Masha amekwepa upuuzi, Kitila amekata mzizi wa fitina

W

wandamba

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2014
Messages
357
Likes
637
Points
180
Age
54
W

wandamba

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2014
357 637 180
Baadhi ya viongozi, wasomi magwiji na wachambuzi nguli wa masuala ya kisiasa mara kadhaa wamekuwa wakisema kuwa kubaki ndani ya Chadema kunahitaji maarifa haba, akili fupi na uwezo mdogo wa kufikiri au kupima na kupambanua mambo .

Wanasema hivyo wakidai ndani ya chama hicho kumekosekana mpango mkakati wa kukijenga chama hicho na kuonekana ni taasisi halisi ya kisiasa yenye kuchukua juhudi ya kusaka amana, imani ili kuaminiwa na wananchi au kuvuna kura kwenye uchaguzi Mkuu.

Wadadisi wa mambo ya siasa wanabainisha kuwa ndiyo maana hadi sasa Mwanasiasa Mkongwe nchini Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amekataa katakata kutangaza kama amejiunga na Chadema licha ya kujitoa CCM nyakati za kampeni za uchaguzi Mkuu .

Mzee Ngombale inadaiwa tokea awali akiwa CCM amewahi kukiponda chama hicho na mara kadhaa amenukuliwa akisema hakijatokea chama chenye mfumo wa kisiasa, chenye sera mwanana, oganaizehsheni na miongozo bora.

Mwanasiasa huyo amekipima chama hicho, kukichambua na wakati fulani licha ya kutokuwa mwanachama halisi, amekuwa akimshauri Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akitaka wajiondoe na kutoonekana chama cha kiharakati ili kuwa taasisi kamili.

Ujio wa Waziri wa zamani wa Mambo ya ndani ya Nchi Mwanasheria Lawrance Masha ndani ya Chadema ulisukumwa na hamaki, tamaa ya fahari ya macho kwenye mikutano ya hadhara ya Chadema hatua ambayo inatajwa kuchangia kumpa matumaini hewa na kutaraji pengine Chadema kingeshinda na kuchukua dola.

Mara kadhaa Masha kwa kutumia usomi wake, upana wa maarifa, uzoefu katika siasa na uongozi kila alipojitutumua na kushauri alibezwa, kukwepwa huku baadhi ya wanasiasa wenye uoni mdogo na muhafidhina wakimtenga na kumpuuza.

Wiki mbili kabla ya kufikia uamuzi wake Masha alikuwa na mazungumzo marefu na Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond Edward Lowassa na kumueleza kuwa amefikia maamuzi ya kujiondoa chadema na kufanya shughuli zake binafsi.

Yapo maelezo kuwa Lowasa alimbembeleza na kumsihi sana Masha abatilishe msimamo wake na kutaka awe mwenye subira kwani si muda mrefu chama hicho kitabaki mikononi mwao huku kina Mbowe na washirika wake watakalia benchi kwasababu wameshindwa siasa za mapiku na ushindani.bMasha alimkatalia katakata Lowassa na kusema amechoshwa na upuuzi

Kwa upande Prof Kitila Mkumbo amepitisha maamuzi rasmi ya kujiunga na Chama cha Mapinduzi akiwa Mkoani Singida. Amekuwa mpinzani kwa miaka mingi akitokea Chadema ambapo alikuwa Mshauri Mkuu na Mjumbe wa Kamati kuu.

Piia amewahi kuwa mshauri mkuu na muasisi wa ACT Wazalendo. Profesa Kitila alijiondoa Chadema akiwa na kina Samson Mwigamba, Habib Mchange na Zitto zuber Kabwe baada ya kuzuka mizengwe na kutoridhishwa na mwenendo wa Chadema.

Prof Kitila atakumbukwa kwa uandikaji makala zenye fasihi huku akizibebesha ujumbe wenye muwala pia kuandaa ilani ya uchaguzi ya Chadema ya uchaguzi wa mwaka 2010 iliyomnadi mgombea urais wa chama hicho wakati huo Dr Wilbroad Slaa.

Wachambuzi na wafuatiliaji wa masuala ya siasa wanadai Chadema hakijawahi kuwa na Ilani ya uchaguzi 'realistic , cmprehensive and professional' kama ile ya mwaka 2010 iliondokwa na Profesa Kitila tangu chama hicho kilipoanzishwa .

