duh interpreneur inabidi ubadili jina ujiite google lol! Full data maswali yote humu umeyajibu na umepata 100/100
ila kwa kuongezea tu hata mi ninayo kwa mfuko mmoja wa sement napata tofali 120 udongo natumia vumbi la mawe au wanaita ''morram'' mashine inahitaji kumwagiwa oil mara kwa mara ratio ya udongo na cement ni 1:40 maji ndoo 3 za lita 20 ila hii ratio inategemea na aina ya udongo na kiasi cha mfinyanzi kwenye udongo ila kuna mashine zake za kutumia disel au umeme zinatoa tofali zinazolingana na kwa siku fundi3 wanapiga tofali 500 wakichoka 400 ila haivunji kiuno na ukinunua mashine kwa hawa wa tba au nhbc wanatoa training bure kwa vijana utakao watumia kukufanyia kazi hadi wafuzu tayari kufanya biashara au kujengea nyumba yako. Yako economic unasave hela ila yanatumia maji mengi kumwagiliwa kama ya tofali za cement za kawaida. Ukihitaji tufanye biashara kwa anayetaka nauza tofali moja sh. 900 hapa utajenga nyumba bila kuwa fisadi