Mashabiki wa Yanga kutoka Comoro watua Dar, waja na boti isiyotumia injini

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
May 25, 2015
6,482
20,428
Baada ya mashabiki wa Yanga kutua Dar kwa kutumia baiskeli wakitokea Mtwara, na mwingine akitokea Kigoma kwa pikipiki, Kali kuliko zote ilikuwa leo asubuhi baada mashabiki 13 wa klabu ya Yanga kufika bandari ya Dar es Salaam wakitokea Comoro.

Mashabiki hao wamewavutia watu waliofika kuwapokea hasa ikizingatiwa ujasiri wao walipoamua kutumia chombo cha mtumbwi kisicho na injini au mashine badala yake walipiga kasia maarufu kama mwiko ili tu wapate kuwaona wababe wa Dar es Salaam wakiwaning'iniza mikia pale Taifa.

Kila la heri Yanga, mabingwa wa kihistoria
 
Picha na video huwa zinapendezesha sana post tatanishi Kama hizi
 
Back
Top Bottom