Profesa Kitila Mkumbo alikuwa miongoni mwa viongozi wa Chadema ambao mwaka 2013 walianzisha vuguvugu la kuhoji uhalali wa Mwenyekiti wao kuingiza kipengele cha kuondoa ukomo wa kugombea nafasi ya uenyekiti katika katiba ya Chadema. Vuguvugu hilo lilipelekea kusukwa mkakati wa siri uliowahusisha kina Zitto Kabwe, Samson Mwigamba na Habib Mchange .

Hata hivyo mpango huo kabambe ulifichuka mapema kabla ya kuanza kwa kamati kuu ya chadema na kujikuta Mbowe akashinda kiubwete uchaguzi na kuwa Mwenyekiti mwaka 2014. Pamoja na kubebeshwa maudhui ya msingi yaliokuwemo kwenye waraka huo, washirika wa Mbowe waliutafsiri na kuuita mkakati wa uasi, usaliti na hujuma dhidi ya chama.

Japo baadhi ya wanachama na viongozi wachache waliwa sifu na kusema hakuna mwenye haki miliki ya nafasi ya uenyekiti wa chama, Mbowe ameendelea kubaki juu ya kiti chake cha urithi toka kwa watangulizi wake kina Mzee Edwin Mtei na marehemu Bob Nyange Makani

Katika siasa za vijembe na propaganda, Prof Kitila atakumbukwa kwa kuwapachika jina wafuasi wa Chadema akiwaita Nyumbu huku akiwalinganisha kitabia na wanyama pori waitwao Nyumbu ambao hutembea, kula, kusafiri na kukaa kwa makundi.

Nyumbu anaaminika ana akili ndogo sana katika kufikiri na kutenda. Profesa Kitila amesisitiza kuwa, Nyumbu hufuata nyayo bila kuhoji, hushangilia akiambiwa ashangilie na hukimbia akiona wa mbele yake anakimbia. Jina Nyumbu limeseelea kutumika tangu enzi hizo katika siasa za utani na kutupiana matani.

Huenda Prof Kitila tangu awaite Chadema ni kama kundi la Nyumbu hakuwahi tena kulirudia jina hilo, lakini kauli yake moja ya siku moja ilisambaa mithili ya moto unaowaka nyikani na kuteketeza misitu minene

Kwa sasa Prof Kitila ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji. Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk John Magufuli aliuona uwezo wa Profesa Kitila akaona ipo haja ya kumruhusu aitumikie Serikali kwa kumpa nafasi ya juu ya kiutendaji. Kabla ya hapo, kwa miaka mingi Prof Mkumbo alikuwa mhadhiri katika chuo kikuu cha Dar es Salaam kitivo cha elimu akiwa amebobea katika masomo ya saikolojia ya elimu.

Ujio wa Prof Kitila Mkumbo katika chama cha mapinduzi haukushtua sana, maana tayari Watanzania walishaonaiona azma ya wazi ya mwanasiasa huyo msomi kutaka kumsaidia Rais na Serikali yake ya awamu ya tano.
 
Malcom Lumumba

Malcom Lumumba

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Messages
12,367
Likes
33,392
Points
280
Malcom Lumumba

Malcom Lumumba

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2012
12,367 33,392 280
Azma ya kutaka kumsaidia raisi au azma ya kujipendekeza miksa unafiki humo humo
Lakini mwisho wa siku ana haki ya Kikatiba kufanya hivyo.
Huu ni ukweli ambao hatuwezi kuukataa (The Penumbra of Human Rights)
 
1000 digits

1000 digits

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2012
Messages
3,670
Likes
2,635
Points
280
1000 digits

1000 digits

JF-Expert Member
Joined Oct 16, 2012
3,670 2,635 280

Lipi rahisi na lenye manufaa kwa binadamu anayependa maisha ya raha na ukubwa :
Kujiunga na chama ambacho mwenyekiti wake ni Rais wa nchi na anayeweza kukuchagua uwe katibu mkuu wa wizara / nafasi yoyote anayoona inafaa au kubaki upinzani ambapo hakuna chochote zaidi ya kupambana mpaka upate hata huo ujumbe wa nyumba kumi unaweza unaweza ukachezea vitasa vya dola kabla ya kutangazwa mshindi.
Kurudi CCM sio ujasiri ni kurudi kwenye malisho bora.

CCM sio kwamba ina mfumo mzuri bali ni kwa sababu mwenyekiti wake huwezi kumtofautisha kirahisi na mungu huku dunia kwa mamlaka aliyo nayo kupitia katiba ya nchi.

