Mashindano ya kunywa gongo yaondoka na mshindi

Mashindano ya kunywa gongo yaondoka na mshindi

Wamenikumbusha mbali sana nilipiga mizinga mikubwa sita ya konyagi na safar lager sita sikuamka siku tatu duuuuuuh kweli pombe hainaga ushemeji
 
Huko Mtwara jamaa mmoja ajulikanaye kama Abdlah Chande amefariki dunia baada ya kuibuka mshindi wa kunywa mizinga minne ya gongo
Kijijini Likolombe mashindano haya yapo kila wakati...

Kipindi hiki washiriki walikuwa wanne ambapo kipenga cha kwanza washiriki wote waliweza kumaliza mizinga ya kwanza
Kipenga cha pili mshindi wa pili alichemsha

Kipenga cha tatu wakabaki wawili na kipenga cha mwisho Marehemu Chande ndio akaibuka mshindi kwa kumaliza mizinga yote mine lakini hakuweza kupokea zawadi yake ya Tsh 2000/= kwakuwa alianguka na kufariki dunia huku mshindi wa pili akiwa hoi
Post kama hii utaikuta JF pekeee
 
Samahani mshana, nmekuwa mtu Wa kufatilia Uzi zako toka Mda mrefu sana ila kwa Leo Nina swali 1 , Hivi hiyo avatar uliyoiweka ni wewe mwenyewe maana nmekaa nikatafakari juu ya kuweka hiyo picha nikabaki na majibu yangu tu moyoni , ebu niambie ni wewe au ni mwingine na kama ni mwingine basi nahisi atakuwa special sana kwako,,
 
Jamaa inabidi azikwe na kombe pamoja na medali yake. Fisi kafia kwenye mzoga!
 
Ni elfu mbili kamili 2000/=
Unajua watu wanaoishi Dar wengi hawajui maisha ya sehemu za vijjini hususani kusini huko. Huko sh 2,000 ni fedha nyingi sana. Kuna jamaa alikwenda kwenye msiba maeneo hayo akasema wao pombe kuu ni gongo. Akasema aliwanunulia vijana fulani debe moja la pombe ya gongo wakamuona ni mfadhili wa nguvu sana. Kama nakumbuka vizuri alisema bei ilikuwa 1500.
 
Audio inanishinda kuleta hapa bingwa wa kupiga mbeta kata ya Mwena Jina Maligumu
Alikuwa anajigamba hana koo la nyama nyama yeye analo la plask
 
Duh stelingi kauwawa. Ila kafa kishujaa. Hiyo buku 2 inabidi wapewe ndugu zake kwa marehemu ni mshindi halali
 
Wangempa mshindi wapili hiyo elfu 2 akajiuguze inanikumbusha mwaka 2000 mtaani kwetu kulikuwa na mashindano ya kunya maziwa ya moto kwa dk tano mshindi alikuwa anapewa elfu 10 jamaa alishinda lakini hela yote iliisha kwa ajili ya kujiuguza anadai alikuwa anaona tumboni kama kuna tanuli la moto na ulimi umebanikwa kwenye moto mpaka mwisho wa siku alitumia elfu 30 kujiuguza ilihali yeye alishinda elfu 20
Denis nipe story vizuri namna inavokuwa kunya maziwa ya moto!!!!!
 
Back
Top Bottom