Masasi: Nyumba ya mbunge, magari 20, trekta vyachomwa moto... Watu wawili wadaiwa kuuawa!

Kwa vyovyote vile yawezekana wako mafichoni, wanasubiri watu wa masasi walale usiku ili wawakamate moja baada ya mwingine. Ila nadhani karibu 90% ya vijana wa Masasi leo watalala uhamishoni Msumbiji.
Kwanza hawa sio watanzania ni wa mchumbiji hawa tuwafukuze
 
nilikuwa Msemo Hotel (mjini Mtwara) mchana wa leo, Nikamuona Chagonja na RPC wa Mtwara wakiwa wanakula kuku kwa juisi. Nikajiuliza, Hivi viongozi wa NGAZI ZA JUU WA JESHI LA POLISI wako hapa wanatumbua kuku, Kama ingekuwa wanaokufa kule Masasi wangekuwa ni wazazi na ndugu zao je wangekuwa hapa mda huuu wakitumbua kuku?
Yaani hii serikali ni ya mashetani kweli!
Newton's Third Law of Motion states "To every action, there is an equal and opposite reaction" Hivyo basi haya yanayotokea hapa Mtwara na Masasi na kwingineko ni analogous to This Newton's law of motion
 
Magari 18,pikipiki 7 yateketezwa kwa moto.vyote vikiwa ni mali za halmashauri ya masasi na baadhi ni vya watumishi wa halmashauri hiyo.

Inasikitisha. Raisi yuko wapi ? Makamu wa raisi yuko wapi ? waziri mkuu yuko wapi ? viongozi wa chama wako wapi ? waziri wa mambo ya ndani yuko wapi ? Nape na Mwigulu wanasemaje ?
 
Sasa tunaelekea kusiko, mwanza cheche zilianza masasi nako ndo hali kama hiyo, morogoro nako mm nianze kujitayarisha pa kukimbilia pamoja na familia yangu!

Hakuna haja ya kukimbia saa ya ukombozi imekwisha fika!.
 
mie nadhani suluhisho la kuchoma magari na nyumba za halmshauri si zuri cha kufanya ni maandamano yasiyokuwa na uharibifu, cha kukatisha tamaa ni pale vyombo vya usalama vikianza kufanya upekuzi wao wengi wataangamia mikononi mwa polisi na hakuna atakaewatazama na kuwaonea huruma
 
Rais yuko nje ya nchi, Makamu wa rais hajulikani aliko, Waziri mkuu yuko busy na graduation ya DIT, Secretariat ya CCM wanakata mayenu-Kigoma!

Tuna tatizo kubwa! Na katika vyote, nimeshangazwa sana na kitendo cha team ya Kinana kujitangaza TBC (wanacheza mayenu) huku Masasi kuna mgogoro mzito!
 
Kwanza hawa sio watanzania ni wa mchumbiji hawa tuwafukuze
Ebu yachunguze tena maandishi yako haya...ila kumbuka lazima uwe na ushahidi ili kudhibitisha kuwa fulani ni raia ama la.

Vinginevyo kama umeandika haya ili kuvuruga uzi huu sikubaliani na wewe uzi huu uvurugwe !
 
Hivi vipofu kama wewe bado wapo tu ndani ya taifa hili au ndio njaa ileile

hata mie namshangaa huyu button za pc yake anazibonyezea bongo kweli?wamakonde wameanzisha wimbo tz nzima tunajiandaa kuitikia chorus,yeye sijui yuko wapi!
 
Jicho langu la tatu limeusoma huu mtifuano wa mtwara kwa namna tofauti ...kwa mbali nauona ni mpango ulioandaliwa na usalama wa taifa kwa dhamira fulani lakini inaonyesha kunampasuko mkubwa kati yao kwa maana ya wengi wao kutoridhika na mwenendo wa serikali hivyokupelekea kuwaacha wananch wazitekeleze dhamira zao ili waufikishe ujumbe kwa serikali husika.Ifahamike wanufaika wa huu mfumo tata ni wachache kuliko wanaoteseka ...Nowadays police, Jeshi,walimu,wastaafu,wanafunzi hadi raia wakawaida wamepoteza matumaini na serikali yao so hii ni dalili ya hatari kwa serikali ...Binafsi ctaki kuamini kama jeshi lilishindwa kuwadhibiti waandamanaji huko mtwara...( mtizamo binafsi ).
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Ongezeni bidii kuigeuza nchi hata kama ni kwa kumwaga damu... si mtwara tu, hata mwanza, tabora, kigoma, dsm na kwingineko anzeni...

Taifa halitatawalika lini.......... Kwa sababu zipi......... Kwa manufaa ya nani?.

Ni rahisi sana kukaa kwenye keyboard na kuanza kutema ushuzi kama mtu anaeamulisha mbwa kwenda kubwata.

If your really up for fight, come down to ground zero.

I'm really sorry for those people lost their life in vain.
 
No way CCM inabidi iondoke tu madarakani..... tena washiriki vizuri namna nzuri ya kuachia madaraka....
Wananchi wakifikia namna hii....utailipua nchi bure!!!
CCM acheni kubana wananchi, upinzani hili ndilo suluhisho.....
 
Yale ya Misri na Tunisia yanaweza kutokea kabisa huku kwetu kwa hali hii ilivyo.
 
Duh! Shughuli ya Prof. Bila shaka sasa amefurahi na roho yake. Kweli tunatakiwa tuongeze shule kata Mtwara na Lindi maana hizi nanii medium school haziusaidii.
 
The fact remains the government should sit down and lay down strategies to cub down the commotion japo nawaunga mkono wanakusini kuwa umeme wa gesi kwanza ujitosheleze kusini kabla ya kuelekea kwingineko.
 
JF imekuwa kama kilabu cha pombe za kienyeji. Jii mada imeanza tu blah blah blah watu wameuawa, zinafuata shutuma nyiiingi kwa serikali na polisi, sawa. Mbona asipatikane mtu wa kueleza ni nini kimetokea?

Naona tu hapo kwamba fujo zimeanzishwa na boda boda, sasa hao bodaboda kama wameanzisha fujo na kuuana, hilo linahusianaje na serikali?

Hebu apatikane shuhuda anieleze na mimi nielewe tunung'unike pamoja jamini
 
Back
Top Bottom