Mashahidi kesi ya Ponda wajichanganya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashahidi kesi ya Ponda wajichanganya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Malaria Sugu, Jan 18, 2013.

 1. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2013
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mashahidi wa tatu na nne upande wa Jamhuri katika kesi inayomkabili Sheikh Ponda Issa Ponda, jana walijichanganya baada ya kushindwa kuieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wanakifahamuje kiwanja cha Bakwata cha Marcus Changombe walichobadilishana na Kampuni ya Agritanza Limited na kupewa kiwanja cha Kisarawe.

  Mashahidi hao ni Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini Masood Mkome (72), Bakwata pamoja na Meneja Ujenzi wa Kampuni ya Agritanza Limited Hafidh Seiph Othman (42).

  Mkome aliulizwa maswali na Wakili wa Serikali Tumaini Kweka kama ifuatavyo:

  Wakili: Umekuja mahakamani kuongelea mabadilishano kati ya kiwanja cha Marcus kuwa cha Agritanza, shahidi unakumbuka tarehe mliyobadilishana?

  Shahidi: Sikumbuki mwaka wala tarehe kwa sababu siwezi kujua kila kitu.
  Wakili:Wewe kama Mwenyekiti mnapata wapi mamlaka ya kiutendaji,na ilikuaje kuhusu eneo la Marcus Chang’ombe?

  Shahidi: Tulipata nguvu katika Baraza la Wadhamini la Ulamaa.
  Wakili: Mnasema mlibadilishana kwa njia gani?

  Shahidi: Muulize Katibu Mkuu Said Loniwa kutoka Baraza la Wadhamini ndiye Katibu Mkuu wa Baraza na ndiye mwenye mafaili yote.

  Wakili wa Juma Nasoro wa upande wa utetezi naye alimhoji shahidi kama ifuatavyo:
  Wakili: Wewe kama shahidi umewahi kufika katika kiwanja cha Kisarawe mlichobadikishana na Agritanza?

  Shahidi: Sijawahi kufika ila kuna baadhi ya watu wa baraza la wadhamini wameenda na siwafahamu kwani kipindi hicho sikuwepo.

  Wakili: Je, unao muhtasari wowote au maandishi yanayoonyesha mkataba mlioingia na kampuni ya Agritanza?

  Shahidi: Siwezi kujua vitu vipo kwenye mafaili na muhifadhi ni Katibu Mkuu na siwezi kukumbuka kila kitu hata wewe huwezi ila unajua kuuliza tu.

  Wakili wa utetezi, Yahaya Njama alipomhoji, shahidi aligoma akidai ni maswali mengi, lakini hakimu alimuamuru ayajibu.

  Wakili:Wewe ni kabila gani?
  Shahidi: Sisi wote ni Watanzania na usiniulize mambo ya ukabila.

  Wakili: Nyie mlikuta kimeuzwa mkamalizia je,wanachama wenu ambao ni Waislamu watawaaminije na wakizuia kuuzwa watakuwa na kosa?

  Shahidi aliiambia mahakama kuwa waliopoteza uaminifu hawapo na alipoulizwa swali amekuja kufanya nini mahakamani wakati hajui mshtakiwa wala mshtaki, alidai kuwa alikwenda kutoa ushahidi wa kubadilishana kiwanja.

  Shahidi wa pili, Hafidh Seiph alidai kuwa ndiye aliyeenda polisi Chang’ombe baada ya kuvamiwa na kuibiwa.


  source: nipashe

  MY TAKE.
  KWELI PONDA KASHTAKIWA KWA KOSA LA KIWANJA MBONA ANANYIMWA DHAMANA. MBONA ANAFUNGWA PINGU? AU MFUMO UPO KAZINI?
  MAANA UKITAKA KUKERA MFUMO FANYA HAYA
  1)Likemee BAKWATA. uKIFANYA HAYO UTAENDANA NA DHANA NZIMA YA UUNDWAJI DHIDI YA KURUDISHA NYUMA MAENDELEO YA WAISLAM
  2)Hoji utendaji wa NECTA. Hapa utawakera wale wanaofaidi ambao wengi wapo katika system
  3)zungumzia OIC na hoji Vatican na MOU.
   
 2. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #2
  Jan 18, 2013
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,061
  Likes Received: 752
  Trophy Points: 280
  Ponda dawa yake kumpiga na mada kesi aozee hukohuko jela
   
 3. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2013
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli. tatizo la nchi yetu akianzwa Ponda atafuata dk slaa. Maana juzi waislam walipigwa katika maandamano. jana tukawaona wanafunzi wa IFM wakitandikwa vigogo. UNAFIKI WETU NDIO UNAOPFIKSHA HAPA
   
 4. p

  petrol JF-Expert Member

  #4
  Jan 18, 2013
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 321
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  Nimesoma gazeti moja likieleza kwamba walibadilisha kiwanja cha chang'ombe ekari nne kwa ekari arobaini huko kisarawe kwa lengo la kujenga chuo kikuu. Kwa mtu anayeelewa thamani ya ardhi katikati ya Dar hawezi hata siku moja kuwaza, achilia mbali kukubali, kuachia ekari nne za mjini kwa ekari 40 za kisarawe. Kama waislamu walitaka eneo kubwa la kujenga chuo kikuu ni wazi serikali isingesita kuwapatia kwa sababu Tanzania haina tatizo la ardhi. Hata wangetaka ekari 200 wangepewa, tena bure tu. tunaweza tusikubaliane katika mambo mengi na bwana ponda, lakini uamuzi wa bakwata kuachia ekari nne za chang'ombe kwa kisingizio chochote kile ni uamuzi wenye walakini. upo uwezekano wa kesi hii kuivua nguo bakwata na kumwongezea kete ponda kama mtu makini na mwenye uchungu na mali za waislamu. tusubiri tu ukweli utabainika ndani ya mahakama.
   
 5. m

  malaka JF-Expert Member

  #5
  Jan 18, 2013
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ndio hivyo tena urafiki unapofikia mwishoni. Na sijui nin kinaendelea maana Manumba nae ugonjwa wake haujulikani. Mungu tupe macho na akili ya kumjua adui yangu kabla aisee.

  Ila mwisho wa yote ELIMU Muhimu sana.
   
 6. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #6
  Jan 18, 2013
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,814
  Likes Received: 1,380
  Trophy Points: 280
  Kwa matendo ya Ponda na wafuasi wake, anastahili kuozea rumande! Heko serikali kwa kumdhibiti PONDA!
   
 7. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #7
  Jan 18, 2013
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,814
  Likes Received: 1,380
  Trophy Points: 280
   
 8. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #8
  Jan 18, 2013
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,969
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Nakumbuka mchungaji mtikila aliwahi kuwekwa ndani na kunyimwa dhamana.

  nakumbuka wachungaji wa Upatu wa DECI walikaa ndani kwa muda mrefu bila kupata dhamana.

  ni hao wachache kwa leo ukitaka wengine nitakutajia.

  kuchanganya imani na sheria ni kuwachanganya waumini na wafuasi wa dini.
   
 9. n

  nemasisi JF-Expert Member

  #9
  Jan 18, 2013
  Joined: Oct 4, 2012
  Messages: 1,860
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Sina matatizo na uislam wala waislam maana zaidi ya yote mzazi wangu mmoja ni muislam lakini ki ukweli Ponda, Ilunga na sheikh Farid huwa akili yangu inakataa kuwaamini, wacha akae kidogo huko ndani maana hata sasa kila mtu anaona, tangu ametulizwa huko ijumaa inatumika kwa swala badala ya vurugu! Acha pumzishwe tu
   
 10. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #10
  Jan 18, 2013
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Hata coloured wa Ki south Africa akili zao zilikataa kumuamini Mandela, Klu klax clun akili zao zilikataa kumuamin Rev. Martin Luther King, Hata shombe shombe wa kiarabu wa sudan akili zao zilikataa kumuamini Hayati John Garang wa SPLA, hata wewe shombeshombe wa kiislam haishangazi akili yako ikikataa kumuamin akina Ponda
   
 11. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #11
  Jan 18, 2013
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,969
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  kaka, umenena.

  wanaochochea uhasama hawajui kuwa tanzania karibu kila nyumba ina mkristo na mwislamu.

  Kuwagawa waislamu na wakristo lazima uonekane mjinga wa kwanza Tanzania.
   
 12. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #12
  Jan 18, 2013
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,969
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Badala ya kuelekeza lawama kwa rais ni mantiki zaidi kumlaumu mwislamu aliyekubali kununua kiwanja cha waislam wenzake ambacho kingetumika kwa maendeleo yao na huyo ndiye shahidi namba moja dhidi ya Ponda mahakamani.
   