Mtu Kutoka CCM chama ambacho mwenyekiti wake ameshika funguo za hazina na kujiunga na upinzani inahitaji ujasiliri na imani kubwa sawa na ile ya Yesu kutoka mbinguni kuja kufa msalabani ili kuwaokoa wanadamu.
 
F

Fitinamwiko

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2012
Messages
4,808
Likes
257
Points
180
F

Fitinamwiko

JF-Expert Member
Joined Aug 13, 2012
4,808 257 180
Nakwenda Zimbabwe
 
Madrid86

Madrid86

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2015
Messages
1,333
Likes
641
Points
280
Madrid86

Madrid86

JF-Expert Member
Joined Jul 12, 2015
1,333 641 280
Time will tell.
 
UmkhontoweSizwe

UmkhontoweSizwe

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2008
Messages
3,592
Likes
729
Points
280
UmkhontoweSizwe

UmkhontoweSizwe

JF-Expert Member
Joined Dec 19, 2008
3,592 729 280
Dr Kitila ndo alikuwa hazina ya kufikiri (think tank) ya chadema, toka ameondoka hakuna lolote jipya ambalo chadema have come up with. Ukichanganya na kuondoka kwa Dr Slaa (dr wa ukweli!) ndo ikawa mwisho wa mambo yote. Chadema kwishiney. ....!
 
bendaki

bendaki

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Messages
954
Likes
153
Points
60
bendaki

bendaki

JF-Expert Member
Joined Feb 5, 2013
954 153 60
Be realistic hata wewe mleta hoja.

1. Kuna chama cha siasa kukaa kama taasisi hapa Tanzania? Tulianza na chama kimoja na kilichokuwa kimeshika hatamu. Jiulize kushika hatamu ndio nini? Unaweza kutofautisha chama na serikali kuwa ni kipi ni taasisi katika mazingira ya chama kuwa kimeshika hatamu? Kama utakuwa huwezi utajuaje ni kipi kilichokaa kama taasisi chama au serikali?

a) Wakati huo ndipo CCM ilijimilikisha mali nyingi zilizokuwa mali za umma kama ardhi, viwanja vya michezo, mahoteli, majumba kadhaa ambayo hadi leo ni mali zake. Iliwatumia watu kwa njia mbali mbali zikiwa halali na zisizo hali kuboresha mali hizo lakini kwa kukosa mikakati kwa kuwa hakuna utaasisi unaosemwa na mleta hoja hivyo vyote vimekosa mwendelezo (Angalia viwanja vya michezo hasa mpira ambavyo CCM kwa pupa ilivichukua havifai na vin fifia kila kukicha)

b) Baada ya vyama vingi CCM imeendelea kuwa na mawazo mgando ya kuwa itaishi katika maisha ya vyama vingi maana katiba ilibidi kubadilika, lakini itatenda kwa nguvu ya chama kimoja na kushika hatamu. Faida yake kwa chama hiki ni nini? kupata vya bure na vya bure vikikosa ni kupiga madili na madili yakishindikana ni kufisadi.

- Katika kujifanikishia haya inakataa katiba mpya na mara zote inataka katiba ya 1977 iwe ndio ya maisha. Utawasikia kuwa CCM iishi milele, jiulize kwa nini milele?

- Iwe imeshinda au haikushinda uchaguzi fulani inalazimisha itangazwe yenyewe. Hapa wamejitahidi kuhodhi vyombo vya kusimamia na kutangaza washindi, hapa utaasisi uko wapi? Wanalazimisha kumiliki taasisi ya urais, ubaunge na mahakama.

- Demokrasia kwao ni kuchagua na kuchaguana. Lakini ni wapi wanaonyesha kuwa demokrasia inaonekana katika maisha ya watanzania kuwa demokrasia inatendeka? Kama mtu mmoja anahodhi maisha ya maamuzi yote ya watu mil 50 hapo kuna kuonekana demokrasia ikitendeka?

Kama kuna mengi ambayo Watanzania wangependa kuyaamua wao lakini bila kutaka kwao kuna mtu mmoja au watu kadhaa ndio wanawaamulia watake wasitake hapo kuna demokrasia? Na je hiyo ndio taasisi ya kutolea mfano?

