Mashabiki wa arsenal wahusishwa mlipuko wa bomu

Kintiku

JF-Expert Member
Feb 3, 2011
617
319
Vijana watau walishikiliwa na polisi mjini Damascus baada ya mlipuko wa bomu uliowaua waandishi wawili wa kigeni wiki iliyopita. Ilikuwaje basi?

Baada ya ule mlipuko mkubwa sana watu wengi walipiga mayowe na kukimbia kila mtu anavyoweza, wengi walipata mshtuko wa moyo na kuzirai. Lakini ajabu vijana hawa watatu hakukimbia wakabakia maeneo yale bila woga ki vile na wakaendelea na stori wakishangaa ule mlipuko.

Baada ya hali kutulia polisi waliwaendea wale vijana na kuwaambia lazima wanahusika na ule mlipuko maana wao hawakustuka, kuzimia wala kupiga mayowe. Pia wananchi wengi wakawazonga wale vijana. Baada ya kuhojiwa wale vijana wakasema wao hawakushtuka na ule mlipuko kwa vile wao ni mashabiki wa timu ya Arsenal ya England eti mioyo yao imeshazoea milipuko. Ndugu polisi hebu fikiria timu yetu wiki hii inapigwa tatu bila wiki inayofuata inashinda tano sasa huo moyo si umeshazoea kupanda na kushuka- ndo maana sisi hatukushtuka. Polisi na wananchi waliokuwa wamewazunguka wakaishia kusema kumbe kuna faida ya kuwa shabiki wa The Gunners..................
 
Back
Top Bottom