Mashahidi wakwamisha kesi ya Mchungaji Mtikila | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashahidi wakwamisha kesi ya Mchungaji Mtikila

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, May 3, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mwenyekiti wa Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila.  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kesi ya kutoa lugha ya uchochezi na kudai kuwa Rais Jakaya Kikwete ni gaidi, inayomkabili Mwenyekiti wa Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, jana ilishindwa kuendelea kusikilizwa ushahidi baada ya mashahidi kushindwa kufika mahakamani.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kesi hiyo ilipangwa kuanza kwa kusikilizwa ushahidi wa upande wa Jamhuri mbele yan Hakimu Mkuu Mkazi Genivitus Dudu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ponsiano Lukosi, aliomba mahakama kupanga tarehe nyingine ya kuanza kusikiliza kwa sababu mashahidi waliotarajiwa kutoa ushahidi hawakufika mahakamani.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Hakimu Dudu alisema mahakama haina pingamizi na maombi hayo ambapo aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 17, mwaka huu itakapoanza kusikilizwa.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Awali, upande wa mashitaka katika kesi hiyo ulidai kuwa unatarajia kuita mashahidi tisa watakaothibitisha tuhuma dhidi ya Mtikila.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mtikila anadaiwa kuwa Oktoba 21, mwaka 2007, kuitisha mkutano na kutoa lugha ya uchochezi katika viwanja vya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Ilala jijini Dar es Salaam.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Upande wa mashitaka ulidai kuwa unatarajia kuita mashahidi tisa ili kuthibitisha mashitaka dhidi ya Mtikila.[/FONT]
  “[FONT=ArialMT, sans-serif]Ahadi zote za Jakaya Kikwete siku zote zinaongozwa na imani yake ya dini tena kutekeleza malengo yake ya kusilimisha nchi….hatuwezi kuvumilia mtu anayekuwa muhuni aongoze nchi…” ilinukuliwa hati ya mashitaka.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Ilidaiwa kuwa Oktoba 21, 2007 katika eneo la Ilala katika kota za NHC zilizopo karibu na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), mshtakiwa alitoa lugha za uchochezi.[/FONT]  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Hawamuwezi huyu jamaa.
   
Loading...