Mashaka juu la andiko la mke mmoja katika Biblia

Weakman

JF-Expert Member
Jul 23, 2021
861
1,384
Kuna Mambo mengine yanapaswa kufikiriwa kwa kina

Tumeona katika biblia jinsi mababa wa Imani walivyojitwalia wanawake wengi wakawaoa na kuwazalisha hapo kale

Desturi hio ilitamalaki kwa Karne na Karne, na inachofurahisha ni hata wapakwa mafuta wa Bwana walijikusanyia warembo wakutosha kwenye makazi yao

Hivi kweli Mungu Wetu alikuwa anachukizwa na desturi hiyo na kwamba alikuwa anavumilia tu?
Mungu alikuwa mkali Sana katika suala la kuishi kitakatifu, Aaah jamaani! Yaani ashindwe kuwadhibiti katika hili dogo tu la kuwabana wawe na mke mmoja!?

Tazama Mfalme Daudi alipora mke na alizaa nae mtoto ambae alikuja kuhudumu Kama Mfalme wa Taifa Hilo la Mungu,

Najiuliza Tena, hivi Paulo mtume aliyepita kufungua makanisa na wengi kubatizwa waliwaacha wake zao baada ya kubatizwa na kuwa wakristo?

Kuna hoja dhaifu imetolewa kwenye biblia eti waliachwa waoe wake wengi kwa sababu ya udhaifu/ugumu wa mioyo yao, basi hata sheria zingine zisingewekwa kwa sababu ya Ugumu wa mioyo yao

Hapa wakristo tumepigwa na kitu kizito!

Ama ni maandiko yaliyoongezwa na kanisa letu katoliki, au aliyetafsiri eneo Hilo kutoka kugha ya asili ya biblia ameingia Chaka, alishindwa kupata maneno sahihi ya kiingereza

Leteni fikra zenu!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Na mimi nakuuliza! Jee Mungu Alikosea Kumuumbia Adam Eva m.1??
 
Hivi ni kweli aliumba Adam na Eva tu? Au hao ndo waliotajwa? Kaini alipomuua abeli ni taifa lipi alikimbilia? Na hilo taifa lilitokana na Adam na Eva tu?
 
Na mimi nakuuliza! Jee Mungu Alikosea Kumuumbia Adam Eva m.1??
Mada inajaribu kuchunguza uhalali wa maandishi yanayoibua sheria ya Mke mmoja,
Wewe unaleta hoja ya Mungu kukosea kuumba!
Yaani unataka tutafute makosa ya MUNGU kwa kutumia maandiko ya Mwanadamu?
Mungu hapimwi kwa maandiko ya wanadamu, Bali maandiko yanapimwa kwa kuhusianisha uhalisia na uweza wa MUNGU!

Swali lako lilipaswa kuwa, "Je! maandiko ya Adamu kuumbiwa Eva mmoja yamekosewa?"

Jibu Ni kwamba, "Hayajakosewa"
Maandiko hayo yamekusudia kuwafunulia wanadamu kuwa
1. Mungu ndio muumba
2.Mungu amemuumba Mwanadamu kwa jinsia mbili, nazo zitajamiiana na kuzaliana
3.Mume Ni mkuu wa familia!
4.Mume asipokuwa na akili ataangushwa kiuchumi, kisiasa na kimaadili na mwanamke

Maandiko hayo hayakukusudia kuleta sheria ya ndoa
1.Mke mmoja
2. Kutoa mahari
3.Wazazi ndio wenye mamlaka ya kuidhinisha ndoa
4. Mchungaji na Imamu ndio wenye mamlaka ya kufungisha ndoa

Nikukumbushe, kwenye maandiko hayo Mungu amempa mume mamlaka ya kumtawala mwanamke!
Kuoa na kutoa talaka, kuoa zaidi ya Mke mmoja ni sehemu ya kumtawala mwanamke

Kwenye Safina Nuhu alitwaa viumbe wawili kwa agizo la Mungu, yaani ng'ombe wawili dume na jike, kuku wawili dume na jike na wengineo
Hio ilimaanisha viumbe hao wakazaliane Mara baada ya gharika kumalizika!
Haikuwa na maana kuwa jogoo awe na jike moja tu eti kwa sababu Mungu alimuamuru Nuhu kuchukua dume moja na jike moja!

Kwani hujui Mungu Amekaimisha baadhi ya Mamlaka Yake kwa Kanisa??
 
Back
Top Bottom