A
Anonymous
Guest
Habarini, naleta taarifa hii kwa masikitiko makubwa sana...
Mashine ya CT SCAN katika hospitali ya Mloganzila ni mbovu takribani mwezi mmoja na nusu na hali ni mbaya, wagonjwa wengine inawapasa wapange foleni katika kupata huduma hii.
Ni aibu kwa Hospitali yenye hadhi ya TAIFA kama Mloganzila kukosa huduma hii muhimu, pamoja na jitihada za Mh Rais kukuza sekta ya afya lakini kuna baadhi ya watendaji wanamuangusha.
Wagonjwa wanahamishwa kutokea Muhimbili Mloganzila kwenda Muhimbili Upanga jambo ambalo ni usumbufu kwa wagonjwa na vilevile gari wanalotumia (Ambulance) sio salama kwa matumizi ya wagonjwa yaani limechakaa halifai ni basi tu wanaforce ili mambo yaende (NINGEWEKA PICHA YAKE MUONE ILA NAWASITIRI KWA MUDA)
Tunapaza sauti suala hili lifanyiwe kazi haraka na mashine irudi kwenye hali yake ya kawaida.
ASANTE