 13. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #13
  Jan 18, 2013
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,877
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 180
  Naomba kuelimishwa, hivi Sheikh Ponda ameshitakiwa kwasababu ya
  1. Kuikemea BAKWATA?
  2. Kuhoji utendaji wa NECTA?
  3. Kuzungumzia OIC, Vatican na MoU?

  Kama sio hayo mashitaki yaliyoko mbele ya mahakama, kwanini sasa mleta thread anayaunganisha na kesi inayomkabili Ponda?. Sitashangaa nikiambiwa kwamba huko MSIKITINI mnadanganywa kwamba Ponda ameshitakiwa kwa makosa hayo na nyinyi (waislamu) bila kufanya utafiti mnachukulia hizo CHUKI na UCHOCHEZI as the WORD OF GOD. Kweli waliosema kwamba If you think education is expensive try ignorance hawakukosea. Inaelekea wenzetu mumeamu kujaribu UJINGA.
   
 14. S

  Seif al Islam JF-Expert Member

  #14
  Jan 18, 2013
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 2,158
  Likes Received: 139
  Trophy Points: 160
  mwisho wa kufanya uhuni hapa mjini kwa jina la waislamu umekwisha.
   
 15. R

  Rene Member

  #15
  Jan 18, 2013
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama mashahidi wenyewe ndio wanajibu hivi basi kazi ipo!
   
 16. betlehem

  betlehem JF-Expert Member

  #16
  Jan 18, 2013
  Joined: May 9, 2012
  Messages: 7,279
  Likes Received: 1,783
  Trophy Points: 280
  kwa hiyo kumbe haki inatendeka,waislam wanaofanya madudu kipigo,wanafunzi wakifanya madudu kipigo,wakristo wakijichanganya kipigo; sasa wewe unacholalamika nini kama mwalimu kachapa darasa zima?kwa hiyo kumbe wewe unaridhishwa na jinsi muendesha mashtaka tumaini kweka (mkristo) anavyoendesha kesi kwa kuwabana waliompeleka ponda mahakamani ee? sasa kwa nini tusiiachie mahakama mpaka mwisho kinyume chake tumekaa pembeni tunafufutika!
   
 17. s

  sweke 34 JF-Expert Member

  #17
  Jan 18, 2013
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 694
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye OIC nikutolee mfano. Kama kungekuwa na organization ya nchi za kikristu...na lengo lao ni pamoja na kueneza ukristu na mambo yake mengine. Wewe kama muislam ungekubali Tanzania ijiunge na organization hiyo? Jibu nadhani ni hapana.
  Mambo ya vatican ni sawasawa na Islamic republic of Iran. Wote wana balozi zao hapa.
  Kwani hao wa OIC hawawezi kuwapa misaada yao mpaka tujiunge nchi nzima kama ni nchi ya kiislam??
   
 18. g

  gen parton JF-Expert Member

  #18
  Jan 18, 2013
  Joined: Jan 15, 2013
  Messages: 405
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hili gaid ponda kwanza sio raia wa tz pili anawabuluza mamburula wenzake wasioenda shule mbana waislam walioenda shule huwa hawapo kwenye mkumbo wa anawachukua watu kama yeye wanafiri kwa kutumia masaburi
   
 19. s

  shika Senior Member

  #19
  Jan 18, 2013
  Joined: Nov 3, 2012
  Messages: 167
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  lakini kumbuka PONDA hajawekwa ndani kwa ajili ya uchochezi na vurugu zilizosababisha makanisa kuchomwa moto,la hasha,yupo ndani kwa mashtaka ya mgogoro wa kiwanja na waislam wenzie,bila hivyo Shehe POND angekuwa nje siku nyingi,kwa hiyo wananchi wasidhani kwamba serikali imeshughulikia matatizo ya uchomaji makanisa.
   
 20. A

  Aman Ng'oma Verified User

  #20
  Jan 18, 2013
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 918
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  Mimi naimani nao sana pamoja na kwamba mzazi wangu mmja ni mkristo.Kwasbabu hata akina mandela wakati wanapigania uhuru walionekana ni wakorofi na ni watu wanaotaka kuhatarisha amani ya nchi lakini baadae wakaonekana ni mashujaa.
  Nchi hii tutaivuruga wenyewe kwa kuwakandamiza wengine tena waziwazi.
   
Loading...