OLESAIDIMU
JF-Expert Member
- Dec 2, 2011
- 19,139
- 9,575
kwa kweli mimi ni mwanachadema damu lakini kuna mahali hata nyie wachangiaji wenzangu tuwe tunaongea ukweli,KUHUSU KUTUMIA MAGARI YA KIFAHARI VIONGOZI CHADEMA HIYO TABIA WANAYO,kwa wale wanaofuatilia siasa za ndani kumbukeni siku ujumbe wa chadema ulioenda ikulu kuwasiliana na rais,haraka haraka niliona vx kali sio tu vx ili ina ubora wa kipekee wa wale viongozi,VX aliyokuwa kapanda mbowe sio ya kitoto hata mil 80 sidhani kama utaweza kuipata ,pili wabunge wengi wa chadema wana magari ya kifahari ingawa kuna wachache sana wanayakawaida,ANGALIA GARI YA REGIA MTEMA ALIYOPATANAYO AJALI,mtoto ana miezi kadhaa bungeni anatembelea vx tena viti maalum ,wakati baba yake hapo tabata tunamjua,KWELI KWA HILI VIONGOZI WA CHADEMA BADILIKIE TUMIENI RAV 4 NI GARI NZURI ,NGUMU,INAENDA BARABARA ZOTE MIL 20 TU INATOSHA BADALA LA HAYO YA MIL 80
Kigarama...
Naomba nitumie maneno haya kukufumbua macho. Unapoishi jirani kuna mtu ana VX na mwingine ana Suzuki Nomade. Mwenye VX akilala na njaa akaenda kumwomba mwenye Suzuki chakula kesho yake, nadhani mwenye Suzuki atamwambia mwenye VX kuuza gari lake la gharama kubwa na fedha atakayopata atanunua Suzuki (ili aweze kusafiri) na inayobaki atanunua chakula na nyingine atafanya mtaji wa biashara...hakika hata patwa na njaa tena.
Sasa Kigarama...
CCM ikiambiwa masuala ya msingi kama afya na elimu inasema hakuna fedha nchi yetu bado maskini. hakika lazima tuende nje kuhemea ili tuweze kupata chochote cha kula. kama haya ni ya kweli, basi tumia mfano wangu wa awali wa hao watu wawili yaani mwenye VX na mwenye Suzuki.
kwa hiyo Kigarama...
CDM ina maisha yake, ili kusaidia Taifa hili Tajiri linaloitwa maskini na magamba ilikuja na mpango mzima wa kuwakwamua watanzania...waunge mkono!
CHADEMA ilitoa hoja za msingi sana wakati wa Kampeni za Mwaka 2010 na zikakubalika na wananchi wa Tanzania.
Mgombea Urais wakati huo MH: Willbroad Peter Slaa na wagombea wa nafasi za Udiwani na Ubunge walikuwa wanatoa tuhuma kwamba serikali iliyopo madarakani inafuja fedha za wananchi kwa kununua magari ya kifahari aina ya Land Cruiser VX na V8 wakati fedha hizo zingetumika vizuri zingeleta maendeleo kwa wananchi. Katika kukoleza hoja hiyo ikaaminishwa kwamba kama CHADEMA ikishika madaraka basi magari hayo ya kifahari yatauzwa na madala yake yatanunuliwa magari madogo ya bei rahisi.
Slaa alikuwa anasema aina ya magari yanayotumiwa na Wakuu wa Wilaya na Mikoa thamani yake ni sawa sawa na gari moja kujenga Zahanati Nne vijijini. Wanachi waliambiwa kwamba magari hayo yatauzwa na fedha itakayopatikana itatumika kuwekeza kwenye Elimu.
Baada ya uchaguzi wa Mwaka 2010 viongozi wa CHADEMA hawatumii VX au V8 kwa matumizi ya kichama na yao binafsi, au thamani ya magari hayo imeshuka baada ya wao kuanza kuyatumia?
UKIKEREKA SEMA UPENDAVYO!!
Ni kwa mujibu wa sheria......suala la usahihi ni subjective mno
Nazungumzia "consistency" ya chama kwenye mambo wanayoyapigania wakati wa Kampeni. Kusema akili yangu mbovu hakuondoi ukweli kwamba hata hayo mashangingi ya CHADEMA yananunuliwa na kwa kodi za wananchi. Wewe hujui kuna baadhi ya wabunge kabla ya kuwa wabunge hata Baiskeli walikuwa hawana uwezo wa kununua.
Unajisahaulisha kwamba wabunge wote walipewa mkopo wa shilingi Milioni 90 na ofisi ya Bunge kwa ajili ya kununulia magari yao?
