Mashaka: nchi hii kuna watu wachache wanaotawala watu wengi.

MC RAS PAROKO

JF-Expert Member
Feb 14, 2013
623
595
Ipo tofauti kati ya mtawala na kiongozi, uongozi ni kuonesha njia ila
utawala ni uongozi bandia. Baada ya hapo unaweza kupima viongozi wa nchi hii na ndipo utagundua wengi wamevaa koti la uongozi ilihali ni watawala. Wapo watu wachache wanaotawala watu wengi kwa maslahi yao wachache na kuna mbinu za kutawala wanasema ukitaka kuwatawala watu lazima uwagombanishe ili washindwe kuwa na umoja wa kupambana na wewe mtu mmoja au kikundi cha watu, wasiwasi nilionao mimi hawa watawala wetu huenda wanatumia mbinu hii ili tushindwe kuwapindua kwani ukiangalia taifa letu kuanzi uhuru miaka ya 1961 hakuna wakati nchi hii imekua na nyufa au mipasuko kama hii tunayoisikia wakati huu mara gas huko mtwara, mara muungano huko zanzibar, mara waislam na wakristu, mara Bakwata na necta hapa ndo ninaanza kupata mashaka kwamba huenda vitu hivi vinatengenezwa na baadhi ya watawala wetu ili sisi tukae kujadili udini, ukanda n.k na wao waendelee kutuibia rasilimali zetu. Mtanzania mwenzangu amka ili tuwe na umoja kama taifa kwani umoja wetu ndio utatusaidia na tukiwa wamoja HATUSHINDWI NA LOLOTE. Na siku moja tutafurahia rasilimali zetu kwa kuaga umaskini na kula mema{keki} ya taifa pamoja kama ndugu.
Ila tukikubali kupalilia mbegu za chuki na ubaguzi ambazo nina mashaka zinapandwa na wale watawala wetu kuna hatari ya kuwa na somalia hapa, na hao watawala wagawane keki ya taifa wao wenyewe tena gizani bila sisi kujua kutokana na tofauti zetu.

"SISI SOTE NI NDUGU TUEPUKE KUBAGUANA" naomba kuwasilisha
 
Ni kweli, na mbaya zaidi tumegeuka kama wale wa uwanja w fisi wachezao kila santuri baada ya kuweka " mambo yao"
 
Mleta mada ana hoja hapa. Watawala wanatugawa tunagawika

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mleta mada ana hoja hapa. Watawala wanatugawa tunagawika

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

nashukuru mkuu mdeki huwa naamini msomi hapuuzii jambo lolote. Tatizo ndo hilo tumekubali kupangwa kwa mafungu mafungu kama nyanya sokoni
 
Last edited by a moderator:
Wakati bado tunao wa sisi kubadili fikra zetu kwani Tanzania tuipendayo tunapaswa kuitengeneza wenyewe bila kusikiliza porojo za wanasiasa ambao kwa kiasi kikubwa wana mchango mkubwa kwenye haya matatizo yetu tuliyonayo.
 
ni kweli kwani kila binadamu ana akili yake binafsi na ukiwa upande wa kulia wa mwenzako yeye atakuona upo kushoto kwake.

Hoja yako ni ya msingi ila sio ngeni , hoja kama hizi zimejadiliwa sana hapa jamvini ndio maana nikasema sioni jipya. jaribu kutanua fikra basi uje na kitu kipya sio kila siku tunajadili jambo hilo hilo.
 
Hoja yako ni ya msingi ila sio ngeni , hoja kama hizi zimejadiliwa sana hapa jamvini ndio maana nikasema sioni jipya. jaribu kutanua fikra basi uje na kitu kipya sio kila siku tunajadili jambo hilo hilo.

nalifahamu hilo ila tambua kwamba jf ni jukwaa huru na kila siku member wapya wanajisajili nao pia wanahitaji mada kama hizi kwani hawakuziona kabla na wapo members wa muda mrefu lakini hawajapata wasaa wa kuyajadili haya ila nashukuru kwa mawazo yako na ninayaheshimu pia. Ahsante
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom