Mashairi ya wimbo wa Nick wa Pili

mandwa

JF-Expert Member
Aug 13, 2013
1,359
1,250
Msaanii tajwa ametoa wimbo mpya unaitwa Sitaki Kazi mwenye mashairi aweke hapa

Verse 1

Uko wasiwasi mtu bila nafsi/ umeajiriwa shirika la mtu binafsi.

Sina wasiwasi mtu mwenye nafsi/ sijaajiriwa nimeajiri yangu nafsi.

Poleni mishahara imejaa makato/

Biashara mjini ndo zimejaa mapato.

Poleni ajira itakulinda toa vyeti/

Sihitaji kulindwa mi sio mtoto wa geti.

Tokeni ajira ni mpaka wa akili yako/

Mpaka ufukuzwe kazi ndo ugundue kipaji chako.

Ajira ya mkeo chini ya boss /

We housegirl pekee nchini anakuita boss.

Sivai tai siikatai utamaduni wangu mi ni kuuliza why.

Elimu bongo imekosa plani ya pili/ kosa la pili haufundishwi kuwa tajiri.
 

qn of sheba

JF-Expert Member
Sep 13, 2011
3,230
1,250
Verse 1

Uko na wasiwasi mtu bila nafsi/ umeajiriwa shirika la mtu binafsi.
Sina wasiwasi mtu mwenye nafsi/ sijaajiriwa nimeajiri yangu nafsi. (Poleni).
Mishahara imejaa makato/
Biashara mjini ndo zimejaa mapato. (Poleni)
Ajira itakulinda toa vyeti/
Sihitaji kulindwa mi sio mtoto wa geti. (Tokeni)
Ajira ni mpaka wa akili yako/
Mpaka ufukuzwe kazi ndo ugundue kipaji chako. (Oneni)
Ajira ya mkeo chini ya boss /
We housegirl pekee nchini anakuita boss.
Sivai tai siikatai utamaduni wangu mi ni kuuliza why.
Elimu bongo imekosa plani ya pili/ kosa la pili haufundishwi kuwa tajiri.
 

MBUFYA

JF-Expert Member
Aug 15, 2011
445
170
Huu wimbo umesifiwa hata na Waziri wa kazi na ajira. Leo bubgeni katika utangulizi wa hotuba yake
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom