Mashaka ya uraia na usalama wetu Tanzania, wageni wameingilia mchakato! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashaka ya uraia na usalama wetu Tanzania, wageni wameingilia mchakato!

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by busar, Aug 6, 2012.

 1. b

  busar JF-Expert Member

  #1
  Aug 6, 2012
  Joined: Dec 22, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Nchi inaporomoka tena kwa kasi, kasi ya ajabu. Imeshaporomoka katika Elimu, Afya,, Kilimo, Ukusanyaji kodi, matumizi ya fedha iliyopo, na mengine mengi.

  Hili la uraia ndo litaimaliza nchi yangu Tanzania Tanzania tuipendayo kwa moyo wote. Nimeshuhudia wahindi, waarabu, na weupe kadhaa wakialikana kutoka makwao kuja kujiandikisha kupata vyeti vya uraia. Hata kiswahili hawakijui..

  Hii inatufikisha pabaya, tena pabaya.

  Nchi Haina mwenyewe...

  Napendekeza zoezi hili lifutwe.
   
 2. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #2
  Aug 6, 2012
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,466
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Too sad.Hali ni mbaya kuliko maelezo.
   
 3. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #3
  Aug 6, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,490
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  Nimeshuhudia huku Kiwalani wapakistani na wahindi kibao wakijiandikisha, sijui serikali iko wapi!?
   
 4. Neiwa

  Neiwa JF-Expert Member

  #4
  Aug 6, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 728
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Nadhani sio kila kitu cha kulaumu serkali ama usalama wa taifa, katika mahojiano mengi yalofanyika na viongozi mbali mbali juu ya zoezi la kujiandikisha vitambulisho vya taifa walitoa tahadhari kuwa kuna raia watataka kujifanya ni wananchi na wapate hivo vitambulisho. Vigezo na masharti wameweka ni mengi mengine hadi ni kikwazo kwa sie wenyewe wananchi.

  Pia tambua kuwa kuna vitambulisho vya wale ambao ni Watanzania na wale ambao sio watanzania na wanaishi hapa Tanzania (ikihusisha wahindi, waarabu, na wengine wengi kutoka nchi za majirani lakini ni wakazi wa Tanzania ambao pia wanapata vitambulisho vya taifa ila vikionesha wazi sio raia bali mgeni).

  Sasa sababu wenzetu wana nidhamu sana katika sector ya vitu kama hivo (usalama na kujiandikisha mambo ya msingi) wao ni lazima wameipa kipaumbele kuliko hata sie wenyewe raia. Naamini kabisa kama wana ndugu yupo nje na mara kwa mara huishi hapa nchin hawaoni taabu kugharamia kurudi nchini kujiandikisha.

  Na hata hivo umeshauriwa ukiona ukiritimba wowote unafanyika katika uandikishaji iwe reported.
   
 5. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #5
  Aug 6, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,058
  Likes Received: 858
  Trophy Points: 280
  Kwanini watu wa muundo huo wapewe vyeti vya uraia jamani?Au wanajiandikisha kama wakimbizi?Hii nchi inakera sana aisee!!
   
 6. Kiwi

  Kiwi JF-Expert Member

  #6
  Aug 6, 2012
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 949
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Mimi binafsi nashangazwa sana na mchakato mzima wa vitambulisho vya raia wa Tanzania na umuhimu wake, hasa kwa kuwa ni wiki chache tu kabla ya sensa. Ninasikia harufu ya ulaji mkubwa sana ambao unafichwa kupitia zoezi hili.

  Sioni kwa nini watu wapange foleni kutwa nzima ili kujaza fomu ambazo baadaye watapatiwa vitambulisho, na huku mwezi huu huu wa nane kutakuwa na zoezi la kuwahesabu watu. Kwa nini kama suala la vitambulisho vya raia wa Tanzania lilikuwa/au ni muhimu, wahusika wa kuandikisha watu wasiwe walewale watakaopita kila nyumba kuhesabu watu? Hapo serikali itakuwa imeua ndege wawili kwa jiwe moja, na kero ya kupanga foleni na hatimaye kuambiwa rudi kalete barua ya mjumbe n.k vitaondoka.

