Kuna wakati wana jf mna point lakini jinsi mnavyoandika inakera kweli. Nitatoa mfano, nilisoma katika shule moja ya kanisa. Katika shule hiyo, kama ulibainika kutoroka wakati wa usiku basi wewe hapakuwa na njia nyingine isipokuwa kufukuzwa. Siku moja, mimi na rafiki yangu tulisingiziwa na mlinzi kwamba tulikuwa tumetoroka, lakini kumbe tulikuwa tumetumwa na mlezi mmojawapo wa shule. Usiku ilipigwa kengele na wanafunzi wote walikusanyika na sisi hatukuwepo. Kesho asubuhi tulitafutwa mapema sana na tulianza kuulizwa kwa nini hatukuwepo shuleni wakati wa kuitisha majina. Kwa vile rafiki yangu alikuwa na kisa na mlinzi alifikiri kwamba huu ndiyo ulikuwa mda mwafaka wa kuchamba mlinzi. Hivyo malinzi aliposema hawa walitoroka mlezi, rafiki yangu alisema wazi wazi, "Wewe mzee ni mwongo sana wewe! Sisi hatujatoroka. Na unatabia ya kutufuatilia sana!" Mimi nilimwambia usiseme hivyo. Mlezi alinipa nafasi nijieleze na nilisema hivi, "Nashukuru sana mlezi, kwa kweli nikisema kwamba huyu mzee anachosema ni uongo nitakuwa namkosea adabu, lakini kweli anachosema si kweli kwani sisi tulitumwa na mlezi fulani." Kweli rafiki yangu alisimamishwa masomo kwa mda wa wiki mbili, hii ni kutokana na matumizi ya lugha mbaya.
Jambo la msingi hapa ambalo mleta mada ameleta ni: Je kweli viongozi wa CDM wanatumia magari haya ambayo walipiga kelele kwamba yanatumia mafuta mengi, gharama yake ya kununua ni kubwa na mambo kadha wa kadha? Kimsingi kama wanatumia magari haya naona hii si haki na ni kukosa msimamo. Je wakati wanasema hayo hawakuwa wamefanya research ya kutosha, kwamba magari gani yanaweza kutumika badala ya haya? Au ndiyo ule msemo usema, "Nyani hucheka **** la mwinzie, kumbe lake ni jekundu zaidi," Tunapoweka sera, lazima tuwe na dhamira za kweli, tunapotoa msimamo wetu lazima tuusimamie, na si kutoa matamko bila utafiti wa kutosha. Kama utafiti haujafanyika hakuna haki ya kuongea.
Mtoa mada jifunze jinsi ya kufanya utafiti. Pia wana jf jifunzeni kujibu hoja si matusi, hayasaidii. Hawa CDM tusipowajadili leo kesho wanaingia madarakani, tutaendelea hivyo na mwisho wake ni kuvuna mabua.