CDM walichokuwa wanalalamikia ni suala la Serikali kuwa na magari ya kifahari ambayo ni ya bei kubwa na yana high fuel consumption.. Na vle vle yana gharama kubwa kwenye kuyamaintain.. Hiyvo unakuwa ni mzigo mkubwa na wa gharama kwa serikali..! Sasa mtoa uzi unaposema CDM wanayatumia magari ya aina hiyo unapaswa kutuweka wazi.. yanalipiwa na Serikali..? Kama ni mkopo ni haki yao wabunge wote kama ilivyoainishwa katika privileges za wabunge.. Na ukumbuke hata katika taasisi na mashirika mengine yana utaratibu wa kutoa mikopo ya magari kwa wafanyakazi wao ili kuwaharasishia kwenye usafiri wafanyakazi ili kuleta ufanisi.. Na mbunge ana choice ya gari gani anunue.. Mh. Mnyika yeye aliamua kununua Toyota Vitz na pick up.. Kama mwingine alinunua vx ni haki yake.. Kiwango kinachotolewa na serikali cha mafuta kwa magari ya wabunge ni kile kile uwe na Vitz au vx.. Services ya magari yao wanalipa wenyewe wabunge..
Nadhani hoja inajibiwa kwa hoja mimi siamini kama maneno yaliotumika hapo juu kwenye mjadala wa hoja kama kiazi,akili mbovu,mjinga,mvivu wa kufikiri,mfuasi wa kibwetere yana nafasi,cha msingi tujifunze kuvumiliana na kujibu hoja za msingi kwa hoja na wala si jaziba maana tunaamini watu wenye access ya JF walio wengi ni wasomi na wenye uelewa wa mambo.
You may agree to disagree but kwa hoja ili kwa mtu ambaye si mwanasiasa au muumini wa chama chochote apate mwelekeo
kwamantiki hiyo waeza kubaliana nami kuwa kama sheria inasema hivyo basi haiko sawa ni matumizi mabaya ya kodi za watz hivyo tunahitaji sheria hii ibadilishwe au sivyo?
Kigarama...
Naomba nitumie maneno haya kukufumbua macho. Unapoishi jirani kuna mtu ana VX na mwingine ana Suzuki Nomade. Mwenye VX akilala na njaa akaenda kumwomba mwenye Suzuki chakula kesho yake, nadhani mwenye Suzuki atamwambia mwenye VX kuuza gari lake la gharama kubwa na fedha atakayopata atanunua Suzuki (ili aweze kusafiri) na inayobaki atanunua chakula na nyingine atafanya mtaji wa biashara...hakika hata patwa na njaa tena.
Sasa Kigarama...
CCM ikiambiwa masuala ya msingi kama afya na elimu inasema hakuna fedha nchi yetu bado maskini. hakika lazima tuende nje kuhemea ili tuweze kupata chochote cha kula. kama haya ni ya kweli, basi tumia mfano wangu wa awali wa hao watu wawili yaani mwenye VX na mwenye Suzuki.
kwa hiyo Kigarama...
CDM ina maisha yake, ili kusaidia Taifa hili Tajiri linaloitwa maskini na magamba ilikuja na mpango mzima wa kuwakwamua watanzania...waunge mkono!
Akili yako mbovu,chadema iliadress yale yanayonunuliwa kwa kodi za watz.kuelewa kugumu sana ndgu yangu...kiazi
Mkuu kama Chadema ina maisha yake na ina jitosheleza kwa nini inaendelea kupokea ruzuku inayo toka serikalini na ambayo ni kodi ya wananchi? Jamani watu hamjui swala la ruzuku?
Na wewe endelea hapa ili twende sawa; Basi baadaye mwenye suzuki biashara yake ikawa nzuri na maisha yakamnyookea watoto wake wakawa vijana na wakapata mikopo kwa kutumia influence ya baba yao na kuanza kuishi maisha ya ghali kama jirani yao aliyeuza VX lakini kila mzee wao alipoaswa juu ya vijana wake yeye alijibu ni mikopo yao wenyewe waache wafanye watakavyo bila kukumbuka ya kuwa mikopo ile ali influnce yeye mkuu wa kaya na huko nyuma aliwahi kumshauri jirani yake auze VX.....
My take;Kama mzee angekuwa na busara angewaonya vijana hawa kwa kuwapa mifano ya jirani aliyeuza VX badala ya kusema ni mikopo yao wenyewe.......
Kinachogombewa hapa si mtu bali ni mfumo...
Angalia Rwanda...
Angalia wakati wa Nyerere...
Angalia na wakati wa Mwinyi, viongozi walipotoka Zanzibar...
Kwa hiyo ....ni.... MFUMO!!! ...........ndo tatizo letu kuu.............
Hebu tuache ushabiki katika kila jambo. Mimi binafsi naona mtoa hoja anayo hoja. Kama ni kweli kwamba Chadema wamenunua mashangingi ama kwa matumizi ya chama ama kwa matumizi binafsi basi wamekosea, hawajamaanisha waliyoyatamka kwa vitendo, si mfano mzuri katika hili. Chadema wanapaswa kuonesha mfano kwa maneno na vitendo, hiyo ndio namna pekee ya kujitofautisha na CCM na kufundisha kwa vitendo. Natoa wito kwa viongozi wa Chadema kuliangalia hili jambo kwa umakini maana ni mambo madogomadogo ya namna hii ndio yanaondoa taratibu imani yao kwa chama. Nawasilisha.
Very low mentality this is.........