Masharti ya kujiunga na chama cha mapinduzi (CCM)

Ni muda mrefu sasa nimekuwa nikifuatilia mwenendo wa kisiasa wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) na kujikuta navutiwa nacho.
..nina imani nitaweza kulijenga taifa langu kwa umakini zaidi nikiwa kama mwanachama wa CCM .
..kama kuna kiongozi yeyote wa CCM naomba anisaidie namna ya kujiunga na chama na kupata kadi ya uanachama.
Cc Simiyu Yetu FaizaFoxy MSALANI na wanaCCM wote.
Aisee............:juggle:
 
Ni muda mrefu sasa nimekuwa nikifuatilia mwenendo wa kisiasa wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) na kujikuta navutiwa nacho.
..nina imani nitaweza kulijenga taifa langu kwa umakini zaidi nikiwa kama mwanachama wa CCM .
..kama kuna kiongozi yeyote wa CCM naomba anisaidie namna ya kujiunga na chama na kupata kadi ya uanachama.
Cc Simiyu Yetu FaizaFoxy MSALANI na wanaCCM wote.

Karibu tujenge nchi yetu mkuu! Kujiunga na chama, nenda ofisi yeyote ya CCM iliyo karibu nawe.
 
ha ha ha Jawilat . ni haki yako na inalindwa na katiba. Fka salama.
 
Last edited by a moderator:
Ukiona hiyo dalili ya kutamani kujiunga na makundi ya watu wanaotumia mamlaka yao kukandamiza kundi la watu maskini huku likiwaimbia wimbo mzuri,basi jua kabisa kuwa umeanza kupata ugonjwa wa akili.Na unaweza kujichunguza kidogo tu kabla ya kwenda hospitali.Mfano kama unafurahia kuona simba akimkimbiza swala na kumtafuna ama unafurahia kuona mamba anavyokamata nyumbu anayevuka mto,ama unaishi katika nyumba nzuri lakini unafurahia kuona majirani wakihangaika wakati wa mvua kwa kuogopa mafuriko,ama unafurahia sana na kujiona mjanja unapokuwa kwenye gari na ukakanyaga vidimbwi vya maji ili watembea kwa mguu wanaokukera kwa kuwa barabara unayopita wachafuke kwa maji hayo yaliyochanganyika na tope,ama hujawahi kwenda kabisa kwenda kuona wagonjwa hospitali za serikali,ama hujui kabisa hata magereza ilipo na unaona wafungwa wote ni haki yao tu kuwa huko kwa vile walistahili.Kama una roho ya namna hiyo unahaki ya kutamani kujiunga ccm.Kama hayo niliyoyasema hapo juu ikawa kweli japo hupendi,nenda kamuone daktari wa magonjwa ya akili na saikolojia huenda utapata msaada

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Oooh nadhani hapa nitapata mwongozo sahihi zaidi,huku nilipo sijawahi kuona ofisi za CCM.

oh wow yeah nadhani uko NJE ya NCHI... Hapo kweli itabidi wakufuate huko uliko na Inawezekana... Makada Mbalimbali wanatembelea WanaNchi Nje ya NCHI kwa FEDHA za NCHI...
 
Karibu sana kwenye chama kilichothubutu, kikaweza na sasa kinajenga nchi kupitia ilani yake ya uchaguzi 2010.

CCM hatufanyi mambo ya kisiasa theoretically bali tunafanya practically.

Tembelea kwenye shina lolote la wakereketwa, Balozi wa nyumba kumi au ofisi ya CCM tawi/kijiji na huko watakupa maelezo ya taratibu za kuwa mwanachama.
"There you are mr. MwanaDiwani", kweli mambo yenu huwa ni "practical"
1. Shule za kata kukosa walimu, madawati, maabara, vitabu n.k.
2. Hospital, Vituo vya Afya na Zahanati kukosa wataalamu(Matabibu), Vifaa na madawa
3. Wakulima kukosa pembejeo za kilimo na masoko ya bidhaa za kilimo
4. Rushwa na Ufisadi uliobobea kwenye sekta zote
5. Uongozi unaopatikana kwa mitandao na sio uwezo wa wahusika
Kwa hayo yote CCM mpo "very much practical" hakuna chama duniani kitakachofikia rekodi yenu!
 
Aisee ingekua lazima raia uwe mwanachama wa chama flani hata mimi ningeingiaga CCM.

Hawa jamaa wanaotoana manundu kisa uwenyekiti nilikua nawakubali sana ila sasa hivi nishawaona wale wale njaa kali.

Labda siku waruhusu wagombea binafsi but until then hutaniona TENA kwenye foleni kwenda kumpigia ----- flani kura nimtoe kitambi (GOD FORBID).

Mwendo wa kuadapt na uongozi wowote sio kumtegemea eti Lowasa au Slaa akultee maisha mazuri. WOTE NJAA.
 
CCM ni chama cha wananchi , ulikua nasi toka mwanzo tunapongeza tu kujitambua kwako kuwa wewe ni mwanachama wa CCM hongera kwa kujitambua karibu nyumbani.
 
Unatamani niwaze uwazacho wewe?nipende upendacho wewe?nifanye ufanyacho wewe?
Nipo kwenye nchi ya kidemocrasia yenye mfumo wa vyama vingi,nina uhuru wa chama gani nisimame nacho.
....watanzania tuna matatizo some where....nchi unaona inaenda vzr eehee...! brain is there for brainstoming
 
Nenda ila utacheza mziki kutokana na mapigo yake ukienda kubadilisha mifumo yao ya ulaji wanakuua tu. Kama wengine wanavyofia SA.
 
Kama nilivyosema,nataka kujiunga na CCM, mimi nina elimu ya shahada na cheti cha taaluma. Sasa kabla sijajiunga naomba wana CCM mniambie
1. Je kuna faida gani ya kua mwanachama wa CCM.
2. Kadi naipata wapi ya uanachama.

Naomba mtu asijaribu kuhoji uamuzi wangu, Tuheshimiane.

UPDATES

Toka juzi nilipoomba ushauri humu kuhusu nia yangu ya kujiunga CCM, wadau mmetoa michango yenu mingi na ushauri wenu. Elly B na wengine wote mlionishauri kutokujiunga na ccm nimepokea ushauri wenu mzuri, nimetafakari na kuamua kuachana na nia hiyo ovu iliyokua inanisukuma. Asanteni sana. Mungu awabariki wote.

Ushauri: Elly B elimu hiyo muwe mnaitoa hata huko kwa wananchi wengine isiwe humu jf tu. Waelimisheni ndugu na jamaa zetu ambao hawako humu,sambazeni elimu hiyo kwa wananchi.
 
Last edited by a moderator:
faida ni kwamba utakuwa mnafiki na muongo.pia mwizi na muuaji.halafu mtekaji na mtesaji.kujiunga mtafute boko haram..leo atakuwa dar
 
Back
Top Bottom