Mifano ya hayo ni mingi: Kama watanzania wangeulizwa la kuanzia katika umaskini walio nao wasingependa kuanza na kununua ndege (Bomberdier). Katika ununuzi wa ndege hamukuwa na demokrasia na demokrasia inakosa kwa kuwa na watawala katika chama chao kukosa utaasisi. Kuna uwanja wa ndege Chato, kusimamishwa mambo yaliyowekwa kikanuni kama sherehe za uhuru nk. Matumizi ya fedha kama za sherehe hizo nk.

Hayo yote ni viashiria vya kukosa utaasisi katika chama kinachotawala.

2. Hoja ya kuwa kulikuwepo na uaandikaji wa ilani nzuri na comprehensive. Huwa kuna ilani Tanzania? Kama ilani huwa inakuwepo ni nini kinasababisha nchi tajiri kama hii kwa miaka zaidi ya 55 ni maskini kiwango hiki?

Usomi katika siasa za Tanzania ni usanii tu. kama Kitila alikuwa au anautumia usomi basi ni usanii wa kisomi na hakuna kitu. vyote hivi havipo kwa kuwa CCM ni kichaka cha dhuruma kwa Watanzania nyuma ya kisingizio cha wasomi.

Wasomi wa kitanzania wanajidai kukimbilia siasa ili maisha yao yawe mazuri, ukweli hawakimbilii siasa bali wanakimbilia CCM ili maisha yao yawe ya kupata visivyo hitaji waliyoyasomea bali watayoyazoa mbele ya safari. Ndio maana Masha amerudi CCM baada ya kukuta CHADEMA hamna usanii, Ujiko na madili yanayopelekea kufisadi.

Kwenda CHADEMA inakubidi usiwe na uhitaji wa kwenda kuvuna huko bali kwenda kuonyesha mabadiliko yanatokea kwa watanzania. Watu kama Kitila wasingeweza kudumu CHADEMA. Lowassa CHADEMA atakaa sana maana hana njaa.

3. Hoja ya kuwa huko CHADEMA wasomi wazuri hawawezi kukaa na kuonyesha umakini wa usomi wao, hilo sio kweli. Nani kama Baregu kwa usomi? Lissu? Wapo na wanaonyesha kiwango kikubwa cha usomi wao.
Wasomi wengi ni wachumia matumbo, kukaa Chadema kwa kutarajia kuchuma kirahisi kama CCm ni sawa na msemo wa ngamia kupenya katika tundu la sindano.
 
X

xaracter

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2015
Messages
976
Likes
550
Points
180
X

xaracter

JF-Expert Member
Joined Jul 28, 2015
976 550 180
Hata wakoloni walikuwa na mawazo kama ya wana ccm.
 
tindo

tindo

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2011
Messages
15,551
Likes
19,549
Points
280
tindo

tindo

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2011
15,551 19,549 280
Dr Kitila ndo alikuwa hazina ya kufikiri (think tank) ya chadema, toka ameondoka hakuna lolote jipya ambalo chadema have come up with. Ukichanganya na kuondoka kwa Dr Slaa (dr wa ukweli!) ndo ikawa mwisho wa mambo yote. Chadema kwishiney. ....!
Naunga mkono hoja zako, je risasi za nini sasa?
 
cocochanel

cocochanel

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2007
Messages
21,700
Likes
63,497
Points
280
cocochanel

cocochanel

JF-Expert Member
Joined Oct 6, 2007
21,700 63,497 280
Dr Kitila ndo alikuwa hazina ya kufikiri (think tank) ya chadema, toka ameondoka hakuna lolote jipya ambalo chadema have come up with. Ukichanganya na kuondoka kwa Dr Slaa (dr wa ukweli!) ndo ikawa mwisho wa mambo yote. Chadema kwishiney. ....!
Kabisaaaaaa

Ilisha kwishney..
Wanajijua bali matumbo kwanza.. chama hawajali kilivyo.
 
1000 digits

1000 digits

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2012
Messages
3,670
Likes
2,635
Points
280
1000 digits

1000 digits

JF-Expert Member
Joined Oct 16, 2012
3,670 2,635 280
Dr Kitila ndo alikuwa hazina ya kufikiri (think tank) ya chadema, toka ameondoka hakuna lolote jipya ambalo chadema have come up with. Ukichanganya na kuondoka kwa Dr Slaa (dr wa ukweli!) ndo ikawa mwisho wa mambo yote. Chadema kwishiney. ....!

Hao masink tank kwa nini hawaanzishi vyama vyao kwa hayo wanayofikiri kuwa yanamuelekeo?

