MC RAS PAROKO
JF-Expert Member
- Feb 14, 2013
- 623
- 595
Ipo tofauti kati ya mtawala na kiongozi, uongozi ni kuonesha njia ila
utawala ni uongozi bandia. Baada ya hapo unaweza kupima viongozi wa nchi hii na ndipo utagundua wengi wamevaa koti la uongozi ilihali ni watawala. Wapo watu wachache wanaotawala watu wengi kwa maslahi yao wachache na kuna mbinu za kutawala wanasema ukitaka kuwatawala watu lazima uwagombanishe ili washindwe kuwa na umoja wa kupambana na wewe mtu mmoja au kikundi cha watu, wasiwasi nilionao mimi hawa watawala wetu huenda wanatumia mbinu hii ili tushindwe kuwapindua kwani ukiangalia taifa letu kuanzi uhuru miaka ya 1961 hakuna wakati nchi hii imekua na nyufa au mipasuko kama hii tunayoisikia wakati huu mara gas huko mtwara, mara muungano huko zanzibar, mara waislam na wakristu, mara Bakwata na necta hapa ndo ninaanza kupata mashaka kwamba huenda vitu hivi vinatengenezwa na baadhi ya watawala wetu ili sisi tukae kujadili udini, ukanda n.k na wao waendelee kutuibia rasilimali zetu. Mtanzania mwenzangu amka ili tuwe na umoja kama taifa kwani umoja wetu ndio utatusaidia na tukiwa wamoja HATUSHINDWI NA LOLOTE. Na siku moja tutafurahia rasilimali zetu kwa kuaga umaskini na kula mema{keki} ya taifa pamoja kama ndugu.
Ila tukikubali kupalilia mbegu za chuki na ubaguzi ambazo nina mashaka zinapandwa na wale watawala wetu kuna hatari ya kuwa na somalia hapa, na hao watawala wagawane keki ya taifa wao wenyewe tena gizani bila sisi kujua kutokana na tofauti zetu.
"SISI SOTE NI NDUGU TUEPUKE KUBAGUANA" naomba kuwasilisha