  Pili, kwa mtazamo wangu ni rahisi zaidi kujua nani ni raia na nani si raia kwenye kaya zetu. Ninaamini bado wajumbe wa nyumba kumi wapo, hata kama wanaitwa kwa jina lingine, sijui ndiyo wenyeviti wa serikali za mitaa. Hawa watu tunao mitaani mwetu, na ninavyoelewa wao wanawafahamu (au wanatakiwa kuwafahamu) vizuri watu wao. Wangewezeshwa wao kuwa na madaftari ya orodha ya kila mtu anayeishi kwenye mitaa yao.

  Kila mtu aende kujiandikisha kwa mjumbe wake, akiwa na taarifa zake kamili. Mjumbe atafahamu mtu huyo anafanya kazi gani (ya kuajiriwa ama ya kujiajiri, ama mkulima n.k.), amezaliwa wapi, kama si mwenyeji wa eneo hilo basi anatokea wapi (mkoa gani au kijiji gani), umri wake, jinsia, ameoa/ameolewa, ana watoto wangapi, elimu yake, na ikibidi hata suala la imani (dini) ambalo limeleta kizungumkuti sana kwenye sensa litapatiwa ufumbuzi. Mwenyekiti wa serikali ya mtaa anawajua watu wake, hata kama kuna mkimbizi kajichimbia katikati ya watu wa eneo lake atajulikana. Na kama kuna mhamiaji halali au asiye halali atajulikana.

  Miaka ya mwanzoni mwa 80 kulikuwa na uhaba wa bidhaa mbalimbali nchini, tukawa na orodha za kaya ili kudhibiti upatikanaji wa bidhaa adimu kama sukari, unga, mchele n.k. Nakumbuka kabisa wenyeviti wa serikali za mitaa enzi hizo tukiwaita wajumbe wa nyumba kumi ndiyo waliopewa jukumu la kuandikisha watu. Zoezi lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kuwa mjumbe alikuwa na orodha ya kila mkazi wa nyumba zilizo chini ya eneo lake. Tuliandikisha mpaka wafanyakazi wa majumbani. Nia ilikuwa mtu yeyote asife njaa, na chakula kipatikane kutosheleza idadi ya watu. Ilikuwa ukienda dukani kununua bidhaa unaenda na kitabu chako kinachoonyesha ukubwa wa kaya yako. Na ukipata mgeni ilikuwa lazima utoe taarifa kwa mjumbe ili ijulikane ya kuwa kaya imeongezeka ukubwa na idadi ya mahitaji yako pia imeongezeka. Nakumbuka kuna kaya kubwa zilikuwa zinaweza kupata kilo 3-4 za sukari kwa wiki, lakini kama kaya yako ni ndogo unapewa kilo mbili kwa wiki. Na orodha yote alikuwa nayo mjumbe wa nyumba kumi (mwenyekiti wa serikali ya mtaa)

  Nimeurudia mfano huu kuonyesha ya kuwa 'system' ilikuwepo na bado ipo. Kama kweli nia ni kupata vitambulisho vya uraia ingeweza kufanyiwa kazi ili kupunguza matumizi mabaya ya fedha na kuondoa mianya inayoweza kutumiwa na wajanja kupata vitambulisho ambavyo hawastahili. Vilevile hii ingepunguza kero na usumbufu uliojitokeza wa watu kupanga foleni kutwa nzima, kwa kuwa mjumbe angeweza kwenda majumbani mwa watu wake kwa nafasi zao na kupata taarifa zote.

  Kwa huu utaratibu unaotumika sasa hivi zoezi zima ni mchezo wa kitoto.
   
 7. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #7
  Aug 6, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Vitambulisho viingekuwa kwa Watanzania pekee, nahisi kuna ulaji ushaingia hapo.
   
Loading...