Tangu kuumbwa kwa ulimwengu mageuzi ama kwa vita au kwa falsafa hayajawahi kuletwa na wasomi.
Mageuzi yanaanzishwa na watu wa kawaida wanaoona kuwa wanakosa haki zao hata zile ndogo.

Ukiona mtu alianza kuwaza namna ya kutengeneza gari la kutumia Engine ujue kuwa hakua mfalme bali mlala hoi asiyekua na uwezo wa kumiliki farasi au kuwa na zizi la farasi wa kubadilisha mara kwa mara au alichoka kutumia farasi kutokana na mahitaji yake.
 
Moisemusajiografii

Moisemusajiografii

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2013
Messages
10,529
Likes
9,096
Points
280
Moisemusajiografii

Moisemusajiografii

JF-Expert Member
Joined Nov 3, 2013
10,529 9,096 280
Dr Kitila ndo alikuwa hazina ya kufikiri (think tank) ya chadema, toka ameondoka hakuna lolote jipya ambalo chadema have come up with. Ukichanganya na kuondoka kwa Dr Slaa (dr wa ukweli!) ndo ikawa mwisho wa mambo yote. Chadema kwishiney. ....!
Acha kukariri kama sungura weye kiumbe. Ndiyo ninyi huwa mnabisha kuwa mkila wali hamshibi hadi muongezee ugali.
 
B

bne

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2016
Messages
1,506
Likes
1,498
Points
280
B

bne

JF-Expert Member
Joined Oct 11, 2016
1,506 1,498 280
Kinachoifanya ccm isimame kama taasisi ni dola lkn nje ya dola ccm sio taasisi na itayeyuka kama moshi wa kifuu.
Mfano wa ccm ni KANU ya Kenya. Nje ya dola hakuna chama,
Usidanganye watu hapo hakuna utasisi Bali ni kundi la watu kwenye mkusanyika la ulaji Bali bila dola hilo kundi hutaliona tena.
Unamzungumzia kitila aliyerudi ccm baada ya kupewa cheo, yaani wewe kwa upeo wako mdogo huwezi kujiuliza haya hilo? Kwamba kwann arudi baada ya kupewa cheo na si kabla ya hapo.
Mwisho mm naona mawazo yako ni mfu yenye lengo la kukatisha tamaa ili wote tuwe
 
J

Jaimee

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2017
Messages
2,463
Likes
1,514
Points
280
J

Jaimee

JF-Expert Member
Joined Aug 4, 2017
2,463 1,514 280
Hivi kama chadema hawana mkakati wa kukuza chama kwahiyo suluhisho ni kurudi katika chama ambacho ulikiona hakifai? Sasa hapo utakuwa umetatua nini? au ndiyo ule uvivu wa kufikiri?Au ndiyo ile njaa ya madaraka? Acheni upuuzi, hakuna critical thinking katika hoja iliyopo mezani, labda kwa watoto wa chekechea!
 
64gb

64gb

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2013
Messages
919
Likes
1,581
Points
180
64gb

64gb

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2013
919 1,581 180
Ni heri ukamwamini mlevi na mtoto mdogo kuliko kumwamini mwanasiasa
 
DOUGLAS SALLU

DOUGLAS SALLU

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2009
Messages
15,710
Likes
8,170
Points
280
DOUGLAS SALLU

DOUGLAS SALLU

JF-Expert Member
Joined Nov 13, 2009
15,710 8,170 280
Dr Kitila ndo alikuwa hazina ya kufikiri (think tank) ya chadema, toka ameondoka hakuna lolote jipya ambalo chadema have come up with. Ukichanganya na kuondoka kwa Dr Slaa (dr wa ukweli!) ndo ikawa mwisho wa mambo yote. Chadema kwishiney. ....!
Kama imekwisha bunduki na mabomu ya nini tena? CCM bila mbeleko ya polisi na NEC ni sawa na genge la wasaka tonge tu.
 
J

Jaimee

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2017
Messages
2,463
Likes
1,514
Points
280
J

Jaimee

JF-Expert Member
Joined Aug 4, 2017
2,463 1,514 280
Eti wasomi wamesema! Wasomi gani? Tumepambana sana kufuta ujinga,lakini tukasahau kufuta upumbavu. Asilimia kubwa ya wasomi wa kiafrika wameshindwa kuleta maendeleo endelevu ktk nchi zao.
 
Forum statistics

Threads 1,250,443
Members 481,342
Posts 29,733,174