Mashahidi kesi ya Ponda wajichanganya

Waislam warudishiwe kiwanja chao, bakwata ni taasisi kandamizi iliyopoteza dira na mwelekeo
 
Ni wakati muafaka sasa fisadi aliyejimilikisha kiwanja cha waislam pale markaz chang'ombe amuogope mungu, aachie kiwanja hicho kirudi kwa waislam
 
Kwa matendo ya Ponda na wafuasi wake, anastahili kuozea rumande! Heko serikali kwa kumdhibiti PONDA!
Kama tuna Imani na serikali ya JK kuhusu tuhuma alizozushiwa Sheikh Ponda, basi lazima tukubali serikali hii haina mkono na kutekwa kwa Dr. Ulimboka na mauaji ya Mwangosi
 
Mashahidi wa tatu na nne upande wa Jamhuri katika kesi inayomkabili Sheikh Ponda Issa Ponda, jana walijichanganya baada ya kushindwa kuieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wanakifahamuje kiwanja cha Bakwata cha Marcus Changombe walichobadilishana na Kampuni ya Agritanza Limited na kupewa kiwanja cha Kisarawe.

Mashahidi hao ni Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini Masood Mkome (72), Bakwata pamoja na Meneja Ujenzi wa Kampuni ya Agritanza Limited Hafidh Seiph Othman (42).

Mkome aliulizwa maswali na Wakili wa Serikali Tumaini Kweka kama ifuatavyo:

Wakili: Umekuja mahakamani kuongelea mabadilishano kati ya kiwanja cha Marcus kuwa cha Agritanza, shahidi unakumbuka tarehe mliyobadilishana?

Shahidi: Sikumbuki mwaka wala tarehe kwa sababu siwezi kujua kila kitu.
Wakili:Wewe kama Mwenyekiti mnapata wapi mamlaka ya kiutendaji,na ilikuaje kuhusu eneo la Marcus Chang’ombe?

Shahidi: Tulipata nguvu katika Baraza la Wadhamini la Ulamaa.
Wakili: Mnasema mlibadilishana kwa njia gani?

Shahidi: Muulize Katibu Mkuu Said Loniwa kutoka Baraza la Wadhamini ndiye Katibu Mkuu wa Baraza na ndiye mwenye mafaili yote.

Wakili wa Juma Nasoro wa upande wa utetezi naye alimhoji shahidi kama ifuatavyo:
Wakili: Wewe kama shahidi umewahi kufika katika kiwanja cha Kisarawe mlichobadikishana na Agritanza?

Shahidi: Sijawahi kufika ila kuna baadhi ya watu wa baraza la wadhamini wameenda na siwafahamu kwani kipindi hicho sikuwepo.

Wakili: Je, unao muhtasari wowote au maandishi yanayoonyesha mkataba mlioingia na kampuni ya Agritanza?

Shahidi: Siwezi kujua vitu vipo kwenye mafaili na muhifadhi ni Katibu Mkuu na siwezi kukumbuka kila kitu hata wewe huwezi ila unajua kuuliza tu.

Wakili wa utetezi, Yahaya Njama alipomhoji, shahidi aligoma akidai ni maswali mengi, lakini hakimu alimuamuru ayajibu.

Wakili:Wewe ni kabila gani?
Shahidi: Sisi wote ni Watanzania na usiniulize mambo ya ukabila.

Wakili: Nyie mlikuta kimeuzwa mkamalizia je,wanachama wenu ambao ni Waislamu watawaaminije na wakizuia kuuzwa watakuwa na kosa?

Shahidi aliiambia mahakama kuwa waliopoteza uaminifu hawapo na alipoulizwa swali amekuja kufanya nini mahakamani wakati hajui mshtakiwa wala mshtaki, alidai kuwa alikwenda kutoa ushahidi wa kubadilishana kiwanja.

Shahidi wa pili, Hafidh Seiph alidai kuwa ndiye aliyeenda polisi Chang’ombe baada ya kuvamiwa na kuibiwa.

source: nipashe

MY TAKE.
KWELI PONDA KASHTAKIWA KWA KOSA LA KIWANJA MBONA ANANYIMWA DHAMANA. MBONA ANAFUNGWA PINGU? AU MFUMO UPO KAZINI?
MAANA UKITAKA KUKERA MFUMO FANYA HAYA
1)Likemee BAKWATA. uKIFANYA HAYO UTAENDANA NA DHANA NZIMA YA UUNDWAJI DHIDI YA KURUDISHA NYUMA MAENDELEO YA WAISLAM
2)Hoji utendaji wa NECTA. Hapa utawakera wale wanaofaidi ambao wengi wapo katika system
3)zungumzia OIC na hoji Vatican na MOU.
hiyo ndio serikali ya ccm dhidi ya waislam wa kweli,lakini uchaguzi ukikaribia atapewa dhamana au kuachiwa kabisa kutaka kura za waislam wa kweli
 
Naomba kuelimishwa, hivi Sheikh Ponda ameshitakiwa kwasababu ya
1. Kuikemea BAKWATA?
2. Kuhoji utendaji wa NECTA?
3. Kuzungumzia OIC, Vatican na MoU?

