Hii issue simple sana ya kujitengenezea mkaa mwenyewe, baada ya utafiti nimegundua ni raw materials gani na jinsi gani. Kuna namna nyingi na machine tofouti za kutengenezea ambazo unaweza kubuni mwenyewe.
Swali kubwa Raw materials gani, hapa unatakiwa uwe na sawdust pamoja na makaratasi na maji. mchanganyiko ratio 2parts sawdust 1part paper. Changanya vyote na maji, maji moto yanafanya process iwe haraka ya kulainisha karatasi au unaweza kuwacha usiku kucha mchanganyiko huu. Stage ya mwisho ni kuondoa maji kutoka mchanganyiko kwa njia ya compression, hapana nadhani hata mashine ya kufyatua tofali ya mkono itafaa kwa ajili ya kukandamiza maji yote yatoke na hapo utapata tofali la mkaa, ni muhimu kukausha kwa siku kadhaa ili moto uwake. I hope niweza kuwapa idea ingawa ubunifu ni muhimu sana na kila mtu anaweza kufanya kivyake, ukikosea mara ya kwanza jaribu tena na tena. Nawasilisha.
View attachment 158539View attachment 158540View attachment 158541View attachment 158542