Mashine ya kuinua matiti ya wanawake yaingia nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashine ya kuinua matiti ya wanawake yaingia nchini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Candid Scope, Mar 11, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  WANAWAKE WAFURIKA KUPATA HUDUMA
  BIASHARA huria imezua mengi. Hali kadhalika Sayansi na Tekenolojia nayo, imeleta mengi. Katika kuwaondolea kero wanawake wenye matiti yaliyosinyaa hapa nchini, wataalamu kutoka China wameanza kutoa huduma ya kunyanyua matiti hayo kwa kutumia mashine maalumu.
  Wachina wamejipatia umaarufu katika kuleta bidhaa mbalimbali hapa nchini, zikiwamo za kuongeza nguvu za kiume, kupunguza uzito, kuotesha nywele, kujichubua (kumfanya mtu mweusi awe mweupe), kuongeza makalio nk.

  Huduma hiyo ya kusimamisha matiti yaliyolala, imeanza kutolewa katika Saluni ya Blue Palace, iliyopo nyuma ya Shule ya Mapambano, Sinza jijini Dar es Salaam.
  Haikuwa rahisi kuweza kuamini kuwa vitu kama hivi vinaweza kupatikana Tanzania. Mwananchi Jumapili lilifunga safari mpaka kwenye saluni hiyo inayomilikiwa na Sarafina Mtweve, kujionea jinsi teknolojia hiyo inavyofanya kazi. Mbali na meneja wa saluni hiyo, Trust Mwembe, pia alikuwepo mtaalamu kutoka China aitwaye, Ciisy Pang, ni binti wa miaka 23 tu, lakini anasema kwa miaka minne amefanya kazi hiyo na kuwasaidia wanawake mbalimbali waliokuwa wakikerwa na matiti yaliyolegea au kuanguka.


  Pang na kundi lake wanatoa huduma hii kwa gharama ya Sh150,000 kwa kuanzia, ingawa wanahisi gharama hizo zitapanda katika siku chache zijazo.


  Jinsi matiti yanavyosimamishwa
  Mashine hiyo inayoitwa ‘Beauty Machine' ina uwezo wa kusimamisha matiti ya kila saizi kwa kuwa huambatanishwa na vibakuli (cups) kama unavyoona pichani.
  Kazi kubwa ya mashine hiyo ni kuamsha misuli ambayo hushikilia nyama za matiti. Pang anasema, zoezi la kusimamisha matiti huchukua wiki tatu mpaka sita, inategemea aina ya mteja na wakati mwingine juhudi zake.


  Mtaalamu huyo ambaye anazungumza Kichina na kutafsiriwa na meneja wa saluni hiyo, anaelezea namna anavyofanya kazi ya kuyarudisha matiti kwa muda huo.
  "Kwanza unapaswa ujue kuwa hatutumii dawa yoyote katika zoezi hili, mteja wetu akifika hapa, kinachotumika ni mashine tu ambayo hutumia umeme kama zilivyo dryer za nywele, "Baada ya kumlaza katika kitanda kile, tunachukua kitu mfano wa bakuli (cups) mbili kulingana na ukubwa wa matiti yake, tunayatumbukiza humo, kisha tunawasha mashine," anasema Pang.


  Mtaalamu huyo anasema mashine hiyo ikiwashwa inavuta kama ‘vacuum', na inaweza kuongezwa kasi au kupunguzwa kama inavyofanyika kwenye mashine za kufanyia mazoezi.
  "Tunaiwasha mashine kwa muda wa dakika 45, mteja atachagua siku mbili katika wiki za kufanya zoezi hili mpaka litakapokamilika,"anasema Pang. Tangu mashine hiyo iwasili nchini, takribani mwezi mmoja uliopita, Pang anasema ana wateja wanane anaowahudumia kwa nyakati tofauti ambao wamekiri kuwa maendeleo yanatia moyo.


  Ni kweli mashine hii inasaidia?

  Akizungumza kwa njia ya simu, mmoja wa wateja anayepata huduma hiyo ambaye alijitambulisha kwa jina moja tu Irene anasema, ni wiki ya tatu sasa tangu aanze kupata huduma hiyo, anakiri kuwa matiti yake sasa yameanza kuwa magumu tofauti na mwanzo.
  "Kusema kweli nilikuwa na matiti yaliyosinyaa wala si kulala tu kama ulivyouliza, ila naona sasa yameanza kuwa magumu na kurudi juu kidogo," anasema Irene. Akizungumzia ugumu anaoupata katika zoezi hilo, anasema safari za kila wiki saluni na zile dakika 45 za kukaa kwenye mashine zinamchosha, lakini kwa kuwa amedhamiria, amejitoa mpaka zoezi hilo litakapokamilika.