Kama sio hayo mashitaki yaliyoko mbele ya mahakama, kwanini sasa mleta thread anayaunganisha na kesi inayomkabili Ponda?. Sitashangaa nikiambiwa kwamba huko MSIKITINI mnadanganywa kwamba Ponda ameshitakiwa kwa makosa hayo na nyinyi (waislamu) bila kufanya utafiti mnachukulia hizo CHUKI na UCHOCHEZI as the WORD OF GOD. Kweli waliosema kwamba If you think education is expensive try ignorance hawakukosea. Inaelekea wenzetu mumeamu kujaribu UJINGA.

Hizi kejeli na matusi mnayoyatoa iko siku you'll pay for it, ila we si wa kwanza kutoa kejeli na matusi hivyo sikulaumu umekua ukikua ukisikia waislam watanzania wenzio wakitukanwa na wazee wako nae ukarithi. Besides, vilivyotajwa hapo juu ni miongoni mwa vile Kova alivyosema vinahatarisha usalama wa taifa na hawakua na ushahidi wa kutosha kwa kumkamata kwavyo mana hizo ndo zilikua hoja za waislamu watanzania kama unakumbuka na ulikua ni ukweli kweli tupu kuwa vinazuia maendeleo ya jamii ya waislam hapa Tanzania ndomana wakatumia kesi ya kiwanja kumnyima dhamana wakidhani wanamkomoa, ila iko siku hawawatu mtaongea nao kwa lugha ambayo mtaelewana..we kuwa mpole tu na hapo ndo utagundua thamani ya kusikilizana na kuheshimiana na madhara ya Psychologia ya kushindwa...
:shut-mouth::shut-mouth::shut-mouth:
 
.... tunaweza tusikubaliane katika mambo mengi na bwana ponda, lakini uamuzi wa bakwata kuachia ekari nne za chang'ombe kwa kisingizio chochote kile ni uamuzi wenye walakini. upo uwezekano wa kesi hii kuivua nguo bakwata na kumwongezea kete ponda kama mtu makini na mwenye uchungu na mali za waislamu. tusubiri tu ukweli utabainika ndani ya mahakama.
Watu wengi (nadhani nawe ni mmoja wao) wanasahau mashtaka ya Ponda ni yapi, na utetezi wake unatakiwa uwe vipi. Hapo mahakamani Ponda ameshtakiwa kwa kuvamia kiwanja na kuiba mali ya mamilioni ya fedha. Sasa hata kama ni kweli itabainika kuwa Bakwata walikiuza kile kiwanja kwa makosa, je, hilo litasaidia vipi Ponda kukwepa mashtaka yake ya wizi? Je, mimi nikiweka vitu vyangu kwenye yard yako ambayo awali nilipewa kihalali, ukavichukua na kutokomea navyo, na ushahidi ukaonyesha ni kweli ulivichukua (haukuripoti polisi), unadhani utakwepa adhabu hapo eti kwa kisingizio kuwa eti sasa yard imebainika kuwa ni yako, na kwamba mimi sikumilikishwa kihalali? Hapa kesi sio Ponda et al Vs Bakwata, ni Ponda et al Vs Jamhuri. Sasa hata kama Bakwata wataumbuka, Ponda atakuwaje shujaa akiwa amefungwa kwa wizi?
 
Kama tuna Imani na serikali ya JK kuhusu tuhuma alizozushiwa Sheikh Ponda, basi lazima tukubali serikali hii haina mkono na kutekwa kwa Dr. Ulimboka na mauaji ya Mwangosi
Fitinamwiko,
Bw Ponda amekutwa live akishiriki kubomoa na kuiba mali za wenyewe na pia amekutwa akihamasisha na kushiriki kujenga msikiti katika kiwanja cha wenyewe bila kufuata utaratibu. Haya ni makosa ya jinai na yanastahili adhabu kali ili iwe funzo kwa wengine!

