Ni kweli bwana bajabiri na uyasemayo, hasa kwa watoto wa kike kutaka kuendesha gari, kupata vihela labda vya kuanzisha biashara na kujikomboa. Lakini kwa makampuni kuwatumia mabinti zetu namna hii ni hatari sana. Mabinti zetu itakua rahisi kwao kufikiria kuwa haya mashindano ndio yatakayowatoa kwenye umaskini, si kweli, zaidi ya kuwaletea madhara.

Hatukatai kwa makampuni haya kutumia wanawake au wanaume, swala wanawatumia kwa njia zipi, kwanini wasi promote nembo na biashara zao kwa njia zilizotajwa nami na wadau wengine hapo juu?

Na hili swala la makelele mtaani ya promotions zao, litabidi nalo likomeshwe pia

Kila kukicha tunasikia na kuona mashindano ya u-miss, ina maana TZ kwa sasa haina njia nyingine ya kusaidia watoto wake wa kike zaidi ya kuwatembeza na kuwavalisha vichupi hadharani?
Kwani Voda, Airtel na TBL hawana mashindano mengine ya kusaidia watoto wa kike, kama ya business plan, kufanya vizuri O'level, A' level, vyuoni au kuwapa tuzo wale wanaosaidia jamii?
Wadau mnasemaje?

Hakuna faida wanazoPata! Ninaowafaham wote wana mitazamo ya kuwapata wanaume wenye vipato vizuri ili wawe karibu yao kimahusiano ili watimize malengo. Na huwapata kisha hutelekezwa! Sasa hayo si maadili mema kwa mabinti zetu.
Waamin wanatazamwa na kupata umaaruf kwenye hayo mashindano hivyo kupata matumain ya kutoka kwenye
jebs2002,

Ama kwa hakika hii ni moja katika mada nzuri sana nilizopata kuziona humu JF, nakupa pongezi kwa hilo.

Watoto wa kike wa Kitanzania, Waislaam kwa Wakristo, walio na dini na wasio na dini. Wanatembezwa nusu uchi wakionesha uzuri na haiba zao kwa maslahi ya wengine. Kama si utumwa ni nini?

Ukitazama hayo makampuni yanayo dhamini hayana zaidi ila ni kuhakikisha wanatangaza biashara zao kupitia watoto zetu wakike, wakipita kuonyesha maungo yao na jinsi walivyoumbika. Jee, kama huu si utumwa ni nini?

Tunaiga mambo ambayo si mila wala desturi za Kitanzania wala za Kikristo wala za Kiislam ni za kishetani. Hao watoto maskini ya mungu utakuta wana support yote kutoka kwa wazee wao. Jee, ni tamaa ya maisha, ulimbukeni au ni ujuha? unaowapelekea wazee wa hawa watoto kuona kuwa wanafanya cha maana wanapofikia kuwauza watoto zao kwa njia hii?

Halafu wengine utaona wakishindwa hujiliza kwa uchungu wa kukosa. Na wanaoshinda utaona eti wanajiliza kwa furaha! Ni nini wanacholilia? kukosa fedha za ushindi au furaha ya kuwa sasa watakwenda kuanikwa zaidi?

Halafu kinachokera zaidi ni pale vyombo vya habari vinapowafanya hawa kuwa ni mabalozi wa mambo mema na kuwapeleka sehemu za kulelea watoto wadogo ili wawe mfano bora na waige dada zao wanafanya nini.

Hii ni laana na ushetani na siungi mkono hata kidogo. Ndio hayo, leo mwanao anapita nusu uchi anajianika wewe mzee wake unashangilia. Khaaa.

ukisema TANZANIA unawajumuisha na wazanzibar!.... ZNZ haina mashindano ya u miss.... ni sisi watanganyika na akili zetu za kuiga mambo ya kipumbavu ... na kuacha mambo mazuri...
Zanzibar ikijitenga itabidi nibadili uraia... tanganyika sio nchi ya kukuza mtoto akue na maadali mazuri..

jebs2002,

Ama kwa hakika hii ni moja katika mada nzuri sana nilizopata kuziona humu JF, nakupa pongezi kwa hilo.

Watoto wa kike wa Kitanzania, Waislaam kwa Wakristo, walio na dini na wasio na dini. Wanatembezwa nusu uchi wakionesha uzuri na haiba zao kwa maslahi ya wengine. Kama si utumwa ni nini?

Ukitazama hayo makampuni yanayo dhamini hayana zaidi ila ni kuhakikisha wanatangaza biashara zao kupitia watoto zetu wakike, wakipita kuonyesha maungo yao na jinsi walivyoumbika. Jee, kama huu si utumwa ni nini?

Tunaiga mambo ambayo si mila wala desturi za Kitanzania wala za Kikristo wala za Kiislam ni za kishetani. Hao watoto maskini ya mungu utakuta wana support yote kutoka kwa wazee wao. Jee, ni tamaa ya maisha, ulimbukeni au ni ujuha? unaowapelekea wazee wa hawa watoto kuona kuwa wanafanya cha maana wanapofikia kuwauza watoto zao kwa njia hii?

Halafu wengine utaona wakishindwa hujiliza kwa uchungu wa kukosa. Na wanaoshinda utaona eti wanajiliza kwa furaha! Ni nini wanacholilia? kukosa fedha za ushindi au furaha ya kuwa sasa watakwenda kuanikwa zaidi?

Halafu kinachokera zaidi ni pale vyombo vya habari vinapowafanya hawa kuwa ni mabalozi wa mambo mema na kuwapeleka sehemu za kulelea watoto wadogo ili wawe mfano bora na waige dada zao wanafanya nini.

Hii ni laana na ushetani na siungi mkono hata kidogo. Ndio hayo, leo mwanao anapita nusu uchi anajianika wewe mzee wake unashangilia. Khaaa.

You'll do us a favor...why not doing it now?
Dude .. who are u ..?! btw Tanga yetu pia ilikuwa part ya sultan wa zanzibar wakijitenga tutahitaji tujiunge kule pamoja na mombasa ambao wameanza mchakato ... watu wa bara tuwachie na ustaarabu wenu ... pombe.. uzinzi.. kutembea uchi ..

FF usilie sana. Hii ni sehemu ya ajira milioni kadhaa ambazo mkuu aliahidi kuzitengeneza kila mwaka. Hongera Luteni Kanali Dokta Alhaji JK ongeza mashindano mengine zaidi kupromoti ajira
According to past JF threads nimeshindwa kuiweka hapa...Gazeti la dailynews la tr 11 June liliripoti TZ imeridhia kupeleka wasichana 40 kwenye Reed dance...
TAMWA walikemea, september ndio mwezi wa Reed dance ama ni lini na sie tuembrace tradition hiyo??? Ya mabinti vigoli kucheza nusu uchi kufurahisha wanaume, si heri hata umiss!!...

Hakuna heri mama, "mtoto umleavyo ndivyo akuavyo" na "ukitaka kumkunja samaki awe mbichi, ukimwacha akavunda atakupatisha taabu".

Hayo ya kuwapeleka mabinti huko ni mwanzo tunae binti wa Kitanzania kajianika huko Play boy, uchi wa mnyama na tunamuona yule ni star.

Kwa mwenendo huu, sasa hivi tutaona mapicha ya ngono za Kitanzania yakiuzwa wazi wazi na kupewa baraka na wizara ya utamaduni na kwenda kuzinduliwa na huyo aliyeridhia kuwapeleka mabinti wetu wakaanikwe nusu uchi. Ndio tuna promote biashara za kuuza binaadam, halafu tunajidai hakuna utumwa!