  Matiti yanaweza kulegea tena?

  Pang anasema kama matiti yanalegea kwa sababu fulani mfano uzazi wa watoto wengi, basi yanaweza kulegea tena kama mtu atajifungua na kunyonyesha kwa muda huo.Aidha anasema wanawake wenye matiti makubwa, ni rahisi kuanguka kama hawatayavalisha sidiria kwa muda mrefu. "Wanawake wenye matiti makubwa huwa nawashauri kuvaa sidiria hasa wakati wa mchana na usiku wanaweza kuacha kuzivaa, hii inasaidia kuimarisha misuli inayoyabeba matiti," anasema Pang.

  Jamii inazungumziaje jambo hili

  Baada ya kusikia kuwepo kwa mashine hii nchini, wanawake mbalimbali wamesema wanatamani kupata huduma hiyo lakini wengine, walionyesha woga juu ya matokeo yake.
  "Ni kweli baada ya kunyonyesha watoto wawili sasa matiti yamelegea kabisa, natamani yarudi kama wakati ule wa usichana wangu, lakini nahofia huenda mbele ya safari nikapata madhara," anasema Linda Masatu. Linda anaongeza kusema kuwa ni vizuri mwanamke akawa na matiti yaliyojaa vizuri, lakini anahofia njia zinaweza kuwa na madhara, huku akisema kama ingetokea njia nyingine ya asili asingesita kuifuata.

  Naye Batuli Famau, anasema mwanamke anapokuwa na matiti yaliyosinyaa mvuto wake hupungua, hata anapovaa sidiria anakuwa amebadili mwonekano wa nje tu, lakini ndani bado anakuwa vilevile.
  "Mwanamke mrembo ni yule mwenye matiti mazuri, sasa inapobidi kutumia njia fulani ili yarudi kama tulipokuwa vigoli, tutafanya tu ili mradi kama njia hizo hazitatuangamiza," anasema


  Wanaume nao wameonekana kuunga mkono zoezi la kusimamisha matiti ingawa wengine hawaungi mkono utumiaji wa mashine hii.
  Augustino Magara anasema: "Ni kweli mwanamke mwenye matiti magumu anavutia kuliko yaliolegea na kulala, lakini sasa tuwe makini kabla wake zetu hawajaumia katika mashine, hizi" "Wote tunajua sababu zilizosababisha matiti ya wake zetu yalegee, sioni sababu ya kusema tunataka yaliyomagumu, tuwapende wake zetu hivi hivi na tuwape moyo," anasema Nganara.


  Dk Innocent Mosha wa Kitengo cha Patholojia Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, anasema ni vigumu kwa wataalamu wa afya kugundua madhara ya mashine hizo kwa haraka hadi pale uchunguzi utakapofanyika.
  "Ingelikuwa mazoezi hayo yanachukua muda mfupi, kweli tungepata wasiwasi kwa kuwa, unapoisimamisha misuli kwa haraka ni lazima madhara yatokee, lakini hili la mazoezi, bado sifahamu," anasema Dk Mosha.
   
 2. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  vitoy vya kichina...it just stimulates muscules lakini sio suluhisho. .ukiacha ngima lazima ishuke
   
 3. Dunda kwetu

  Dunda kwetu JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 265
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kila jambo lina wakati wake.ikiwa matiti yame lala alaf nanihii iko freash :behindsofa:tatizo liko wapi eti wajameni
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Ni mradi endelevu, kwani muscules zinakuwa stimulated kwa muda tu kisha zinasinyaa tena na anatakiwa kurudia huko kila baada ya muda fulani. Hii ni sawa na watumia kudungwa sindano kuinua matiti, makalio, mashavu, au kutoa makunyanzi mwilini. Madhara yake baadaye mtu anapojikuta ana maradhi yasiyotibika ambayo chanzo chake ni tata.
   
 5. m

  moshingi JF-Expert Member

  #5
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 278
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umenena Mkuu, uzuri wa gari ni injini wala siyo bodi...ndiyo maana kuku wa kienyeji na bata wanauzwa ghali
  sana kuliko hao wenu wa mjini wa kuchakachua, wazuri rangi lakini injini mbovu....
   
 6. SIMBA WA TARANGA

  SIMBA WA TARANGA JF-Expert Member

  #6
  Mar 11, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 992
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Walah watoto wakinyonya hayo watakuwa mataahira, au mwanaasha.
   
