Mashamba yanauzwa

Mkuu hilo la km 78 from Dar ni ekari ngapi? Je na hizo bei ni fixed au negotiable? Niko interested Mkuu. Tupatie na contacts mkuu.

Linakadiriwa kufika eka 25 hivi,bei sio fixed,aliyenijulisha na kunionyesha hilo shamba sio mzee mwenyewe. Liko karibu na shamba langu,ila hilo halifiki barabarani. Faida/uzuri wake lina kina kirefu cha maji ya kijito hicho.

Contact zangu au za mwenye shamba?
 
mie napenda sana kupata shamba kwa muda huu naomba unipe details zaidi ili mwisho wa mwezi nakuja bongo kupiga kura na ikiwezekana nichukue hilo shamba.
nataka hilo linalopakana na mto ila kama bajeti itanishinda basi naangukia hilo jingine yote itabidi niyaangalie, kama bahati ni yangu nadhani nitayakuta.
Nipe details zaidi mkuu

Bei hizo ni za kuanzia sio fixed. Yapo na mengine alongside na hilo. Pili hutakuwa peke yako, ni pamoja na mimi na wenzetu kama watano hivi,vijana watupu. Tumeshaanza kufanya vitu kidogo. Utayakuta.

Shamba hilo,lina mikorosho mingi,linafaa kwa kilimo cha matunda na ufugaji,kilimo cha umwagiliaji hasa mpunga kinawezekana. Panafikika na si muda mrefu patakuwa hot cake.
 
Wakuu, Mimi ninapenda tuonyeshane mbinu za kufanya biashara ya real estate. Nimejifunzia California na ninaona kama sheria za huko zinafanana na za bongo, twaweza kushirikiana kuleta maendeleo kwetu sote.

REAL ESTATES imegawanyika sehemu nyingi kuna: Nyumba za kuishi, maofisi, nyumba au chumba cha kuuzia vitu, godawni, nyumba au ardhi ya viwanda, shamba tupu, shamba lenye kanyumba au lijumba: na kadhalika. TUJIHADHARI NA UDANGANYIFU (UTAPELI). Unarudisha sana maendeleo.

Wakuu, kataka ulimwengu wa biashara kuna makundi manne. ( 1) Kuna wafanya kazi, (2) wajasirimali au wachuuzi (3) wafanya-biashara (4) Wawekezaji. Uliza swali lolote la finance, nikishindwa nitalipeka kwingine. Haya karibuni. yasser.mziba@yahoo.com


Unapouliza swali naomba uandike uko katika kundi gani. Makundi yote ni sawa tu, sababu ni kutaka kujua uwezo wako, kiujumla. Kwani ni mtu yeyote aweza ingia biashara ya real estate.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom