Mashamba yanauzwa

Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
5,149
4,674
Moja lipo km 78 toka Dsm kwenda Mkuranga,lina mikorosho,linapakana na mto usiokauka,usafiri wa daladala toka mbagala upo. Halifai kwa kilimo cha mazao ya nafaka,linafaa kwa matunda na ufugaji wa aina zote. Bei kwa eka laki sita. La pili ni kama km 60 hivi,linafaa kwa kilimo cha mazao yote na ufugaji,lipo kando ya barabara na usafiri wa daladala upo,ukubwa yapata eka 10 hivi na lina kibanda kibovu na lina mazao ya pwani,bei 5M. Hili lina maji ya msimu wa masika tu. Haya mashamba nimeyaona.
 
nimefurahi sana malila kutukumbusha sisi tuliosahau kuwa na viwanja na mashamba, mimi pia nahitaji shamba ila lipo eneo gani hasa, ukitoka dar kwenda mkuranga kuna temeke, mbagala............. mkuranga, je kama liko kando ya barabara ni mbali na road reserve maana kuja kuambiwa ondoka tunapanua barabara inakuwa haipendezi tupetaarifa kamili, tuwasaidie na wengine
 
Kutoka pale Mkuranga wilayani unafuata barabara ya kisiju kwenda Mafia, kabla ya kuvuka mto Mbezi ndipo lilipo hilo shamba la 5M, kuna mita kadhaa za road reserve,anayeuza ni mwalimu wa shule ya msingi,kwa sababu ana hama na kurudi kwao. La pili ambalo ni km 78 toka Dsm lipo njia hiyo hiyo ( ukifika Mbezi unaingia kushoto) ktk kijiji cha Msorwa. Barabara hii inazunguka kuja kutokea kigamboni. Habari za kupanua barabara zipo kila mahali kwa wakati wake, daraja la mto Mbezi likijengwa hakuna haja kupita mkuranga kwenda huko. Unapita mkuranga kwa sababu hakuna daraja kwa sasa,magari yanavuka chini wakati wa kiangazi tu.
 
Mkuu haya mashamba hasa lile la km 78 liko karibu na shamba la AMADORI lililoko karibu na mto au inakuwaje?tupeane mwelekeo zaidi man.
 
Shamba la Amadori liko kijiji cha Shungubweni kitongoji cha Funza,unavuka mto ule unaokupwa na kujaa,ninalosema mimi liko kijiji cha Msorwa kabla ya kuvuka mto Mduzi. Ukitoka Mduzi ndio unaingia Shungubweni na hatimaye Funza.
 
Jamani hapo Kisarawe tu kuna mashamba mazuri kabisa kwa laki moja tu kwa ekari na ni karibu sana kutoka Dar, kama sikosei si zaidi ya km 40.
 
Kweli kabisa mkuu unachosema,lakini hapo kisarawe unaposema kuna maji ya kufanyia kilimo mkuu? kama ni shamba kiwanja sawa. Kama kuna mashamba mbona watu wanakwenda kununua morogoro na wanapita mapori yote humo njiani ( mdaula,mikese nk),wanakwenda Kilindi kulima kwa nini wasilime hapo Vigwaza.

Mkubwa,sasa hivi shamba zuri ni maji,biashara ya kutegemea mvua inatulostisha mkuu.
 
Nimekusoma mkuu
 
Wakuu wakuu wakuu, hebu subirini kwanza. Yani Mnazungumza hela nyingi sana nadhani bora tuzichangie mawazo. Msiwe na wasiwasi Hamna utapeli hapa wakuu. Wenye kuuza wanauza na wenye kununua wananunua. Tutachofaidika nikua tutachangamsha biashara ya mashamba na kufundisha watu haki za mali (Financial Literacy). Lakini kabla ya kufanya kuna maswali itabidi tuyajibu, ili tusiwapatie watu pesa halafu huenda mtu ni mbadhirifu itabidi afundishwe mbinu za ubanizi kidogo (sio ubahili hapana).

Tutaleta customer service bongo. Nimeshawahi kufanya real eastate na kwenye management team yetu tunawatu amba wanaelewa na ni wabongo wenzetu ingawa timu yetu inawatu kutoka nchi tofauti yani tuwaletea expriance from deferent angles.

Ikiwa kuna mtu amevutiwa na kufanya hilo jambo (Ujasirimali wa real estate hata sasa hivi ndio biashara yako tunakuhitaji), naomba unitumie notification with a heading GREEN INVESTMENT, hali , au face book Yasser Mziba. Nitazungumza na ED wa JF, he's cool dude.

We gotta do this guys. Kila mtu atanufaika. tutawapa watu kazi. Mwana JF yoyote anakaribishwa. Itakua ni project kwa hiyo inamaana itakua na mwanzo na mwisho. halafu tunapima matokeo. Wazee wenye mashamba yenu kwanza nawashauri msiuze. nakama mkiuza tafadhali tutumieni mimi na watako jitokeza. Tutaonyesha namna ya kufanya customer services katika finance, alafu mabenki yatakopi model.
 
Wazo zuri Mkuu. Hapajawahi kuwa na wakati mzuri wa kuwekeza kwenye real estate Tanzania kama kipindi hiki. Tafadhali sijaelewa vizuri ni utaratibu gani mlionao wa kujiunga na hii biashara/network yenu. Mimi niko interested.
 
