mahakama zetu na baadhi ya viongozi hao akiwemo, mbunge Sugu na LijuaLikali kuhukumiwa vifungo jela kwa makosa ya kisiasa na hata mbunge Godbless Lema kusota rumande kwa takribani miezi 4 na hivi sasa tunavyoongea, kiongozi wa Chama kikuu cha upinzani nchini, Freeman Mbowe na Mbunge mwenzie, Esther Matiko, wanaendelea kusota rumande kwa zaidi ya miezi miwili hivi sasa, kwa makosa ya kisiasa, kama siyo kwa viongozi hao kuwa "treated" kama wahaini??

Tumeshudia pia kwa mara ya kwanza katika historia ya mfumo wa vyama vingi nchini vya siasa nchini, kwa hoja za kisiasa zikijibiwa kwa "pyupyu" badala ya kujibiwa kwenye majukwaa ya kisiasa!

Tumeshuhudia pia namna Tume ya uchaguzi ilivyojigeuza kuwa Tume ya CCM ikiwa "assisted" kwa karibu na Jeshi la Polisi nchini

Rejea tukio la Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, hivi karibuni kuwafanyia sherehe za kuwapongeza Askari Polisi, kwa "kuwezesha" kupatikana ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo la Ukonga,

Rejea pia kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, aliyoitoa siku za karibuni alipomuhakikishia Rais Magufuli kuwa mwaka 2020 atamkabidhi Mkoa wa Dar, ukiwa na wabunge na madiwani wote wa CCM!

Kutokana na mwenendo huo wa kisiasa usioridhisha nchini na kumfanya mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, kuongea katika kipindi cha Hardtalk cha BBC, hadi kusababisha awe na "followers" zaidi ya milioni 90 duniani kote, hali iliyosababisha taharuki kubwa serikalini na viongozi hao waandamizi kumwita Tundu Lissu kuwa amekosa uzalendo na kuamua kuisema vibaya nchi yake.

Katika siasa ninachokijua ni hoja kujibiwa na hoja. Kwa maana hiyo ndiyo sababu.mtangazaji huyo wa kipindi hicho cha Hardtalk, Steve Sackur, alitoa mwaliko kwa Rais Magufuli kwenda jibu mapigo ya Lissu kwenye kipindi kingine atakachokiandaa cha Hardtalk

Ninachofahamu ni kuwa kwenye vyombo vya habari vya wenzetu kuna "freedom of expression" na siyo kama hapa kwetu, ambapo najaribu ku-imagine hivi hilo shirika la utangazaji la BBC lingekuwa hapa kwetu nchini kwa kurusha kipindi kile cha Hardtalk hali ingekuwaje??

Nina uhakika wa asilimia 100 kuwa shirika hilo la utangazaji la BBC lingefungiwa maisha kwa sababu ambazo zingetolewa kama kawaida na viongozi wa.serikali kuwa chombo hicho kimeleta habari za uchochezi na kimekosa uzalendo na kinatumiwa na mabeberu!

Nimsihi na kumhimiza Tundu Lissu, kuwa aendelee na ziara yake huko Ulaya na Marekani na kuieleza dunia kuwa kwa kunyimwa haki zake za matibabu na Bunge, ambapo ni kwa mujibu wa kanuni za Bunge hakikuwa kitendo sahihi na kinapaswa kulaaniwa na dunia nzima

Ninaamini njia anayotumia Tundu Lissu ndiyo sahihi kabisa ya kuweza kuueleza Ulimwengu matendo aliyofanyiwa yalikuwa ni ya kinyama uliopitiliza na naiona njia hiyo kuwa ndiyo pekee iliyobaki ya kuirejesha nchi yetu kwenye utawala bora unaojali sheria

Ingawa kwa kukatwa misaada hiyo kutaathiri hali ya maisha ya watanzania walio wengi, lakini mbinyo wa kukata misaada kutoka taasisi za fedha za dunia kama vile Benki ya dunia na Jumuiya nyingine za kimataifa ndiyo njia pekee iliyosalia kwa serikali hii kusalimu amri.
 
Hivi inakuwaje kwa Spika Ndugai kuonekana alikuwa amem-miss sana Tundu Lissu hadi amtake arejee haraka nyumbani??

Hivi si ndiyo huyu huyu Spika Ndugai aliyemnyima Tundu Lisssu stahiki zake za kutibiwa, ingawa ni kwa mujibu wa kanuni zao za Bunge??

Hivi inawezekanaje, Paul Makonda amdhihaki Tundu Lissu kuwa ni mgonjwa wa akili, hadi apendekeze kuwa akirudi apelekwe Mirembe kwenda chekiwa??

Hivi hajawahi msikia Mkuu wake kwenye ziara zake kanda ya ziwa akiwaambia wananchi wa kule kuwa yeye ni kichaa na hivyo kwenye utawala wake anawateua vichaa wenzake??

Hivi ni nani hasa anayestahili kupelekwa Mirembe kati ya Tundu Lissu na Jiwe??
 
Tundu Lisu ni habari nyingine kabisa.
Ni Level ya watu mashuhuri wa enzi za wapigania Uhuru kama akina Nelson Mandela,Julius , Kwame ,Dr. Martin Luther ,Mahatima Ganz na wengine.

Nitawaunga mkono nchi kubwa endapo watamteua Tundu Lisu kwenye Nafasi mojawapo za juu huko UN.

Hata Hivyo Mbowe kuendelea kukaa Gerezani ni jambo la heshima kwa Taifa na ujenzi wa Demokrasia makini na ya kweli ndani na nje ya vyama.

Mbowe amesababisha vyama vya upinzani kujitambua zaidi.
Nadhani huko gerezani alipo patampa elimu kubwa zaidi na ufahamu zaidi.

Kati ya mambo ya maana yaliyofanyika awamu hii ni pamoja na hili la kuhakikisha Mbowe anafuata sheria na kanuni kwa kumtia adabu.

Mbowe ni tatizo sana katika ukuaji wa Demokrasia ndani ya Chadema na taifa kwa ujumla.
Vurugu nyingi ndani ya Chadema zilikua zinaasisiwa na Mbowe na kundi lake na yeye alikua wanaovuruga chama alimradi wawe upande wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acheni uvivu wenu na kufikiri kukaa nyuma ya keyboard na kupepeta na kubwabwaja midomo ndio itawawekea chakula mezani, kwendraaaaa fanya kazi kupe wewe walahi
Wadhungu wamesha washtukia mapiga deal, dadeki malofa mtakula lami walahi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumeshuhudia tokea utawala huu wa awamu ya 5 uingie madarakani, kukifanyika juhudi kubwa sana ya kutaka nchi hii irejee kwenye mfumo wa Chama kimoja.

Tunashuhudia katika nafasi zake za uteuzi, namna ambavyo Rais anavyojitahidi kuwateua makada wa CCM wa kiwango cha "die hard supporters" kuwa ndiyo maDC, maRC na maDED, jambo linalofanya viongozi wa vyama vya upinzani, hususani wa Chadema, kuwa "treated" kama wahaini ndani ya nchi yao!

Hivi unawezaje kuieleza hali ya viongozi wote wa ngazi ya juu wa Chadema kuwa na kesi mbalimbali kwenye mahakama zetu na baadhi ya viongozi hao akiwemo, mbunge Sugu na LijuaLikali kuhukumiwa vifingo jela kwa makosa ya kisiasa na hata mbunge Godbless Lema kusota rumande kwa takribani miezi 4 na hivi sasa tunavyoongea, kiongozi wa Chama kikuu cha upinzani nchini, Freeman Mbowe na Mbunge mwenzie, Esther Matiko, wanaendelea kusota rumande kwa zaidi ya miezi miwili hivi sasa kama siyo kwa viongozi hao kuwa "treated" kama wahaini??