 7. s

  sweke 34 JF-Expert Member

  #7
  Mar 11, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 694
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  matiti yakishalegea yamelegea hakuna jinsi...ladba kama wangekuwa wanafanya ile operation ya kuwawekea silicon indiyo yangeweza kusimama kama ya saa sita...!
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Ni dhahiri kila kitu na wakati wake. Wanawake wanatakiwa kunyonyesha watoto wao kwa miezi sita baada ya hapo mtoto anaweza kukua vizuri tu kwa kutumia chakula cha kawaida, wawasiliane na wataalamu wa lishe ya watoto watawapa taarifa ya chakula gani kinatakiwa kwa mtoto wa umri huo na atakua vizuri tu.

  Unyonyeshaji wa mtoto hadi mwaka mmoja au zaidi ni kumchosha mama yake ni si lazima sana, na hii kusababisha matiti ya mama misuli yake kutokuwa na nguvu kutosha kutokana na kunyumbuliwa pamoja na kufinywangwa mno na mtoto anaponyonya. Lakini utafiti umeonyesha wanawake wanaonyonyesha watoto wao kwa miezi sita tu matiti yao yanabaki na hali nzuri kwa asili mia kubwa kuliko wanaonyonyesha muda mrefu.

  Uvaaji wa sidiria nao husaidia kuyaweka maziwa vizuri na kubaki na umbo la mvuto, kuliko wanaoacha yabaki yalivyo na hatimaye kutokana na natural gravity hunyumbuka na kuwa tepetepe na kuishia kunyumbukia kujaa juu ya tumbo na hivyo kukosa mvuto stahiki.

   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hiyo ni mbaya zaidi ya kudungwa masindano ya kuwekewa silicon, maana madhara kwa afya ni mabaya zaidi. Nafuu hii ambayo inastimulate misuli na kuimarisha ili kujaza titi.
   
 10. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #10
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Hii huduma inapatikana pia kule Wapo Mission Kwa Gamanywa.Wale Wachina waliopo pale wanahudumia pia na kuongeza ubikira.Wanawake waliotibiwa wanalamika muwasho!
   
 11. Aleyn

  Aleyn JF-Expert Member

  #11
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 10,228
  Likes Received: 13,680
  Trophy Points: 280
  Hawa Watu mbona wanamwingilia sana Mungu katika Kazi zake,mara makilo,Bikira feki,kujichubua n.k
   
 12. N

  Njele JF-Expert Member

  #12
  Mar 11, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hawa wachina mambo yao yanapitiliza mno, sasa hii ya ubikira siipati vizuri, maana yake mwanamke ataanza upya kana kwamba ndo leo anaingia ulimwengu wa mahusiano au ni shauri ya kubana mizuli ya njia ya asili ionekane ndogo?
   
 13. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #13
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Nenda pale Wapo Radio uliza kitengo cha Tiba Lishe ,Omba kumuona Askof Gamanywa ndiye Mshauli wa huduma hiyo.Akina dada Wapendwa wanaokaribia kufunga ndoa wamechangamikia sana hiyo.Ila tatizo ni muwasho.
   
 14. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #14
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Wanajichubua mwili mzima isipokuwa sehemu za siri.Wachina wengi hawana makalio,hawanabikila wala hawana matiti yaliyosimama.Wametuletea nywele bandia (mawigi) ambapo wavaaji wakubwa ni Mch Rwakatare na Ana Makinda
   
 15. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #15
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Nimemuona mke wa Nabii Mwingira akiwa ameva mawigi na suluali iliyo na Mchongo kwenye makalio mithili ya Ikweta
   
 16. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #16
  Mar 11, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Au watayakuta yameganda
   
 17. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #17
  Mar 11, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Au waondoe gravitation force isiapply
   
 18. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #18
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kwa ulinganifu njia hii ni nafuu kwa madhara mwilini kuliko ile ya kudungwa sindano kuwekewa silicon mwilini ili kuumusha viungo kama maiti.
   
 19. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #19
  Mar 11, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Ndo mana majanga hayaishi, tunambipp mungu sana
   
 20. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #20
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hapo ndipo natural force inapolazimisha matiti kuelekea chini tumboni badala ya kubaki yamechuchumaa kifuani kama vilele vya mlima Kilimanjaro visivyotikisika. Wanawake wakubali tu kutumia sidiria kuyainua watokapo majumbani badala ya kuingia gharama ambazo zinaweza kuwaathiri kiafya ambazo ni endelevu na wabunifu ni kwa ajili ya msukumo wa kiuchumi zaidi kuliko huduma.
   
Loading...