Mashambulizi kuelekea 2015

Mashambulizi kuelekea 2015

sifongo

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2011
Posts
4,895
Reaction score
5,308
Habari wanajamvi na natumaini mwaka umeanza vyema.

Nimekuwa nasoma makala za wanajamvi humu JF kusema kweli nafarijika kuwa wengi tunachukia jinsi Nchi yetu inavyoyumbishwa na walioko madarakani kwa sasa (CCM) hali hii imenifanya najiuliza maswali mengi hasa matumizi ya kodi ninayolimwa huko kwenye kibarua changu na hii ninayokutana nayo kila mke wangu aendapo kununua sukari, chumvi na kiberiti duka la jirani, je kodi yangu inafanya kazi iliyokusudiwa hasa? hapa nina maana huduma bora za afya, miundo mbinu ya kueleweka, huduma bora za kijamii na mengine mengi ambayo hata wewe mlipa kodi utafurahi kuona jinsi jasho lako linavyotumika na sio kwenda kutibia viongozi wetu mafua, macho na kuchekiwa afya zao huko India.

Kumekuwa na vifo vingi sana vya kina mama wakati wajifunguapo, vifo vya watoto vitokanavyo na malaria na vifo vingi katika jamii yetu vitokanavyo na magonjwa yanayotibika na vifo hivi vinatokea tu kwasababu huduma za afya kwa jamii sio nzuri, madawa hakuna, vipimo vya uhakika hakuna, ma-dr hawafanyi kazi kwa moyo kwani kipato hakiridhishi, hapa ndio najiuliza kodi yangu inafanya kazi gani, utalii,gesi,madini, uvuvi, rasilimali zote za Nchi hii na huo uchumi unaopaa mbona hatuoni faida yake?

Mimi nashauri kwa yoyote mpenda mabadiliko na ustawi wa Nchi hii uwe mwanachama wa CDM usiwe mwanachama wa CDM kwa nafasi uliyo nayo popote pale piga kampeni ya kuiondoa CCM madarakani 2015, muelimishe bibi yako, muelimishe babu yako, muelimishe baba na mama yako na yoyote yule aliye mbele yako, muambie hii Nchi ni yetu sote na sio mali ya viongozi mafisadi wa CCM na familia zao, rasilimali za Nchi hii ni zetu sote Watanzania.

MUNGU IBARIKI TANZANIA KUELEKEA 2015 KUWATOA KUPE KATIKA NGOZI YA MTANZANIA.
 
Mkuu Sifongo tatizo linalotukabili watanzania ni tabia yetu ya kulalamika na kulialia bil a kutoa maoni/ushauri/mapendekezo kuelekea kuondoa hicho tunacholalamikia. Unasema kuna vifo vingi wakati wa kujifungua na vingine vinasababishwa na malaria, hujatoa maoni yako nini kifanyike kurekebisha hali hiyo badala yake unaingiza siasa. Hivi kweli namna bora ya kukabiliana na malaria ni kuiondoa CCM madarakani. Kweli akili za mbayuwayu changanya na za kwako.
 
Nafikiri Mtwara wameanza,kwani wanatumia demokrasia kulalamikia Serikali yao: "kwa nini mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi isifungwe Mtwara?",majibu yasipopatikana mpaka kufikia 2015,basi watawala wataondolewa kidemokrasia kwa kupitia sanduku la kura katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015.
 
Mkuu Sifongo tatizo linalotukabili watanzania ni tabia yetu ya kulalamika na kulialia bil a kutoa maoni/ushauri/mapendekezo kuelekea kuondoa hicho tunacholalamikia. Unasema kuna vifo vingi wakati wa kujifungua na vingine vinasababishwa na malaria, hujatoa maoni yako nini kifanyike kurekebisha hali hiyo badala yake unaingiza siasa. Hivi kweli namna bora ya kukabiliana na malaria ni kuiondoa CCM madarakani. Kweli akili za mbayuwayu changanya na za kwako.

Ni kweli Mkuu malalamiko yamekuwa mengi maana hata Rais wetu haishi kulalamika naamini hata wewe unalijua hilo, nimejaribu kuchanganya na za kwangu kama ulivyonishauri nimegundua kuwa kuna miradi mingi ya malaria ilianzishwa hapa Nchini mingine ikifadhiliwa na Nchi wahisani lakini usimamizi wake ni mbovu, watu wanajipanga kula zaidi badala ya kufanya jambo husika, ishu kama malaria sioni kwanini mpaka leo ni tatizo TANZANIA, mtaani kwangu wanapita vijana wanasema wametoka SERIKALI ZA MITAA wanakuja kupuliza dawa za kuua mbu, mende na wadudu wengine wanatuchaji 2000 kila nyumba, kichekesho ni kuwa wakishapuliza usiku mbu ni kama wamevutishwa bangi wanauma ni hatari, ukifanya uchunguzi utagundua mchakachuo ulifanyika, kila kitu ni dili.....kwanini tusiilaumu hii SERIKALI ilhali ndio inalea uzembe.
 
Back
Top Bottom