Tumeshudia pia kwa mara ya kwanza katika historia ya mfumo wa vyama vingi nchini vya siasa nchini, kwa hoja za kisiasa zikijibiwa kwa "pyupyu" badala ya kujibiwa kwenye majukwaa ya kisiasa!

Tumeshuhudia pia namna Tume ya uchaguzi ilivyojigeuza kuwa Tume ya CCM ikiwa "assisted" kwa karibu na Jeshi la Polisi nchini

Rejea tukio la Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, hivi karibuni kuwafanyia sherehe za kuwapongeza Askari Polisi, kwa "kuwezesha" kupatikana ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo la Ukonga,

Rejea pia kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, aliyoitoa siku za karibuni alipomuhakikishia Rais Magufuli kuwa mwaka 2020 atamkabidhi Mkoa wa Dar, ukiwa na wabunge na madiwani wote wa CCM!

Kutokana na mwenendo huo wa kisiasa usioridhisha nchini na kumfanya mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, kuongea katika kipindi cha Hardtalk cha BBC, hadi kusababisha awe na "followers" zaidi ya milioni 90 duniani kote, hali iliyosababisha taharuki kubwa serikalini na viongozi hao waandamizi kumwita Tundu Lissu kuwa amekosa uzalendo na kuamua kuisema vibaya nchi yake.

Katika siasa ninachokijua ni hoja kujibiwa na hoja. Kwa maana hiyo ndiyo sababu.mtangazaji huyo wa kipindi hicho cha Hardtalk, Steve Sackur, alitoa mwaliko kwa Rais Magufuli kwenda jibu mapigo ya Lissu kwenye kipindi kingine atakachokiandaa cha Hardtalk

Ninachofahamu ni kuwa kwenye vyombo vya habari vya wenzetu kuna "freedom of expression" na siyo kama hapa kwetu, ambapo najaribu ku-imagine hivi hilo shirika la utangazaji la BBC lingekuwa hapa kwetu nchini kwa kurusha kipindi kile cha Hardtalk hali ingekuwaje??

Nina uhakika wa asilimia 100 kuwa shirika hilo la utangazaji la BBC lingefungiwa maisha kwa sababu ambazo zingetolewa kama kawaida na viongozi wa.serikali kuwa chombo hicho kimeleta habari za uchochezi na kimekosa uzalendo na kinatumiwa na mabeberu!

Nimsihi na kumhimiza Tundu Lissu, kuwa aendelee na ziara yake huko Ulaya na Marekani na kuieleza dunia kuwa kwa kunyimwa haki zake za matibabu na Bunge, ambapo ni kwa mujibu wa kanuni za Bunge hakikuwa kitendo sahihi na kinapaswa kulaaniwa na dunia nzima

Ninaamini njia anayotumia Tundu Lissu ndiyo sahihi kabisa ya kuweza kuueleza Ulimwengu matendo aliyofanyiwa yalikuwa ni ya kinyama uliopitiliza na naiona njia hiyo kuwa ndiyo pekee iliyobaki ya kuirejesha nchi yetu kwenye utawala bora unaojali sheria

Ingawa kwa kukatwa misaada hiyo kutaathiri hali ya maisha ya watanzania walio wengi, lakini mbinyo wa kukata misaada kutoka taasisi za fedha za dunia kama vile Benki ya dunia na Jumuiya nyingine za kimataifa ndiyo njia pekee iliyosalia kwa serikali hii kusalimu amri.
Historia ni mwalimu mzuri. Wapinzani wa Mubarak, Qaddafi, Saddam na Al Assad walikimbilia huko pia kutafuta uungwaji mkono. Sote tunajua kilichofuatia. Uchu wa madaraka ni hatari mno

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Back
Top Bottom