Dr Ulimboka ametekwa na watumishi wa Ikulu ambao majina yao yametajwa wazi na Dr. Ulimboka mwenyewe na gazeti la mwanahalisi ambalo pia liliorodhesha namba zao za simu! Hapa serikali haijakanusha hivyo ni wazi kuwa kuna mkono wake!

Mauaji ya Mwangosi bila shaka na kama picha zilivyoonyeshwa katika baadhi ya magazeti na mitandao ya jamii yalifanywa na polisi chini ya uongozi wa RPC wa Iringa. Hapa serikali imehusika moja kwa moja!

Hivyo ndugu yangu tofautisha mazingira ya matukio haya!
 
Ponda anatakiwa achiwe huru.Lasivyo tuamue waislamu tuingie kitaa
 
Nakumbuka mchungaji mtikila aliwahi kuwekwa ndani na kunyimwa dhamana.

nakumbuka wachungaji wa Upatu wa DECI walikaa ndani kwa muda mrefu bila kupata dhamana.

ni hao wachache kwa leo ukitaka wengine nitakutajia.

kuchanganya imani na sheria ni kuwachanganya waumini na wafuasi wa dini.
wanahitaji elimu dunia mkuu
 
Badala ya kuelekeza lawama kwa rais ni mantiki zaidi kumlaumu mwislamu aliyekubali kununua kiwanja cha waislam wenzake ambacho kingetumika kwa maendeleo yao na huyo ndiye shahidi namba moja dhidi ya Ponda mahakamani.
Angenunua MKRISTO SJII INGEKUWAJE!
 
Eliezer Feleshi(DPP) tunataka apunguziwe madaraka katika katiba ijayo.Inshallah sheikh wetu Pondamali issa pondamali ataepuka dhulma na upokwaji wa haki na uhuru toka kwa hawa masheitwani.Amen!
 
Fitinamwiko,
Bw Ponda amekutwa live akishiriki kubomoa na kuiba mali za wenyewe na pia amekutwa akihamasisha na kushiriki kujenga msikiti katika kiwanja cha wenyewe bila kufuata utaratibu. Haya ni makosa ya jinai na yanastahili adhabu kali ili iwe funzo kwa wengine!

Dr Ulimboka ametekwa na watumishi wa Ikulu ambao majina yao yametajwa wazi na Dr. Ulimboka mwenyewe na gazeti la mwanahalisi ambalo pia liliorodhesha namba zao za simu! Hapa serikali haijakanusha hivyo ni wazi kuwa kuna mkono wake!

Mauaji ya Mwangosi bila shaka na kama picha zilivyoonyeshwa katika baadhi ya magazeti na mitandao ya jamii yalifanywa na polisi chini ya uongozi wa RPC wa Iringa. Hapa serikali imehusika moja kwa moja!

Hivyo ndugu yangu tofautisha mazingira ya matukio haya!
Mkuu shukrani kwa maelezo!
Kiwanja ni mali ya waislam, wajanja wamekiuza bila idhini yao. Ok forget about this
Kwanini kosa la kuvamia kiwanja, kuiba mali na kuhamasisha kujenga limevaliwa njuga na serikali ya CCM, but makosa ya kuteka na kutesa pamoja na kosa la kushambulia na kuua ambayo yamefanywa na watumishi wa serikali ya CCM yanasuasua?
Kwa umakini wako hayo makosa matatu kama ulivyoelezea, lipi adhabu yake ni kali na lipi ni least?
 
Kwanza nikupongeze kwa kukubali kuwa Ponda ana kesi ya kujibu na akipatikana na makosa lazima atastahili adhabu!

Pili ni kweli kuwa serikali inahusika katika dhahama zilizowakumba Ulimboka na marehemu Mwangosi! Tatizo hapa ni udhaifu wa katiba yetu kutotoa uhuru wa kutosha kwa mhimili wa mahakama! Kwa hiyo wananchi wote tunapaswa kuendelea kuisema na kuikaripia serikali ili hatua muafaka zichukuliwe kwa wote waliohusika na uhalifu huu ili haki itendeke ingawa tunafahamu kuwa kesi ya nyani ukimpelekea ngedere ni vigumu haki kutendeka!

Hivyo kwa kutumia mwanya huu wa mabadiliko ya katiba inatupasa wananchi wote tuvalie njuga uhuru wa mihimili yote ya dola; serikali, bunge na mahakama!
 
Sheikh Ponda anashinda kesi! sababu wale waliouza kiwanja hawakuwa na mamlaka ya kisheria,hivyo mnunuaji alitapeliwa. Tusubiri sheria ichukue mkondo wake
 
Back
Top Bottom