Mashahidi 14 kutoa ushahidi kesi ya dawa za kulevya za Sh559 milioni

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na dawa za kulevya (ADU), Godrey Nzowa anatarajia kutoa ushahidi katika kesi ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Cocaine zenye thamani ya Sh559 milioni inayomkabili raia wa Liberia, Ndjane Abubakar.

Abubakar anadaiwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya cocaine zenye uzito wa gramu 13,979 kutoka Brazil kwa kutumia hati feki za kusafiria zenye hadhi ya kibalozi, tukio analodaiwa kulitenda Juni 23, 2010 katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA).

Nzowa ambaye alikuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) na wenzake 13, wanatarajia kutoa ushahidi wao Mahakama Kuu Divesheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu uchumi dhidi ya mshtakiwa huyo.

Hiyo ni baada ya upelelezi wa kesi hiyo kukamilika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na mshtakiwa kusomewa maelezo ya mashahidi na vielelezo (Commital Proceedings).

Abubakari amesomewa maeleo yake leo Jumatatu Desemba 19, 2022 na wakili wa Serikali, Adolf Verandumi akisaidiana na Bahati Jaribu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Romuli Mbuya.

Katika maelezo hayo, mshtakiwa huyo na mwenzake raia wa Guinea Conakry, waliingia nchini Juni 23, 2010 saa 1 usiku kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege la South Afrika Airways.

Wakiwa katika eneo la ukaguzi wa mizigo JNIA, mabegi yao yenye hadhi ya kibalozi (Diplomatic Bags) yalibainika kuwa na vitu vusivyokuwa vya kawaidia.

Walipohojiwa na maofisa kutoka JNIA, walidai kuwa wametumwa na nchi zao kuleta ujumbe Maalumu katika Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) na kwamba siku iliyofuata walitakiwa waende Arusha kupekela ujumbe huo.

Hata hivyo baada ya kufanyiwa ukaguzi wa kina walibainika kuwa na hati feki za kusafiria zenye hadhi ya kibalozi, nyaraka mbalimbali, mihuri feki inavyotumika kugongea nyaraka feki zenye hadhi ya kibalozi.

Maofisa hao wa JNIA walifungua begi moja kati ya mabegi mawili yenye hadhi ya kibalozi na kukuta pakiti 14 za dawa za kulevya aina ya Cocaine zikiwa zimechanganywa na kahawa ndani ya begi rangi nyekundu.

Washtakiwa baada ya kuhojiwa walidai kuwa wao wanasafirisha dawa hizo kutoka Brazil, Peru, Colombia, Trinidad na Tobbaga, Chile na kuletea nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania.

Hakimu Mbuya baada ya kusikiliza maelezo hayo, amesema kuwa kesi hiyo ameihamishia Mahakamani Kuu Kitengo cha Uhujumu Uhujumu uchumi na Makosa ya Jinai kwa ajili ya kupangiwa tarehe ya kuanza usikilizwaji wa ushahidi wa upande wa mashtaka na mshtakiwa anataendelea kubaki rumande kwa kuwa shtaka linayomkabili halina dhamana kwa mujibu wa sheria.

MWANANCHI
 
Aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na dawa za kulevya (ADU), Godrey Nzowa anatarajia kutoa ushahidi katika kesi ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Cocaine zenye thamani ya Sh559 milioni inayomkabili raia wa Liberia...
Miaka 12 Mahabusu,yaani kama ni Pesa itakuwa imeshaisha na kuisha
 
Sasa sielewi miaka yote hiyo walikuwa wanachunguza kitu gani ikiwa watuhumiwa mmewakuta na kidhibiti
 
Hizo dawa za kulevya zilipowekwa mpaka kufikia sasa zimeshaleta zaidi ya hiyo pesa,itakuwa zimeuzwa labda walete unga mpya.

Unaweza kushinda kesi kama kisa kimoja alikamatwa na kilo 1 ya unga kesi ilikwenda baadae unga ukaletwa mahakamani ukapungua gramu nyingi.jamaa kaukataa sio wake.

na ili usishangae kuambiwa unga ume expire
 
Back
Top Bottom