MASHINDANO YA SHORT FILM - AIRTEL NI JIPU

Wakwetu03

Senior Member
Sep 15, 2010
190
81
Nimeitoa sehemu

Haya Ndio Majibu ya Airtel Tanzania kuwa washindi walishinda Kutokana na Kura za wananchi, Hapa ndipo figisu zinapoanza kuonekana kwani washindi walioshinda hakuna hata mmoja mwenye kura nyingi kwani
1. mmoja anakura 4 na mwingine anakura 200 ikiwa kuna watu wenye kura 800 je hao nao tusemeje
2. Na kama mlikuwa hamheshimu wapiga kura na washiriki waliokesha usiku na mchana kuomba kura kwa mwezi mzima wa shindano, naikiwa mlikuwa na watu wenu ambao hata filamu zao zisingepigiwa kura zingeshinda basi kusingekuwa na sababu za kutangaza watu waombe kura na kusumbua watanzania

3.Mshindi aliyepewa Tuzo filamu yake imecoppy aidia ya mtu wa nchi nyingine, kumpa ushindi ni sawa na kututusi, Maana kwenye Festival au Awards nyingine filamu inapogundulika kuwa Aidia si yake Huenguliwa kwenye mchuano na Kunyang'anywa Ushindi..Je nyinyi mmefanya nini juu ya hilo?

Ushahidi wa Filamu iliyoshinda na iliyocopiwa aidia ni huo hapo kwenye link
ILIYOPEWA USHINDI:

ILIYOCOPIWA(ORIGINAL):

4. Ikiwa Washindi wanakwenda kuiwakilisha nchi kwenye Mashindano ya Kimataifa ya BANGKOK na Filamu iliyoshinda imecopy idia toka kwenye filamu za thailand (Bangkok), Mnategemea nini?kama si Kufunguliwa mashtaka ya Hakimiliki, au mnategemea wataisifia kwa kucopy aidia zao?

Ina maana Watanzania Tumeishiwa Aidia kweli?, Au ndio matusi ya reja reja
Nashindwa Kuelewa tatizo lipo wa Waandaaji wa Tuzo hizi Airtel Tanzania au Majaji wa Short Filamu Raqey Allaraqya na Hanscana dE Lavenche,
Maana kutokana na majibu yao kupitia email kwenye picha namba 1 kunaonekana kuna uchakachuzi wa wazi..

Kwa kutumia email iliyojibu maswali yetu inaonyesha wazi kuwa washindi waliopewa taji ni batili,

Sijui kwa anaefahamu sheria au utaratibu wa Tuzo kuwa nini hapa kinafanyika?
 
Back
Top Bottom