GREEN INVESTMENT
Mziba, nimekupata mimi niko kwenye mchakato kuangalia nitafanyaje ili niingie kwenye real estate nashukuru kwa kuanzisha hili jambo niweke kwenye list nijulishe tutawasilianaje?
 
Malila,Laki 6 kwa heka mkuranga bado ni nyingi mmno,nimenunua heka 90 elfu,heka 20 kwa 1.8million,hazina mazao ,ni uwala tu, na miembe michache,lilikuwa limepandwa nanasi,miaka 3iliyopita mkuranga,kuna mto,65km from BP roundabout kilwa Road.
nadhani bei hiyo ni ya shamba lenye mazao yakudumu mengi,ila kwa msolwa mashamba mengi yalio na mazao ya kudumu ni KOROSHO ambazo uzalishaji wake mdogo,.
nadhani kwa bei hiyo inabidi utufafanulie shamba lina mazao yapi na uzalishaji ukoje?
 
Mkuu umenikumbusha uwala wangu.

Miaka mitatu iliyopita mimi nilinunua eka kwa Tsh 25,000/ lakini leo nikitaka kupanua eneo langu wananiambia bila laki tatu sipati kitu,watu ni wale wale na uwala ni ule ule. Siku hizi watu wanaamka kwa kasi. Bei zinaanzia mbili na nusu kwa eka mpaka sita pale pale Msorwa,sababu ni nyingi za bei kupanda.

Kijiji kinachofuata kama unaenda beach kitongoji cha Boza, eka moja inacheza kati ya milioni moja mpaka mbili. Kwa maneno mengine,ardhi ya Shungubweni ni ghari zaidi kuliko Msorwa,sababu ni kwamba mafisadi wamepora sana kule Shungubweni kuliko Msorwa plus ten percent issues.

Hili shamba la Msorwa ninalosema,limepanda bei ghafla kwa sababu ya dalili za maendeleo zilizopo pale ndio maana wenyewe wameshituka. Flow ya magari kwenda pale imeongezeka na dalili za ujenzi zipo. Maji ya kudumu ni sababu nyingine,panafikika hata kwa tax, mazao ni mikorosho na imejaa sana ktk shamba.

Kuna mashamba mpaka ya laki moja kwa eka,hayana maji,hayafikiki kwa gari(mchanga sana),nyani kibao na usafiri wa kawaida haupo. Ila kwa mwenye uwezo naweza kumuonyesha yalipo.
 
Mkuu Malila nimekusoma.
mimi shamba lipo 13km from mkuranga center,eneo linaitwa KISE njia ya kwenda BUPU ,huko bei bado ni poa,ila naweza kufika kwa corola,na kuna vihice sh 2500 from mbagala.sijawahi kuvitumia ila nimeshawahi kumtuma mtu apeleke pesa na kukagua kazi alipanda dalala amesema haikumchukua muda kufika huko kutokea mbagala.
nafikiria kwenda mbele zaidi,maeneo ya nyamisati.
 
Njia ipi pale,unafuata ya kwenda kisiju au ya Mtwara? Hapo kise kuna mto au visima?
 
wakuu,kama kuna mtu anaconnection yoyoe morogoro anisaidie natafuta shamba huko,maana nimesikia morogoro unaweza kuchimba na ukapata maji ,ambayo hayana chumvi pia,kwa ajili ya irrigation.
 
Moja lipo km 78 toka Dsm kwenda Mkuranga,lina mikorosho,linapakana na mto usiokauka,usafiri wa daladala toka mbagala upo. Halifai kwa kilimo cha mazao ya nafaka,linafaa kwa matunda na ufugaji wa aina zote. Bei kwa eka laki sita. La pili ni kama km 60 hivi,linafaa kwa kilimo cha mazao yote na ufugaji,lipo kando ya barabara na usafiri wa daladala upo,ukubwa yapata eka 10 hivi na lina kibanda kibovu na lina mazao ya pwani,bei 5M. Hili lina maji ya msimu wa masika tu. Haya mashamba nimeyaona.

Mkuu hilo la km 78 from Dar ni ekari ngapi? Je na hizo bei ni fixed au negotiable? Niko interested Mkuu. Tupatie na contacts mkuu.
 
Moja lipo km 78 toka Dsm kwenda Mkuranga,lina mikorosho,linapakana na mto usiokauka,usafiri wa daladala toka mbagala upo. Halifai kwa kilimo cha mazao ya nafaka,linafaa kwa matunda na ufugaji wa aina zote. Bei kwa eka laki sita. La pili ni kama km 60 hivi,linafaa kwa kilimo cha mazao yote na ufugaji,lipo kando ya barabara na usafiri wa daladala upo,ukubwa yapata eka 10 hivi na lina kibanda kibovu na lina mazao ya pwani,bei 5M. Hili lina maji ya msimu wa masika tu. Haya mashamba nimeyaona.

mie napenda sana kupata shamba kwa muda huu naomba unipe details zaidi ili mwisho wa mwezi nakuja bongo kupiga kura na ikiwezekana nichukue hilo shamba.
nataka hilo linalopakana na mto ila kama bajeti itanishinda basi naangukia hilo jingine yote itabidi niyaangalie, kama bahati ni yangu nadhani nitayakuta.
Nipe details zaidi mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom