Masharti ya kumiliki bunduki vs masharti ya kumiliki leseni ya kuendesha gari la abiria

illegal migrant

JF-Expert Member
Oct 18, 2013
1,277
1,121
Ni jambo ambalo kwa muda limekuwa likinishangaza masharti ya kumiliki silaha ya moto ni kama hayawezekani kwani ukiambiwa ile milolongo uanzie kwa mjumbe, serikali ya mtaa, kata, wilaya, taifa kwa DCI nk inaweza kukuchukua miaka na usipate.

Kitu kinachonishangaza ni watanzania wanaouawa au kujeruhiwa na silaha za moto zilizosajiliwa hawafiki hata kumi tena pengine huwa ni katoka hali ya kujilinda, ila watanzania wanaokufa kwa ajali za barabarani ni maelfu kwa maelfu ambapo leseni yake kupata ni rahisi tu kwani haiangalii historia ya muhusika background check kwa mtazamo wangu ninashauri leseni za kuendeshea magari hususani ya abiria ziwe na masharti magumu pengine yafanane na hayo ya kumiliki silaha za moto
 
Barabara wanazotumia magari ya abiria ni tofauti na binafsi?....mfano gari binafsi likiparamia la abiria hawafi....
Suala la usalama barabarani linahusisha kada mbalimbali, madereva wa abiria, binafsi, pkpk, bajaji, baiskeli, mikokoten, wachunga mifugo, watembea kwa miguuu, wajenz nk
 
tochi ikimnasa amezidi 80km/hr na ni dereva wa abiria anapewa adhabu bila kuangalia sura, wengi wanapelekwa mahakamani na hukumu ziko fasta kuliko maelezo wengi wako gerezani.
 
Back
Top Bottom