Masharobaro wengi huwa hawana hela

okoyoko

JF-Expert Member
Jun 15, 2014
2,664
3,639
Kwa uchunguzi wangu mdogo nliofanya, nimegundua kuwa wakaka wengi wanaovaa kisharobaro, eg juu kidugu plus waves, cheni za gold shingoni jeans, na supra au airforce mguuni huwa ni nadhifu kwa nje tu ila wengi wao mifuko yao ni mitupu, unakuta mtu kavaa kisharobaro lkn mfukoni hana hata 500 ya vocha, masharo wenye hela wapo ila ni wachache saana

Hivyo wadada msidanganyike kuona mwanaume kavaa kisharobaro mkadhani ana hela..
 
Raha ya kuwa na mwanaume awe mgumu kama Johmakini au fidq raha sana, mwenyewe unajiona uko na mwanaume kamili hata asiwe na hela.

Sio hivyo vitoto vya mama mbwembwe nyingi afu vinakuwaga laini.
 
yaani hapo umekosea, ulitakiwa useme masharo wengi huwaga ni mapusha..suala la hela yeyote anaweza kupungukiwa
 
Raha ya kuwa na mwanaume awe mgumu kama Johmakini au fidq raha sana, mwenyewe unajiona uko na mwanaume kamili hata asiwe na hela.

Sio hivyo vitoto vya mama mbwembwe nyingi afu vinakuwaga laini.
Wale sio wagumu mbona? Kumbe wagumu huwajui
 
Havina pesa vinaishi kiujanjaujanja demu anachuna huku anakapelekea pesa kwa hiyo usishangae kupanga ni kuchagua na mwisho wa usharobaro nia majukumu
 
Raha ya kuwa na mwanaume awe mgumu kama Johmakini au fidq raha sana, mwenyewe unajiona uko na mwanaume kamili hata asiwe na hela.

Sio hivyo vitoto vya mama mbwembwe nyingi afu vinakuwaga laini.
ha ha safi sana dada mwanaume mgumu ndo mchakalikaji
 
Ingekuwa hivyo dada zenu huko vijijini wasingekuwa wanatiwa hovyo mimba na hivi visharobaro vikienda kusalimia.
Angelita ni kijiji gani dunia ya leo utaenda kusalimia kwa mfano then watu wakakushobokea?Mfano kijijini kwetu maendeleo yapo kila kitu unapata kuanzia mawasiliano,umeme na vitu vya gharama kama smartphone za bei juu hata aliyepo hapa dar uwezo wa kununua hana.
 
Wale sio wagumu mbona? Kumbe wagumu huwajui
Raha ya kuwa na mwanaume awe mgumu kama Johmakini au fidq raha sana, mwenyewe unajiona uko na mwanaume kamili hata asiwe na hela.

Sio hivyo vitoto vya mama mbwembwe nyingi afu vinakuwaga laini.
hao unaosema wagumu pengine kupanda mlima kilimanjaro wanaishia kituo cha kwanza.
 
ndo yahya wa ladyjaydee hata kazini wanafanya kisharo pia! hataki viti vyakuumiza kichwa kama kujwnga, kulipa kosi, kusimamia biashara yaani
 
Hivi wale watu huwa wana nini, maana wadada wanawazimia mbaya mbovu, wengine hadi kupigana kabisa Sharo mwenyewe hana hata baiskeli daaah, wale hawanaga muda wa kutafuta hela, wako busy kujiremba tuu mapafyumu ndo usiseme akipita pembeni yako utafikiri gari ya pafyumu imepata ajali. Daaah
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom